Kama wana Mtwara, waliandamana kwa ridhaa yao wenyewe bila kuchochewa, huku mbunge wao akiwa nyuma yao, pembeni yao pamoja nao!, then mbunge wao ndio naye sasa amekamatwa na kama ataunganishwa na kushtakiwa, then Mtwara hapata kalika na bomba la gesi halita jengeka!.
Ila kama ni kweli walichochewa na wachochezi ndio hao waliotiwa mbaroni na kushitakiwa, then wachochezi hawa watakuwa wameshikishwa adabu!, Mtwara itakuwa shwari, bomba la gesi litajengwa bila vikwazo vyovyote na gesi itasafirishwa kuletwa Daslam ambako ndiko waliko wanaojua kuitumia hiyo gesi!.
Huko nyuma niliwahi kusema " you can never miss what you never know!", kwani Wa Mtwara wanaijua gesi?, wamewahi kuitumia?, wamewahi kuwa nayo?, how could they miss something they never had?!. Hawa walichochewa tuu!, wao wamezoea kuni!, waendelee kutumia kuni, ila gesi watuachie sisi wa mujini tuliozoea!.
Mtwara na Lindi ni CCM strong hold, wako very loyal kwa chama chao, ndio maana sasa wametulia tuli baada ya wachochezi kukamatwa!.
Wachochezi wote washikishwe adabu!, and soon inakuja sheria mpya ya cyber law, hata "hawa wachochezi wetu humu jf!", watashikishwa adabu!.
Kidumu chama cha Mapinduzi!.
Pasco.