Zamani sana... narudia, kitambo sana wakati nipo bwa mdogo tu!!
Basi bhana... ikawa nipo ground floor na mdada fulani hivi! Huyu mdada alikuwa mshikaji wangu sana ingawaje alikua mkubwa sana kwangu... Tom Boy fulani hivi!
Baada ya kupiga stori mbili tatu mara akaja binti mmoja ambae alikuwa dada wa kazi wa jirani yao! Swali lake la kwanza kwa huyu Housegirl lilikuwa "...mbona umechelewa, ulikuwa unafanya nini?"!
"Samahani dada, nilikuwa naoga..." Ndo jibu alilotoa yule binti, nami nilipoinua macho kumtazama, nikakuta kweli alikuwa na maji maji mwilini!
"Yaani hapo ndo umetoka kuoga? Kabla hujaoga ulikuaje?" Rafiki yangu huyu akamuuliza swali lingine la kijeuri yule housegirl!
Kwa mara nyingine, na bila kutarajia, nikajikuta nainua tena shingo kumtazama yule binti aliyedai anatoka kuoga!! Ingawaje sikukusudia lakini nikajikuta tu nikijiuliza swali lile lile lakini kimoyomoyo!!!
Anyway, hata sijui ni kwanini nimeukumbuka huo mkasa...
Hongera sana Mheshimiwa Mavunde kwa kuanza ukarabati na uboreshaji wa miundombinu Jijini Dodoma!!