Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde ashiriki zoezi la ufunguzi wa barabara zilizokuwa hazipitiki kwa Muda mrefu
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde leo ameshiriki na viongozi wa Kata ya Chigongwe kukagua zoezi la kufungua barabara yenye urefu wa kilomita 5.2 kutoka eneo la Chigongwe-Ngh’ambala ikiwa ni sehemu wa utekelezaji wa Ahadi za Mbunge huyo za kufungua barabara hiyo ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wananchi wa eneo hilo.
Kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza adha ya matumizi ya muda mrefu ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine ndani ya kata ambapo awali wananchi walikuwa wakipata tabu kupita maeneo yasiyo rasmi kwasababu ya kukosekana kwa barabara inayounganisha mitaa husika.
"Tumeanza sasa ukarabati na kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali za ndani ya Jiji na pembezoni ya Jiji ili kuwapunguzia adha wananchi kutokana na kutopitika kwa urahisi kwa baadhi ya barabara katika maeneo mbalimbali" alisema Mhe. Mavunde
Nitaendelea kushirikiana na TARURA kuhakikisha tunayafikia maeneo mengi zaidi yenye barabara korofi kadri bajeti itakavyoruhusu.
Ora et Labora”Sala na Kazi”
De Populo servorum “Mtumishi wa Watu”