Mbunge Juliana Masaburi azungumza na Baraza la Vijana UVCCM Bunda

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MHE. JULIANA MASABURI AZUNGUMZA NA VIJANA WA BARAZA LA UVCCM WILAYA YA BUNDA MKOA WA MARA

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi tarehe 15 Julai, 2023 amekutana na Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda lenye Majimbo matatu ya Bunda Mjini, Bunda Vijijini na Mwibara.

Katika Baraza hilo Vijana wa UVCCM Bunda wamemueleza Masaburi kuwa wanakutana na changamoto za Kukosa Miradi; Kutoshirikishwa kwenye Miradi ya Serikali; Ukosefu wa Kadi za UVCCM na Vijana wanaojitoleq kufanya kazi Serikalini kutopewa kipaumbele nafasi zinapotolewa.

Aidha, Mhe. Juliana Masaburi amewachangia Vijana UVCCM Bunda Viti 50@15,000 vyenye thamani ya shilingi 750,000; na ameahidi kuwapatia Mashine ya Kufyatulia Matofali yenye thamani ya Shilingi Milioni 7,000,000 kama mradi wa UVCCM Wilaya ya Bunda

Vilevile, Mhe. Juliana Masaburi amewasihi Vijana kuendelea kuwa na mshikamano kwani wao ndiyo jeuri ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwataka kuunga mkono kwa vitendo kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Serikali awamu ya sita inayosimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.55.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.55.jpeg
    71.1 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.53.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.53.jpeg
    74.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.52(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.52(2).jpeg
    93.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.52.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.52.jpeg
    77.8 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.50(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.50(1).jpeg
    102.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.50.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-19 at 14.05.50.jpeg
    79.8 KB · Views: 4
Halafu utakuta kuna lipumbavu, familia yao hakuna hata mjumbe wa nyumba linatamba Ccm Ina wenyewe, kumbe wenye Ccm yao ndio hawa.
 
Marehemu baba yake Didas Masaburi alikuwa jambazi mashuhuri ndani ya ccm!! Akiwa mayor wa Dar es salaam ndio alikuwa kinara pamoja na marehemu Idd Simba kuihujumu kampuni ya usafiri Dar es salaam!!! Hopefully binti yake hatarithi tabia za baba yake ingawa waswahili wanasema " tunda halianguki mbali na mti wake"!
 
MHE. JULIANA MASABURI AZUNGUMZA NA VIJANA WA BARAZA LA UVCCM WILAYA YA BUNDA MKOA WA MARA

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi tarehe 15 Julai, 2023 amekutana na Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda lenye Majimbo matatu ya Bunda Mjini, Bunda Vijijini na Mwibara.

Katika Baraza hilo Vijana wa UVCCM Bunda wamemueleza Masaburi kuwa wanakutana na changamoto za Kukosa Miradi; Kutoshirikishwa kwenye Miradi ya Serikali; Ukosefu wa Kadi za UVCCM na Vijana wanaojitoleq kufanya kazi Serikalini kutopewa kipaumbele nafasi zinapotolewa.

Aidha, Mhe. Juliana Masaburi amewachangia Vijana UVCCM Bunda Viti 50@15,000 vyenye thamani ya shilingi 750,000; na ameahidi kuwapatia Mashine ya Kufyatulia Matofali yenye thamani ya Shilingi Milioni 7,000,000 kama mradi wa UVCCM Wilaya ya Bunda

Vilevile, Mhe. Juliana Masaburi amewasihi Vijana kuendelea kuwa na mshikamano kwani wao ndiyo jeuri ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwataka kuunga mkono kwa vitendo kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Serikali awamu ya sita inayosimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Alikuwa usingizi wa Marehemu Namba 1. Siku ya tangazo la kifo Alilia sana Dodoma.
 
Back
Top Bottom