Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

Tumbo linahusika na si kichwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hassani ngoma anapwaya sanaa, kwanza anashindwa kutambua kuwa Baby kabae ni moderator pale yeye anabishana nae kam anabishana na mkewe nyumbani kwake alafu anaropoka sanaa haongei kwa mpangilio nadhani apellekwe kwenye power breakfast kwa akina gea habibu.

anashindwa kuwa very proofesional hivi hata ukiangalia uchambuzi wa habar wanazungumza tu kijinga jinga.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1441653

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi kwa tuhuma za kukutwa na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyara za Serikali
==

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Masoud Suleiman maarufu Suleiman Nchambi (CCM) kwa tuhuma za kupatikana na silaha 10, risasi 536 na nyama zinazodhaniwa kuwa ni za wanyawapori kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Mei 6,2020, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3,2020 majira ya saa sita kasoro usiku katika mtaa wa Lubaga kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

“Mei 3,2020 majira ya sita kasoro usiku Kikosi kazi cha askari wa upelelezi kikiongozwa na Kaimu Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi kwa kushirikiana na Afisa wa Wanyamapori mkoa wa Shinyanga Perfect Mbwambo walifanya upekuzi kwenye makazi ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa Mheshimiwa huyo alikuwa akifanya uwindaji haramu kwenye eneo la Negezi wilayani Kishapu akiwa na gari yenye namba za ujasili T760 DSD Nissan Hard Body”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Katika upekuzi huo walifanikiwa kukamata nyama iliyodhaniwa kuwa ni wanyamapori yenye uzito wa kilogramu 35 zikiwa zimehifadhiwa kwenye jokofu lililokuwa jikoni,jingine sehemu ya mazoezi na nyama nyingine ilikutwa kwenye gari hilo likiwa limeegeshwa nyumbani kwake ndani ya uzio wa nyumba hiyo”,amesema Kamanda Magiligimba.

“Katika gari hilo kulikutwa silaha moja aina ya shortgunWakati askari hao wakiendelea na upekuzi ndani ya chumba chake cha kulala zilipatikana silaha zingine za aina mbalimbali na kufanya jumla ya silaha zilizokamatwa kuwa 16 ambazo ni Airgun 3, Shortgun 3,Rifle 8, Pistol 1 na Mark IV 1 pamoja na risasi 536 zikiwa kwenye kabati la nguo",anaeleza Kamanda.

“Baada ya uchunguzi wa awali iligundulika kuwa silaha 10 ambazo ni Airgun 2, Rifle 5, Shortgun 2 na Mark IV 1 kati ya 16 anazimiliki isivyo halali”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema nyama hizo zimepelekwa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na gari husika limekamatwa.

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Natoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kumiliki silaha isivyo kihalali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema Kamanda Magiligimba.
Huyu mbunge ni mwindaji au ni jangili la kuuwa wanyama? Au an kampuni ya kuuza silaha? Kama Yuko karibu na national park Basi amemaliza wanyama porini.
 
Wanafanya hata huyo Babie Kabaye aonekane pwagu ty kumbe dada ana madini mengi tu.
 
Ngoma ni mdini sana!

Hata wakati wa Prof Assad vs Ndugai alikuwa akimsimanga sana Spika Ndugai.



Hicho kipindi kabae na ngoma wote hawana secular thinking, Tanzania kwenye journalism tunafanya kitchen parties, angalia interview zao zote wakifanya na christians utaona hilo, Revisit interview yao na Dr Gwajima they were foolishly exposed on partisanship
 
Wahindi, warabu na wasomali hivi hawa wananchi wanao wachagua huwa wamekosa kwenye makabila yao watu wa kuwachagua? shame on them
 
Wahindi, warabu na wasomali hivi hawa wananchi wanao wachagua huwa wamekosa kwenye makabila yao watu wa kuwachagua? shame on them

Ngozi nyeupe ilibarikiwa yan wanakubalika kotekote, wanajitambua na wachapa kazi,,co kama sisi majungu mbele mwisho ndiomana hatufiki mbali. Angalia watu wa igunga wameyaona matunda chini ya rostam.
 
Ngozi nyeupe ilibarikiwa yan wanakubalika kotekote, wanajitambua na wachapa kazi,,co kama sisi majungu mbele mwisho ndiomana hatufiki mbali. Angalia watu wa igunga wameyaona matunda chini ya rostam.
Nyumba za tembe ndiyo matunda? Moshi, Arusha, Mbeya, Mwanza na Iringa hawajawahi kuchagua mhindi, mwarabu wala msomali mbona wana maendeleo kuliko Singida, Igunga, Morogoro, Kishapu n.k?
 
Mwenye uelewa wa masuala ya silaha anisaidie sifa za hiyo silaha aliyoshika huyo mama.
IMG_20200507_095944.jpg
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom