Kama sikosei huyu mbunge alijitahidi sana kuwasilisha kero za wananchi wake kwenye kikao cha bunge la bajeti mwaka huu, lakini kukawa na usanii wa kiaina akazimwa! Na kuna kipindi aliweka wazi kuwa wananchi wake walimwambia kama hakupata ufumbuzi wa kero zao basi asirudi. Sasa, ameamua kusimama na wananchi, tatizo ukiwa ccm unatakiwa usimame na wawekezaji na sio wananchi!
Hofu yangu kwenye hili ni kwamba kama ccm na serikali yake hawakuwa makini, Mbarali kunaweza kuwa kubaya kuliko Nyamongo. Matatizo ya Mbaralali ni ya muda ,mrefu lakini cha ajabu badala ya serikali kutatua wamezidi kupalilia mgogoro kwa kuwapa nguvu wawekezaji. Huyu Mbunge ana kesi na ccm wanaweza kumuewekea mizengwe (kupitia mahakama au tume ya uchaguzi) ili asiweze kugombea (kama ni kweli kahama chama inabidi uchaguzi mdogo ufanyike maana ubunge kupitia ccm unakuwa umekoma).