Mbunge wa Mwibara (CCM) apoteza kiti

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Kuna kila dalili kwamba mbunge wa Mwibara kwa tiketi ya CCM bwana Kajege atavuliwa kiti chake cha ubunge punde. Taarifa zaidi zitawajia.
 
Kulikuwa na kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Mwibara iliyokuwa inasikilizwa na Jaji Francis Mchome. Kesi hiyo ilikuwa inataka kutengua matokeo ya uchaguzi wa jimbo kufuatia madai mbalimbali yakiwemo matumizi ya vyombo vya serikali kwenye uchaguzi huo. Nadhani leo ilikuwa ni hukumu na anachosema Paparazi yawezekana ni matokeo ya hukumu hiyo.

M. M.
 
Paparazi yuko offline itakaa hapa kwa muda au itaenda kwenye Nyepesi kama hakuna more details.
 
Ole, iweke kama Breaking News:Mbunge wa Mwibara apoteza kiti. Ni habari za uhakika na nimezithibitisha toka Musoma. Ni kweli aliyekuwa mgombea wa TLP ameweza kujenga hoja mahakamani na ameshinda na mahakama imeona kuwa Mbunge Charles Kajage hakuchaguliwa kihalali.
 
1390.jpg

aliyekuwa Mbunge wa Mwibara Charles Kajage (CCM)
 
si unajua tena KLH ni mtandao mkubwa.. kwa kushirikiana na JF of course.. (nyani don't even think.. LOL)
 
Kulikuwa na kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Mwibara iliyokuwa inasikilizwa na Jaji Francis Mchome. Kesi hiyo ilikuwa inataka kutengua matokeo ya uchaguzi wa jimbo kufuatia madai mbalimbali yakiwemo matumizi ya vyombo vya serikali kwenye uchaguzi huo. Nadhani leo ilikuwa ni hukumu na anachosema Paparazi yawezekana ni matokeo ya hukumu hiyo.

M. M.

Jaji huyu ndio jaji aliemng'oa Azim Premji Kigoma mwaka 1994. Mnakumbuka kesi ile? Hana mchezo Jaji huyu.
 
Hili fundisho tu, avumaye baharini papa kumbe wengine kibao wapo.The electoral process is plagued with corruption, inabidi kuwaumbua zaidi na zaidi pamoja na kuelimisha wananchi ili kujenga a credible electoral process.
 
Jaji huyu ndio jaji aliemng'oa Azim Premji Kigoma mwaka 1994. Mnakumbuka kesi ile? Hana mchezo Jaji huyu.

sawa kabisa! kuna wakati tunaweza kuwa na wasiwasi na vyombo vyetu lakini mara nyingi nimekuwa nikiamini sana Mahakama Kuu na ya Rufaa katika mambo mengi kuliko mahakama nyingi za chini. Na upande mmoja ni kuwa wapo majaji na mahakimu ambao bado wanaangalia ushahidi na wanaofuata kokote utakakowapeleka.
 
Jaji huyu ndio jaji aliemng'oa Azim Premji Kigoma mwaka 1994. Mnakumbuka kesi ile? Hana mchezo Jaji huyu.

Huyu JAJI naona anafaa kukabidhiwa faili zoote za kesi za kupinga matokeo ya ubunge, coz ndani ya Bongo kushinda kesi ya matokeo mahakamani tena ikiwa mlalamikaji mpinzani, sio mchezo babake!
Tumeona JAJI wengi hapa ukereketwa mbele sheria baadae.
 
Sasa Upinzani hilo ndilo jimbo la kujipima nguvu mpya. Itabidi muhamishie majeshi yote huko.

Vipi yule mbunge wa TLP aliyepoteza ubunge Kagera, uchaguzi lini?
 
Jaji huyu ndio jaji aliemng'oa Azim Premji Kigoma mwaka 1994. Mnakumbuka kesi ile? Hana mchezo Jaji huyu.

Kama huyu jaji ni kiboko yao je kuna uwezekano akikabidhiwa ya le mafaili ya ile kesi ya rushwa ya Radar na yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, au jamaa wataogopa?
 
wako slow.. habari zinakuja JF kwanza wengine wanafuata!!! we taste the food before it is taken to the table!
 
Back
Top Bottom