Mbunge Tabasamu Amtia Moyo Mwigulu Amuambia Awe na Ngozi Ngumu Tu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946

MHE. TABASAMU HAMISI AMTIA MOYO MWIGULU AMUAMBIA AWE NA NGOZI NGUMU TU

"Leo niko kizalendo zaidi, kuna watu ni majemedari wa kupiga kelele na kuzungumza sana maneno makali kwenye mitandao, Waziri Mwigulu maneno haya yangekuwa yanatoboa mwili wako leo ungekuwa umejaa Viraka na Bandeji mwili mzima" - Mhe. Tabasamu Hamisi, Mbunge wa Sengerema.

"Unachotakiwa sasa hivi ni kuwa na ngozi ngumu tu na kujenga imani halafu baadaye unatoboa nchi inatukanwa kila kona na ujue sababu ni watu wamechoka hawana pesa mifukoni kwahiyo mtu akikaa akafikiri hana cha kufikiri anaingia mtandaoni na kuanza kutukana sasa hili lazima ulijue" - Mhe. Tabasamu Hamisi, Mbunge wa Sengerema.

"Hawa wataalamu wetu wakati wanaandaa bajeti wawe wanatuita na sisi tuliochomwa jua sana huko mtaani tuje kuwashauri namna ya kuandaa bajeti kuna vitu ambavyo tutawaeleza hiki weka hiki toa lakini mkijifungia ndani ninyi mliokaa kivulini mnakaa kwenye magari yenye AC na kila kitu mkimpelekea Waziri naye huku anaendelea kutukanwa sana" - Mhe. Tabasamu Hamisi, Mbunge wa Sengerema.

"Hali siyo nzuri huku chini Miradi mingi sana inafanyika maendeleo yanazunguka kama tairi la gari nchi inakuwa kama imepata uhuru sasa hivi kila kitu kinafanyanyika lakini kuna jambo la kujiuliza kwanini kelele zinakuwepo? huku chini kuna watu wakitoka saa 12 asubuhi kwenda kutafuta pesa wanachomwa jua mpaka saa 12 jioni anarudi na elfu tatu au elfu mbili anapitia dagaa kwaajili ya kwenda kula nyumbani na hawa watu wapo wengi nchi hii leta mpango wa kuleta pesa wananchi nao wapate pesa nazo zizunguke kama tairi la gari na kelele nazo zitapungua" - Mhe. Tabasamu Hamisi, Mbunge wa Sengerema.

"Lazima muangalie huku chini wananchi wanatakiwa wapate miradi itakayowaendesha yatengenezwe masoko ya garama nafuu, ipo miradi mingi inayokwenda na pesa nyingi zimekwama kuna magari mabovu katika halmashauri kwanini yasiuzwe tukapata fedha ili zirudi kwa wananchi huku chini zikafanye kazi?, mnakuwa na vitu vibovu mnavishikilia hayo magari yauzwe tupate fedha za kuendeshea ofisi" - Mhe. Tabasamu Hamisi, Mbunge wa Sengerema.

"Bandari ndiyo malango pekee utakaokuja kututoa sisi kwenye matatizo, wengi waliokuwa wanapotosha walikuwa na maslahi kwenye hii bandari wanandugu wa ile bandari wanapotoshwa wanapewa pesa kwenye mitandao ili wapotoshe kwamba bandari inauzwa inauzwa kwa lipi? wakati kitu kipo kwenye mikataba, Waziri wa Fedha endelea kuwa na ngozi ngumu lakini uwakumbuke wachoma jua" - Mhe. Tabasamu Hamisi, Mbunge wa Sengerema.
 

Attachments

  • maxresdefaultsderhjuyi.jpg
    maxresdefaultsderhjuyi.jpg
    55.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom