Abood ahaidi tsh. Mil. 15,000,000/- zahanati kata Magadu

Oct 8, 2023
37
17
OFISI YA MBUNGE JIMBO LA MOROGORO MJINI.

NEEMA KATA YA MAGADU.

MHE. ABOOD AHAIDI TSH. MIL. 15,000,000/- ZAHANATI KATA MAGADU


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz. M.Abood leo tarehe 13.01.2024 ameshiriki Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Magadu akiwa ndiye Mgeni Rasmi, uku akipokelewa kwa Shangwe, nderemo na Vifijo na Wajumbe walioupamba mkutano huo.

MHE. ABOOD AKAKIPONGEZA CHAMA KATA MAGADU
Mhe. Mbunge hakusita kutoa pongezi zake kwa Chama cha Mapinduzi Kata ya Magadu hasa kutokana na ushiriki pamoja na ushirikiano wao katika kusimamia Miradi mbalimbali ya Wananchi ambayo kimsingi yeye Mwenyewe Mbunge sambamba na Viongozi wenziwe Wilaya ya Morogoro Mjini wamekuwa wakipambana uwepo wake na kuzaa matunda Mathalani Miradi ya Maji Magadu, Miradi ya Elimu iliopo hii leo, Afya n.k

MIL. 15,000,000/- ZA-AHIDIWA UBORESHAJI WA ZAHANATI MAGADU
Kama ilivyokawaida yake, Mhe. Mbunge akiahidi utelekeleza, sasa Neema ni zamu ya Kata ya Magadu mara baada ya neema hiyohiyo kuwa imeshazifikia Kata nyinginezo, ambapo amehaidi kutoa Tsh mil 15 uboreshaji wa Zahanati ya Kata ya Magadu ili Wakina Mama wajifunguwe Salama na Huduma ya afya iboreshwe na kuwa karibu mno na Wananchi.

MHE. ABOOD AMSHUKURU MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAH.
"Miradi mingi iliopo katika Kata ya Magadu inayowanufaisha Wananchi Kata hiyo na maeneo mengine Jimboni ni msaada mkubwa kutoka kwa Mama atupendae Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" hivyo Mhe. Mbunge amesema ataendelea kumshukuru bila kuchoka uku akimpongeza kwa Kazi yake Nzuri.

Kwa kumalizia hotuba yake Mhe. Mbunge akawaomba Wajumbe wa CCM Kata ya Magadu kuendelea kuwa na Ushirikiano katika kusimamia Utekelezaji wa Ilani.


Ofisi ya Mbunge Jimbo la Morogoro Mjini
Kitengo cha Habari.
20240113_124757.jpg
 
Back
Top Bottom