Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

View attachment 1441653

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi kwa tuhuma za kukutwa na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyara za Serikali
==

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Masoud Suleiman maarufu Suleiman Nchambi (CCM) kwa tuhuma za kupatikana na silaha 10, risasi 536 na nyama zinazodhaniwa kuwa ni za wanyawapori kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Mei 6,2020, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3,2020 majira ya saa sita kasoro usiku katika mtaa wa Lubaga kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

“Mei 3,2020 majira ya sita kasoro usiku Kikosi kazi cha askari wa upelelezi kikiongozwa na Kaimu Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi kwa kushirikiana na Afisa wa Wanyamapori mkoa wa Shinyanga Perfect Mbwambo walifanya upekuzi kwenye makazi ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa Mheshimiwa huyo alikuwa akifanya uwindaji haramu kwenye eneo la Negezi wilayani Kishapu akiwa na gari yenye namba za ujasili T760 DSD Nissan Hard Body”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Katika upekuzi huo walifanikiwa kukamata nyama iliyodhaniwa kuwa ni wanyamapori yenye uzito wa kilogramu 35 zikiwa zimehifadhiwa kwenye jokofu lililokuwa jikoni,jingine sehemu ya mazoezi na nyama nyingine ilikutwa kwenye gari hilo likiwa limeegeshwa nyumbani kwake ndani ya uzio wa nyumba hiyo”,amesema Kamanda Magiligimba.

“Katika gari hilo kulikutwa silaha moja aina ya shortgunWakati askari hao wakiendelea na upekuzi ndani ya chumba chake cha kulala zilipatikana silaha zingine za aina mbalimbali na kufanya jumla ya silaha zilizokamatwa kuwa 16 ambazo ni Airgun 3, Shortgun 3,Rifle 8, Pistol 1 na Mark IV 1 pamoja na risasi 536 zikiwa kwenye kabati la nguo",anaeleza Kamanda.

“Baada ya uchunguzi wa awali iligundulika kuwa silaha 10 ambazo ni Airgun 2, Rifle 5, Shortgun 2 na Mark IV 1 kati ya 16 anazimiliki isivyo halali”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema nyama hizo zimepelekwa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na gari husika limekamatwa.

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Natoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kumiliki silaha isivyo kihalali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema Kamanda Magiligimba.
Hii itaisha tu kama ya Akram mdogo wake Rostom Aziz tu,stay tuned

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilidhani Wabunge wanaoonekana hawafai ni wa Upinzani pekee na CCM wote ni Malaika kumbe hata Kwao kuna Vitimbi?
Ngoja nikupe elimu kidogo.

Tunaelekea kwenye uchaguzi hapo Oktoba, 2020.
Kuna wengine nao wanataka kula, ni lazima iwepo njia ya kuachiana ulaji.

Umeelewa?

Sijasema hao wanaotafuta ulaji ni wasafi kuliko huyo wanayemwondoa njiani.
 
Huyo wanajua siku nyingi kuwa ni jangili lakini analindwa na system kwani ndio wafadhili wa CCM.
Ukiona hivyo ujue CCM imepata mtu mwingine wa kumpa Ubunge hivyo lazima wamuondoe kwa maovu wayajuayo.
Style ya CCM ni kuwalinda wafadhili hata wawe wanakula nyama za watu, lakini siku wakikuchoka na kutaka kumpa kiti hicho mwingine basi lazima wakufanyizie tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
ndugu jadili uovu wa mtu.chama cha mapinduzi kinahusikaje mkuu.chama sio kibaya,mbaya mtu. Jadilini hilo jangili. CCM isihguswe kabisa
 
Hao ndiyo wagonga meza mahiri wakiwa bungeni.

Linatoka Chama Cha Majambazi.
 
Wazee wa uwindaji, huo mzigo wa silaha kama ana miliki kitalu cha uwindaji😂😂
 
Huyu ni mwenzetu hivyo hii kesi itakuwa nyepesi sana... Tutakachofanya ni kusubiri kelele za mitandaoni zipoe

Ni sawa tu.Si hata yule aliyekuwa kamanda aliyekamatwa na vitambulisho vingi sana feki vingine vya maafisa kule Arusha sijui walimwitaga olembaya mwisho si alipelekwa Juu.Yule mwingine naye tulimwona humu walimwita naye Mujusi wa kuteleza si nae ni hao hao.Serikali kuweni macho,wanatumaliza hawa wakijificha kwenye maji ya kijani na njano.Sio wenzenu hao Jr
 
Hakuna kesi hapo atatoka tu na ataendelea na majukumu yake kama kawaida

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hii awamu, sio.Labda afanyeje, na sisi tunalifuatilia tujue mwisho wake na silaha zetu zimerudi na haki ya wanyama waliouawa inapatikana.Humu yapo mengi.Tunasubiri kusikia Mwizi mwingine wa silaha aliyeonekana humu na kuwatesa sana wakazi wa ngarenaro Arusha Kamanda wa vijana Mujusi tujue nae yamepaaishwa au yamezamishwa.
 
Kwa hii awamu, sio.Labda afanyeje, na sisi tunalifuatilia tujue mwisho wake na silaha zetu zimerudi na haki ya wanyama waliouawa inapatikana.Humu yapo mengi.Tunasubiri kusikia Mwizi mwingine wa silaha aliyeonekana humu na kuwatesa sana wakazi wa ngarenaro Arusha Kamanda wa vijana Mujusi tujue nae yamepaaishwa au yamezamishwa.
Huyu alikuwa ana kesi ya kutoa rushwa biharamulo 2018 kuna mtu alimgusa kesi iko wpi??kangi je si alikamatwa kwa kuomba rushwa na uwaziri akapewa au ilikuwa awamu ya kwanza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mmoja ni marehemu kwa sasa,niliwahi kutana naye miaka ya nyuma huko Kilombero,nikaambiwa alilazwa siku tatu kwenye jeneza. Hawa jamaa ni washirikina,wezi,majangili,waongo,wazinzi,wanafiki na wauaji wakubwa. Kiujumla hawa ni wafuasi wa yule jamaa aliyetupwa duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Duhh! Ni nani alietupwa hapa duniani mkuu!
 
Back
Top Bottom