Mbunge Lema apandishwa kizimbani, afunguliwa kesi 2 za jinai. Anyimwa dhamana

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mh. GODBLESS J LEMA (MB) wa Jimbo la Arusha Mjini ndiyo anapelekwa Mahakamani muda huu. Atapandishwa kizimbani saa 2:30 asubuhi.
Tafadhali tunaomba Wananchi mjitokeze Mahakamani (RM's COURT) kwa wingi.

Imetolewa na;

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Arusha Mjini

=======================

Updates
More Updates Mahakamani Arusha: Shauri lilifunguliwa na mawakili John Mallya na wenzake kuiomba Mahakama Kuu kuwaamuru Polisi kumfikisha Mahakamani Mh Godbless Lema kwasababu ni ubatili kisheria kuendelea kumshikilia imeshatolewa uamuzi mapema hii na Polisi wamepewa nusu saa wawe wamemfikidha mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu na sio Hakimu Mkazi tena..

******
Hilo ni pigo la kwanza takatifu kwa Jeshi onevu...linalopalilia na kuotesha mbegu mbaya ya kutoheshimu sheria kwa kisingizoo cha 'maagizo toka juu'
Mh GODBLESS J LEMA (MB) wa Jimbo la Arusha Mjini amefikishwa Mahakamani ( RM's COURT) leo Jumanne tarehe 8/11 \2016 majira ya saa 2:10 asubuhi. Kesi yake inasimamiwa na jopo la Mawakili nguli wakiongozwa na John Mallya,
Regold Nkya, Sheck Mfinanga, Charles Adiel.
Mh Jaji MAGIMBI ameamuru Mh GODBLESS J LEMA (MB) aletwe mbele ya Mahakama yake tukufu ndani ya nusu saa kuanzia alipotoa maamuzi hayo saa 3:00 asubuhi.

Lema amefunguliwa kesi mbili za jinai ambazo ni kesi no; 440 na 441
Wakati tunasikiliza kesi iliyofuguliwa na mawakili wetu upande wa jamuhuri wakasema walishamleta mtuhumiwa mahakamani wakati kesi inaendelea kusikilizwa ghafla tukapewa taarifa kwamba wamempandisha mahakama ya hakimu mkazi basi jaji kwa busara akaarisha kesi hadi watakapomaliza kesi ya mh mbunge.
Mahakama inaendelea kinachoendelea Wanasheria wanaanza kupingana kwa vifungu vya sheria
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesomewa mashtaka ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais Magufuli. Arudishwa rumande baada ya kunyimwa dhamana Moderator Lema ameshtakiwa kwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Raisi Magufuli rekebisheni


Hii nchi sijui inaelekea wapi?
Lema leo ameaga kwa kuonyesha silaha kubwa dunia.. Biblia takatifu baada ya kurudishwa tena magereza baada ya kunyimwa dhamana.



tmp_11029-IMG-20161108-WA0034294166605.jpg

tmp_11029-IMG-20161108-WA0036181281590.jpg
 

Attachments

  • VID-20161108-WA0032.mp4
    5.2 MB · Views: 101
Taarifa kutoka Arusha
======================

Mh GODBLESS J LEMA (MB) wa Jimbo la Arusha Mjini ndiyo anapelekwa Mahakamani muda huu. Atapandishwa kizimbani saa 2:30 asubuhi.
Tafadhali tunaomba Wananchi mjitokeze Mahakamani (RM's COURT) kwa wingi.

Imetolewa na;

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Arusha Mjini
AMEFANYA KOSA GANI HUYU MJAMAA??
 
Makamanda mnahamasishana kufanya mambo ya kijinga tu, ila hutasikia makamanda wakihamasishana kufanya kazi! Sasa kujaa mahakamani kunaweza badili, mwenendo na hatimaye hukumu ya kesi? Hembu mkue kiakili maana hamkui mambo yenu ni Yale Yale tu kila siku. Very boring people with their boring party as well.
 
Tatizo sio kumkamata mtu unapomtuhumu kutenda kosa, tatizo ni kumuweka mahabusu kinyume cha sheria za nchi ambazo zinasema mtuhumiwa afikishwe mahakamani ndani ya masaa 24, hata kama upelelezi haujakamilika mahakama itaamua kama mtuhumiwa anastahili dhamana au la.Kinachokera ni wale tuliwapa dhamana ya kulinda haki zetu kutumia mamlaka waliyonayo kukandamiza haki zetu.
 
Makamanda mnahamasishana kufanya mambo ya kijinga tu, ila hutasikia makamanda wakihamasishana kufanya kazi! Sasa kujaa mahakamani kunaweza badili, mwenendo na hatimaye hukumu ya kesi? Hembu mkue kiakili maana hamkui mambo yenu ni Yale Yale tu kila siku. Very boring people with their boring party as well.
 
Wajitahidi kunusuru uchumi unaoendelea kudorora waachane na wanasiasa ambao kazi yao ya msingi ni siasa. Hivi leo ukisema kuwa mikutano ni mpaka 2020 katibu mkuu wa CCM unategemea afanye kazi gani? Tungependa wanasiasa kama Kinana, Zito, Lisu, Mbowe, Serukamba, Masinji etc wafunguliwe geti tumemisi hotuba zao za kusisimua zinatufanya kupunguza usongo wa mawazo.
 
Back
Top Bottom