Mbunge Martha Mariki Aipa Tano Serikali Mradi wa Bwawa la Nsekwa - Mlele

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

Mbunge Martha Mariki Aipa Tano Serikali Mradi wa Bwawa la Nsekwa - Mlele

MBUNGE wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameipongeza Serikali Kwa Kuleta fedha Shilingi Bilioni 2.4 kwaajili ujenzi wa Bwawa la Maji litakakalo saidia upatikanaji wa Huduma ya Maji katika Kijiji Cha Nsekwa na halmashauri ya Mlele Kwa ujumla.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameipongeza Serikali Kwa Kuleta fedha Shilingi Bilioni 2.4 kwaajili ujenzi wa Bwawa la maji litakakalo saidia upatikanaji wa Huduma ya Maji katika Kijiji Cha Nsekwa na halmashauri ya Mlele Kwa ujumla.

Akizungumza akiwa katika Ziara ya Kutembelea Kata za Mkoa wa Katavi alipotembelea Bwawa hilo katika Kijiji Cha Nsekwa Mbunge Martha Mariki amesema hatua hiyo ya serikali kuwekeza ujenzi wa Bwawa hilo itasaidia upatikanaji wa Huduma ya Maji Kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.

“Tumetembea na kushudia uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika kata hii ya Nsenkwa Zaidi ya bilioni 2.4 zimwekezwa katika bwawa hili, bwawa hili limetengezwa kwa ajiliya kuwasaidia wananchi kupata maji safi na salama nab wawa hili likikamilika litanufaisha kata Zaidi ya kata tano ambazo ni Inyonga, Nsenkwa, Ilela, Kamsisi na Utende” Amsema Mbunge Martha.

Katika hatua nyingine amesema kuwa serikali kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika mkoa wa Katavi ikiwemo miradi ya Maji,Afya,Elimu,na Barabara ni ishara ya serikali kudhamilia kusogeza huduma Kwa wananchi Kwa vitendo.

"tumeshuhudia miradi Mingi katika mkoa wetu wa Katavi hii inaonyesha nikwa namna gani serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan inania ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa wa Katavi " Amesema Mbunge Martha

Diwani wa Kata ya Nsenkwa Elijius Malando ameishukuru Serikali Kwa kuona umuhimu wa kujenga Bwawa hilo katika Kijiji Cha Nsenkwa Kwani litasidia upatikanaji wa maji Kwa wananchi Kwa kiwango kikubwa.

“Ni matumaini yangu vijiji kumi na nane vitanufaika kwa bwawa hili, tunamshukuru sana Mh. Rais kwa kutuona kupitia mradi huu wa bwawa la Nsenkwa kwani wananchi watapata huduma yam aji safi nasalama kwa wakati” Amesesma Diwani Malando.

Mbunge Martha Mariki ameanza ziara katika Wilaya ya Mlele Kwa Kwa Kuzitembelea Kata za Ilunde, Ilela na Nsekwa ambapo pamoja na mambo mengine ametoa shilingi Laki Tano Kwa Kila Kata alizozitembelea Kwa UWT Ili kusaidia wanawake wa jumuiya hiyo kujikwamua kiuchumi pamoja na kutoa Kadi za UWT Ili kuendelea kuongeza wanachama.

Mbunge huyo ameemdelea kuwa sisitiza Wananchi kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali Ili Wananchi waendelee kunufaika na serikali yao kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ziara hiyo inaendelea Kesho katika Kata za Kamsisi, Utende na Inyonga katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
 

Attachments

  • 1N.JPG
    1N.JPG
    26.4 KB · Views: 3
  • 2J.JPG
    2J.JPG
    12.3 KB · Views: 2
  • 3B.JPG
    3B.JPG
    29.2 KB · Views: 2
  • 4L.JPG
    4L.JPG
    36.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom