Mbunge Martha Mariki Asema "Kuwatenga Watu Wenye Ulemavu ni Dhambi Kubwa Sana

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

Mbunge Martha Mariki Asema "Kuwatenga Watu Wenye Ulemavu ni Dhambi Kubwa Sana

WAKAZI wa mkoa wa Katavi wameaswa kutowatenga watu wenye mahitaji maalumu badala yake wawe sehemu ya kuwaelimisha juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali Kwenye kundi hilo.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki wakati akizungumza na wanawake wa UWT Kata ya Usevya Halmashauri ya Mpibwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.

Mbunge huyo ameeleza kuwa Serikali Kwa kuzingatia umuhimu wa Kwa kundi la Walemavu kuhakikisha wanapatiwa Elimu na kunufaika na fursa zinazotolewa na Serikali.

"Naomba nitoe wito Kwa wananchi wenzangu wa mkoa wa Katavi na wanausevya tuache kuwaficha Watu wenye ulemavu majumbani Kwani serikali hutoa fursa ya kundi hili kupata Mikopo na Elimu kuhusu mambo mbalimbali" Amesema mbunge huyo.

Aidha Katika hatua nyingine amewaomba wananchi hao kuwasaidia kundi la Walemavu Kwa kuwaelimisha juu ya fursa za Mikopo zinazotolewa na serikali Ili waweze kujikwamua kiuchumi

"Uzuri wa serikali yetu Kwa kutambua umuhimu wa Kundi hili la Walemavu Kupitia Mikopo ya Asilimia Kumi Walemavu wanayofursa ya kupata Mikopo bila kujiunga katika vikundi hivyo ndungu zangu tuwe mabalozi wazuri huko tuendako Kwa kutambua fursa hiyo" amesema Mbunge Martha.

Awali Akiwa katika Kijiji cha Ilalangulu Kata ya Kibaoni ametembelea Jengo la mama na Mtoto Kijiji cha Ilalangulu na kuipongeza serikali Kwa juhudi inazozifanya za kuendelea kuimalisha miundo mbinu ya afya hasa Kwa akina mama wakati wa kujifungua.

"Naipongeza serikali Kwa Kwa ujenzi wa jengo hili la mama na Mtoto hapa Ilalangulu jengo hili lipo katika hatua za mwisho mwisho likikamilika litasidia Sana akina mama wenzangu kujifungua katika hali ya usalama zaidi" amesema Martha.

Ziara ya Mbunge maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki inaendelea katika Wilaya ya Mlele halmashauri ya Mpibwe ambapo ametembelea Kata za Kibaoni,Usevya na Ikuba ambapo ameweza Kutoa shilingi Laki Tano Kwa Kila alizozitembelea na kutoa Kadi za UWT Kwenye Kata hizo ili kuendelea kuongeza Wanachama wa UWT.

Pamoja na hayo amewachangia Waendesha Bodaboda katika Kijiji Cha Ilalangulu Shilingi Laki Mbili Kwaajili ya kutunisha mfuko wa Vijana hao.

IMG-20230804-WA0062.jpg
IMG-20230804-WA0059.jpg
IMG-20230805-WA0002.jpg
IMG-20230804-WA0061.jpg
IMG-20230805-WA0001.jpg
IMG-20230805-WA0001.jpg
IMG-20230804-WA0060 (1).jpg
 
Back
Top Bottom