Mbunge Lema apandishwa kizimbani, afunguliwa kesi 2 za jinai. Anyimwa dhamana

Mungu apishe mbali asije zaliwa mtoto mwenye tabia kama za hovyo Lama za lema popote duniani.Amen

wewe fanya masikhara na Mungu tu.. goliath alijiona kuwa na nguvu kuliko daudi lakini aliuwawa na mkono wa daudi

sasa nyie Chama Cha Mandezi mnajiona mko "untouchable" juu ya sheria mna macho lakini hamuoni mna masikio lakini hamsikii mnasahau kuwa Mwenyezi Mungu huwatumia walio dhaifu kuwaangusha wenye nguvu ili kujidhihirisha uwezo wake mbele ya watu wake

siku yenu yaja.. yetu macho
 
Tuko interested kujua charge aliyoshitakiwa nayo,huku mtaani tunajiuliza kwa maneno yale aliyotamka litakuwa ni kosa gani?

1.Sio abusive language -in the real definition of abusive language.
2.Sio deformation.
4.Sio kutishia kuua kwa maneno.
5.Sio uchochezi

Sasa ni kosa gani,mlio mahakamani tusaidie sisi maamuma wa sheria.
mkuu
2. defamation
 
shika adabu wee miya. usilete mzaha kwa maisha ya rais. watu kibao na hela kibao inatumika kumlinda halafu lema kwa ujinga wake eti anamtabiria kifo kama hafuati matakwa ya ukawa. ukawa hawa waliyokufa kifo cha mende kwenye uchaguzu. ndio maana huyu lema wamemkamata. nahisi safari hii haponyoki.
kwahiyo maisha yako na ya familia yako ni expendable si ndio?
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu unaoieleza hapa.L ema hawezi kutukana watu halafu eti ameshika silaha ya dunia ,hakuna kitu kama hicho.Hiyo hiyo silaha ndiyo itamhukumu kwa sababu hana adabu.

adabu kwa mamlaka isiyotii sheria inazosimamia
 
Masuala ya Imani kuyapeleka mahakamani sidhani kama ni sahihi. Hivi shekh Yahaya aliwahi kupelekwa mahakamani utabiri wake wa 2010? Au kwa sababu Lema ni Mbunge wa Chadema?. Ila nachoamini ikiwa alichosema Lema hakina kibali kutoka kwa Mungu hata angehubiria dunia nzima hakuna kitakachotokea na si kwa sababu ya vyombo vya dola na sheria zilizopo na zitakazotungwa. Lakini Kama kweli Mungu amesema na Lema hata angefungwa, awekwe rumande miaka kumi au ahukumiwe kifo makusudi ya Mungu hayazuiliki.
 
Mh. GODBLESS J LEMA (MB) wa Jimbo la Arusha Mjini ndiyo anapelekwa Mahakamani muda huu. Atapandishwa kizimbani saa 2:30 asubuhi.
Tafadhali tunaomba Wananchi mjitokeze Mahakamani (RM's COURT) kwa wingi.

Imetolewa na;

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Arusha Mjini

=======================

Updates
More Updates Mahakamani Arusha: Shauri lilifunguliwa na mawakili John Mallya na wenzake kuiomba Mahakama Kuu kuwaamuru Polisi kumfikisha Mahakamani Mh Godbless Lema kwasababu ni ubatili kisheria kuendelea kumshikilia imeshatolewa uamuzi mapema hii na Polisi wamepewa nusu saa wawe wamemfikidha mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu na sio Hakimu Mkazi tena..

******
Hilo ni pigo la kwanza takatifu kwa Jeshi onevu...linalopalilia na kuotesha mbegu mbaya ya kutoheshimu sheria kwa kisingizoo cha 'maagizo toka juu'
Mh GODBLESS J LEMA (MB) wa Jimbo la Arusha Mjini amefikishwa Mahakamani ( RM's COURT) leo Jumanne tarehe 8/11 \2016 majira ya saa 2:10 asubuhi. Kesi yake inasimamiwa na jopo la Mawakili nguli wakiongozwa na John Mallya,
Regold Nkya, Sheck Mfinanga, Charles Adiel.
Mh Jaji MAGIMBI ameamuru Mh GODBLESS J LEMA (MB) aletwe mbele ya Mahakama yake tukufu ndani ya nusu saa kuanzia alipotoa maamuzi hayo saa 3:00 asubuhi.

Lema amefunguliwa kesi mbili za jinai ambazo ni kesi no; 440 na 441
Wakati tunasikiliza kesi iliyofuguliwa na mawakili wetu upande wa jamuhuri wakasema walishamleta mtuhumiwa mahakamani wakati kesi inaendelea kusikilizwa ghafla tukapewa taarifa kwamba wamempandisha mahakama ya hakimu mkazi basi jaji kwa busara akaarisha kesi hadi watakapomaliza kesi ya mh mbunge.
Mahakama inaendelea kinachoendelea Wanasheria wanaanza kupingana kwa vifungu vya sheria
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesomewa mashtaka ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais Magufuli. Arudishwa rumande baada ya kunyimwa dhamana Moderator Lema ameshtakiwa kwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Raisi Magufuli rekebisheni


Hii nchi sijui inaelekea wapi?
Lema leo ameaga kwa kuonyesha silaha kubwa dunia.. Biblia takatifu baada ya kurudishwa tena magereza baada ya kunyimwa dhamana.



View attachment 430919
View attachment 430922

Hivi Lema siku hizi ni mchungaji?
 
Hebu tujisahaulishe kidogo kuhusu kamanda Lema tuendelee na sherehe za Donald J Trump kwanza
 
Jamani makamanda shughulikieni Hiyo dhamana ili aweze kupata maono zaidi , kule haruhusiwi kuwa na bibilia na kulala kwa mangangamu hivyo ndoto Zenye maono hawezi kuziota.
 
Anaweza kuwa na mental issues huyu na anahitaji psychiatric care. Anafikiri kukamatwa na polisi mara kwa mara ndiyo umaarufu. Sad !
 
Back
Top Bottom