Mbunge Musukuma asitake Kuhalalisha kuwa wenye Elimu ndogo wapendelewe, wasikilizwe sana na waonewe mno huruma na Watu kwa gharama ya kuwananga wasomi

Generalist

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,327
2,000
Ni kweli nakubali kuwa kusoma ( kuelimika ) sana siyo Kutusua ( Kufanikiwa ) Kimaisha kwani kama ingekuwa hivyo basi Mimi Generalist nisingekuwa na Maisha haya Duni ( ya Dhiki ) niliyonayo sasa kwa Elimu yangu hii ya haka ' tudigrii ' kangu Kamoja tu ninakokamiliki huu mwaka wa 12 sasa.

Lakini pia haimaanishi kuwa basi kwakuwa hukubahatika kuwa na Elimu za Wastani ( Degree ) aliyonayo Generalist, ya Kati ( Masters ) aliyonayo Sky Eclat na Mmawia na ya Juu kabisa ( Doctorate ) aliyonayo Mtani wangu Mwigulu Nchemba basi kila mara Uwadhihaki waliyobahatika kuwa nayo.

Generalist naheshimu sana Michango ya Mbunge wa Geita Msukuma na huwa ninavutiwa ( napenda ) mno Ujengaji wake wa Hoja hasa juu ya Masuala ( Issues ) ya Mambo Mtambuka ( Current Affairs ) yanayoendelea nchini.

Ila sijapendezwa na Kitendo cha Mbunge huyu Msukuma cha kutaka Kutumia Elimu yake haba ( ya Darasa la Saba ) kama Tiketi ya Kuwadharau wenye Elimu Kubwa ( Wanataaluma ) hapa nchini Tanzania na kama Kichaka chake cha Kuuficha Udhaifu wake kama Mbunge na Maendeleo Haba ya Jimboni Kwake.

Vile vile Generalist pia sipendi Vitendo vya Wasomi ( Intellectuals ) hapa Tanzania cha Kujiona na Kuwadharau wale wasiosoma sana kama Wao kwani Jukumu lao kubwa siyo Kuwadharau bali ni Kuwaelimisha na Kuwasaidia katika Kufikiri ili basi mwisho wa Siku Mawazo yao yote ( Fikra zao zote ) yawe ( ziwe ) na Tija kwa Maendeleo Mtambuka ya Taifa la Tanzania na Watanzania kwa ujumla.

Nimshauri tu Mbunge wa Geita Msukuma kuwa huu muda anaoutumia kila Siku Kuchukizwa na Kuwananga vibaya Wasomi wa Tanzania ( hasa Wanasiasa na Wabunge ) Wenzake angeutumia katika Kujielimisha zaidi kwa kwenda Shule na ikibidi nae afike hadi Chuo Kikuu ili basi baadae nae abadilike Kifikra na Kimtazamo ajue kuwa kumbe huenda haya Makelele yake na Chuki zake kwa wenye Elimu Kubwa ( Wasomi ) ni Matokeo ya kutopata Elimu Kubwa ambayo inasaidia kumfanya Msomi kuwaza Makubwa zaidi.

Msukuma akasome bado muda anao tu.
 

Sonkuno

JF-Expert Member
Nov 16, 2017
202
250
Mimi ninachoamini mtu aliyesoma anajua vitu vingi vingi sana ambavyo hao wakina msukuma hawajui degree ni Elimu kubwa sana. Sijui wabunge wasomi Wanamuogopa kumjibu ndio maana anavimba kichwa na kuwa nanga, hakusoma tu akubali au arudi shule umri na umbo vinamruhusu.
 

Generalist

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,327
2,000
Mimi ninachoamini mtu aliyesoma anajua vitu vingi vingi sana ambavyo hao wakina msukuma hawajui degree ni Elimu kubwa sana. Sijui wabunge wasomi Wanamuogopa kumjibu ndio maana anavimba kichwa na kuwa nanga, hakusoma tu akubali au arudi shule umri na umbo vina mruhusu
Na nashangaa kuona wamemnyamazia.
 

Makwasa

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
297
250
Mimi ninacho amini mtu aliye soma anajua vitu vingi vingi sana ambavyo hao wakina msukuma hawa jui degree ni Elimu kubwa sana. Sijui wabunge wasomi Wanamuogopa kumjibu ndio maana anavimba kichwa na kuwa nanga, hakusomahakusoma tu akubali au arudi shule umri na umbo vina mruhusu
Hoja za wasomi ndio zinazoplekea wenye elimu kudhalauliwa bungeni.
 

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
563
1,000
Kwanza kabisa, kusoma sio sufficient condition ya mtu kuelimika. Msukuma yeye hadharau kila aliyesoma ila anadharau output mbovu ya mtu aliyesoma halafu anakuwa hopeless kuliko hata asiyesoma. Ukiwa msomi halafu kwa makusudi unaacha kufikiri objectively na badala yake unasukumwa na tumbo basi ukidharaulika usilaumu.

Nyerere aliwahi kusema kuwa tamaa na heshima havikai nyumba moja.

Nchi hii wakati tunapata uhuru hadi miaka ya mwishoni ya 70 ilikuwa na idadi ndogo kabisa ya wasomi kiasi hata mtu aliyepata div zero aliweza kuajiliwa kihalali na kupata cheo, lakini nchi haikushuhudia wimbi la mikataba mibovu na ya kinyonyaji kama iliyoingiwa miaka ya kuanzia tisini na hadi 2015. Sasa kwa nini hao walioikubali wasidharaulike? Tena hiyo haitoshi, huenda siku moja wakasimama mahakamani wao na/au watoto wao kujibu mashtaka ya kuihujumu nchi kwa kiwango hicho.

Wasomi wakitaka heshima wasimamie ukweli .
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,083
2,000
Msukuma yuko relevant kwa msingi, hao waliosoma kiwango cha maarifa yao hakina uhusiano wowote na kutatua changamoto za jamii inayowazunguka.

Amekuwa focused kwa kumsema Prof. Muhongo, yeye kama mtaalamu ilitakiwa asikize hoja za Musukuma achukue sampuli ya madini aliyopewa na kupeleka lab ili kuhakikisha anachoambiwa ni kweli au la. Prof akachukulia poa hoja ya msukuma akaenda mbali kwa kumdhihaki mbele ya wapiga kura wake.

Kuna nyakati wasomi wetu hasa wahadhiri wa vyuo au wasomi wanaofanya white colar jobs kwa muda mrefu hawana practical experience ya kilicho mtaani au field. Sasa wanapotakiwa kuchukua muda kujua nini kinaendelea wao wanadharau kwa msingi wa nadharia za vitabuni.
Mbaya zaidi kuna nadharia zingine zimekuwa developed na wazungu Ulaya kwenye context ya kwao na ziko vitabuni; ukizileta kwenye uhalisia mitaani kwetu hazi-apply.

Elimu iwe shahada, shahada ya uzamili au shahada ya uzamivu ni suala zuri sana; ila mwenye elimu akishindwa ku-connect na wasiosoma ili atatue matatizo yao, hiyo elimu inabaki kwenye cheti na joho alilovaa siku ana graduate. Kuna wasomi wanyenyekevu sana na wako tayari kukaa na yeyote kujua anawaza nini ili kutokea hapo wa-connect; kuna wasomi wana dharau sana, ni as if ukiwa PhD holder au Prof unakuwa na thamani na raia wa daraja la kwanza na asiesoma ni mtu asie na lolote.

Wasomi wakiwa wanyenyekevu, watakuwa na heshima kubwa sana nchi hii, ila wakileta dharau na bahati mbaya hao akina Musukuma wanawazidi hela, basi wanaendelea kudhalilishwa mara kwa mara.

Kumbukeni jamaa mmoja akiwa waziri anamponda Mtanzania mwenzake eti yeye ana degree nne na hawezi kuongea nae, mtu huyo huyo ukifika muda wa kuomba kura, hao LY ndio anawategemea wamsaidie kumpa kura aende bungeni.

Wasomi wetu baadhi wanashusha credibility yao wenyewe kwa uvivu wa kufikiri kwa kudhani ukiwa na PhD certificate basi ume-clear kila kitu.
 

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,454
2,000
Hili jambo ni kweli umeshindwa tu kuliwasilisha vizuri. Lakini nadhani wasomi wamenyamaza sana kiasi Musukuma anataka kuhalalisha illiteracy yake ionekane ni jambo la kujivunia na kutweza utu na elimu ya wenye Elimu.

Mimi nina Degrees 3 but huwa sijitanabaishi katika Umma kwa kutangaza Degree zangu. Hili watu huliona kwenye utendaji napokuwa kazini au mambo ya kitaaluma popote napokuwepo.

Otherwise nabaki tu kama Chizi mwingine yeyote wa hapa JF na Tanzania au Duniani kwa Ujumla.
 

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
4,345
2,000
Mimi ninachoamini mtu aliyesoma anajua vitu vingi vingi sana ambavyo hao wakina msukuma hawajui degree ni Elimu kubwa sana. Sijui wabunge wasomi Wanamuogopa kumjibu ndio maana anavimba kichwa na kuwa nanga, hakusoma tu akubali au arudi shule umri na umbo vinamruhusu.

Ukianza kukumbuka jinsi ya kujazia coursework, presentation ulizofanya tena kwa confidence, ukakumbuka assignments kibao ulizofanya plus test na hapa na pale, utafahamu elimu yetu kiukweli haisaidii watu kujiongeza maana unakuta msomi na PHD yake ni muoga hata wa kujiajiri sasa mtu ambae hakusoma anapata ujasiri maana akiangalia hata pesa kakushinda utamweleza nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom