Mbunge wa Kahama Mjini ashauri Vyuo Vikuu kuwajibika kutafuta ajira kabla ya kusajili Wanafunzi

Umeamua kumu attack? Ishu ni kwamba ana hoja au hana? Usikimbilie kuhukumu njia zake alizotumia kutoboa
Atakuwaje na hoja wakati hakusoma? Anawezaje kukosoa mitaala wakati haijui? Tatizo la vijana wasio na kazi siyo kwamba elimu yetu ina shida bali ni kwamba Serikali imevuruga sekta binafsi na ikakaa miaka 5 bila kuajiri. Matokeo yake graduates wanaonekana useless
 
Nilicheka Sana aliposema wanaosomea taaluma km ya udaktari ni Sawa Tu wakisoma chuo miaka mitatu maana anachokisomea anafanya practical kwenye hospitali,Hilo wwnanchi hatuna tatizo nalo,sasa wenzangu na mie mfano mtu anasomea procurement sijui wenyewe mnaita manunuzi unasomaje chuo miaka mitatu..unanunua nn miaka yote hiyo km siyo kupoteza muda tu..yaani unasomaje miaka mitatu manunuzi alafu unarudi nyumbani unamwambia mzazi nimesomea manunuzi Nani sasa atakuajiri kwenye Duka,miezi name inatosha degree

Huyu Mwamba na msukuma wananifurahisha sn
Hahahah unasomea manunuzi miaka mitatu wakati watu wananunua vitu kila saa!😂😂😂
 
Atakuwaje na hoja wakati hakusoma? Anawezaje kukosoa mitaala wakati haijui? Tatizo la vijana wasio na kazi siyo kwamba elimu yetu ina shida bali ni kwamba Serikali imevuruga sekta binafsi na ikakaa miaka 5 bila kuajiri. Matokeo yake graduates wanaonekana useless
Hata kama ingekuwa haijavurugwa bado tatizo la ajira lipo tu! Huwezi ku justify kwa kusingizia kuvurugwa kwa sekta binafsi!

Ajira ni swala zito maana sio wote walipata ajira 2010-2015
 
Hata kama ingekuwa haijavurugwa bado tatizo la ajira lipo tu! Huwezi ku justify kwa kusingizia kuvurugwa kwa sekta binafsi!
Huyo mbunge anasema kuwe na masomo yanaitwa;
Personal development
Money literacy

Ndio elimu ya Tanzania imekosa hivyo?

Anajiona anajua sana kuliko watunga mitaala iliyotufikisha hapa.
Hovyo kabisa
 
Ukiingia chuo
Unafundishwa taaluma mbali mbali;
Ufundi, ualimu, udakitari, sheria, uchumi, uendeshaji biashara, uchimbaji madini. Nk
Ubaya upo wapi?

Chuoni unafundishwa masoma ya kiada kwa kutumia vitabu vya kiada.
Unaelekezwa kusoma vitabu vya ziada, Library zipo,internet ipo vyote unaelekezwa.

Sasa ubaya wa elimu ya Tanzania upo wapi?
 
Mtu akisimama na kushauri masoma mapya yaongezwe au/na masomo fulani yaboreshwe hiyo ni sawa.
Kozi mpya kufuatana na wakati sawa.
Kozi fulani zifutwe kutokana na wakati sawa.
 
Huyu ni comedian tu na anataka siku zote kuwadharau waliosoma kwa vile yeye ni Darasa la 7. Bado watu hawajasahau namna alivyofanya uharamia wa biashara ndani ya Lake Victoria. Amebeba Sana magendo, amekwepa sana Kodi, ameua sana maafisa wa Serikali.

Na mara ya mwisho kwenye miaka ya mwanzo mwa 2000 alihusika kuwamwagia watumishi wa TRA tindikali. Kisha alipokuwa wanted akakimbilia Zimbabwe.

Kishimba hata madawa ya kulevya ameuaza Sana kwa kubeba kwenye magari yake kati ya SA, Zimbabwe na Tanzania.

Asidharau elimu kwa vile ametajirika kwa njia OVU
We jamaa una machungu sana kuona mwamba ni tajiri ila wewe na degree yako unalipwa laki 4!

Jamaa ana hoja hilo ndilo la msingi sasa concetrate kwenye kupangua hoja! Hio elimu yako bila pesa ni ushuzi tu kwenye jamii maana hamna kitu utafanya bila hela. Binafsi nigerudishwa utotoni sasa nikaambiwa kuchagua kutafta hela na kusoma ningekimbilia kutafta hela maana elimu ya la 7 inatosha sana kujitambua, hio degree haina maana kama huna hela ni sawa na sifa ya kupendeza tu!
 
Ukiingia chuo
Unafundishwa taaluma mbali mbali;
Ufundi, ualimu, udakitari, sheria, uchumi, uendeshaji biashara, uchimbaji madini. Nk
Ubaya upo wapi?

Chuoni unafundishwa masoma ya kiada kwa kutumia vitabu vya kiada.
Unaelekezwa kusoma vitabu vya ziada, Library zipo,internet ipo vyote unaelekezwa.

Sasa ubaya wa elimu ya Tanzania upo wapi?
Ubaya upo kama haiwezi kukuletea pesa! Mfumo uliopo ni kusoma kuajiriwa ukomboe wadogo zako na wazazi wako uzeeni! Sasa kama unamaliza kisha unaenda kupiga debe kwenye dala dala au kutembeza kashata na kuuza mtumba hio degree ina maana gani! Kwa elimu ya std 7 usingeweza kufanya hayo!?
 
Mtu akisimama na kushauri masoma mapya yaongezwe au/na masomo fulani yaboreshwe hiyo ni sawa.
Kozi mpya kufuatana na wakati sawa.
Kozi fulani zifutwe kutokana na wakati sawa.
Muda upunguzwe kutokana na wakati! Tunapotezeana muda tu! Shule iwe fupi sio unasoma kwa miaka 16 at minimum kisha unarudi mtaani kufanya vitu ambavyo ungeweza kuvifanya kwa shule ya miaka 7 tu!

Imagine mtu aliedunda form 4 ataongeza mwaka mmoja wa cheti so atamaliza shule after 17yrs! Provided haja postpone mwaka au ku carry over! Ina maana anamaliza degree na miaka 26 incase alianza shule na miaka 8
 
Darasa la 1-3 watoto wanasoma Kusoma, Kuhesabu na kuandika

Madarasa yaliyobakia shule ya msingi wanasoma Hisabati, Kiswahili, Siasa, Historia, Jiografia, Sayansi, Sayansi kimu

O level wanasoma compulsory masomo Kama history, geography, maths, Kiswahili, Siasa, biology na english kama compulsory. Na wanasoma elective Kama chemistry, physics, agriculture, French, Commerce

Then A- Level wana zero in kwenye combination za masomo matatu matatu Kama PCB, PCM, PGM, EGM, HKL, KLF, ECA etc

Sasa matatizo au mapungufu yako wapi? Hiyo mitaala inakupa kila unachotaka

How can Darasa la 7 la Kishimba linaweza kutoa ushauri wakati hajawahi ingia sekondari?
 
Ubaya upo kama haiwezi kukuletea pesa! Mfumo uliopo ni kusoma kuajiriwa ukomboe wadogo zako na wazazi wako uzeeni! Sasa kama unamaliza kisha unaenda kupiga debe kwenye dala dala au kutembeza kashata na kuuza mtumba hio degree ina maana gani! Kwa elimu ya std 7 usingeweza kufanya hayo!?
Kuna VETA kwa wasio na uwezo wa kwenda higher learning. Tatizo ni kwamba mfumo wa elimu hauongei na mfumo wa ajira. Na ajira zinatengenezwa na Serikali through a strong private sector na zile za moja kwa moja na Serikali
 
Nitajie nchi iliyopunguza Degree ikawa ya miezi 8, sijui labda North Korea
Degree hazina maana mpaka pale ajira zitakapokuwa reliable! Aidha zipunguzwe muda au zifutwe kabisa watu waishi kwa namna ingine sababu swala la ajira limekuwa changamoto dunia nzima sio bongo tu while wale walioko advantaged hawajali!
 
Kuna VETA kwa wasio na uwezo wa kwenda higher learning. Tatizo ni kwamba mfumo wa elimu hauongei na mfumo wa ajira. Na ajira zinatengenezwa na Serikali through a strong private sector na zile za moja kwa moja na Serikali
Hata Veta itafikia mahali itakuwa inatapika watu hawana michongo maana mafundi wakizidi kitaani unafikiri kitachotokea ni nini?
 
Kwani wazazi na watoto wao wanalazimishwa kujiunga na vyuo vikuu? Si kila mtu ana uchaguzi wake. Elimu ya msingi ndio lazima, lakini hiyo baada ya msingi ni hiyari ya mtu.
 
Degree hazina maana mpaka pale ajira zitakapokuwa reliable! Aidha zipunguzwe muda au zifutwe kabisa watu waishi kwa namna ingine sababu swala la ajira limekuwa changamoto dunia nzima sio bongo tu while wale walioko advantaged hawajali!
Kwani kutafuta degree ni lazima? Hiyo ni hiyari ya mtu. Kwa nini iwe tukose wote? Tutazifuata nje ya nchi!
 
Back
Top Bottom