Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

mheshimiwa nimefuatilia na nimeangalia hizo clips zilizowekwa na nnarejea lema anapaswa kushauriwa jinsi ya kuendesha siasa. si kila pahala husemwa lolote, au kusema ili mradi kujitafutia umaarufu au mtaji wa kisiasa.

mwenye akili atakiri kua kweli kuna mapungufu kwa upande wa serikali ktk kutatua hilo suali lkn lema ametumia hio loop hole vibaya. huo ndio ukweli. siasa za kizamani sana za kuchochea wananchi ili iwe mtaji wa siasa

"Wanafunzi wanapata mimba kwa sababu ya vihele hele vyao"...by JK huyo mkulu sasa ndio wa kufundishwa cha kuongea
 
What ila wameenda na hati, au ndio wataitengeneza kesho asubuhi.

Shame on serikali. Inaudhi sana kusikia mambo haya yanaendelea nchini kwetu.

Nyerere atakuwa anasikitika kuona wanaaribu chama chake jamani.

nyererere mwenyewe muuaji tu
 
lazima busara zitumike hata pale wahusika(police)wanapotaka kutekeleza matakwa ya wakubwa zao.
 
Akili ndogo kuongoza akili kubwa!

Kuna issue za msingi za kujadili kama mabilioni (Ufisadi) yaliyotumika kwenye sherehe ya Muungano...

PoliceCCM wanatumika kama "Mkamia" Ushemeji wa Dhaifu na Mwema utalipeleka Taifa letu pabaya.
 
"Wanafunzi wanapata mimba kwa sababu ya vihele hele vyao"...by JK huyo mkulu sasa ndio wa kufundishwa cha kuongea

Mbona unakwepesha mada kamanda? tunamjadili Lema na wala sio JK!

Hata kama JK au hata CCM wote wanapokuwa wanaongea au kutenda maovu, je, hii ina halalisha na CHADEMA wafanye maovu? au kusema ovyo? kama ina halalisha, basi sioni sababu ya kusema CHADEMA ndio mbadala wa CCM.

Msijifanye mnaweka vifua kwa hawa majangili wa amani, ndio ni rafiki zetu tukiwa kwenye starehe, lakini kwenye kuvunja amani ya nchi, watakuwa maadui wetu wakubwa. Lema anastahili adhabu kutokana na kauli zake.
 
Aminia mkuu.ccm hawajui karibu police wote wanalinda mabenk nyumba za wakuu ,wanaweza tumia sila kusaidia mapinduzi au hata mtungua mkuu yoyote.wengi wamechoka hadi sasa ni maadui wa serikali na jeshi lao.

ndoto za alinacha hakuna mapinduzi kwa ajili ya chadema em fkria tena, JWtZ analipwa vizur then amfate chadema??? Jeshi lina wakuu wake mmhhh labda mapinduzi ya ubunge
 
inasikitisha sana, tz tuna watawala madikteta

inasikitisha kuwa na wabunge wasioitakia amani Tanzania, zaman walpokuwa wanataka wabunge wazee sikujua kumbe vijana bangi tupu inaumiza sana.
 
ccm wanajisumbua bure arusha hawatuwezi lema anawasumbua sana viongozi wa ccm ubunge walimvua kwa hila lakini haki huwa haipotei mahakama ikamuridisha kwa kishindo hawajifunza bado wanajisumbua
 
Acha UPUMBAVU kwa pesa za lumumba.MUNGU anaona huu upumbavu wako na anajua kuwa LEMA hajawai kusema hivyo.
Utukane, utoke mapovu mdomoni, FACT is Lema yuko lupango.
Hii ni licha ya majigambo earlier on in the week na nilimsikia akisema kwenye luninga yeye au Mungu tu ndio wataamua hatma yake huko Arusha.

Sasa wewe Kohelethi kama una ubavu wa kiakili au vinginevyo msaijie huyu kijana, maana wabaya wake wamemtight.
 
Last edited by a moderator:
Utukane, utoke mapovu mdomoni, FACT is Lema yuko lupango.
Hii ni licha ya majigambo earlier on in the week na nilimsikia akisema kwenye luninga yeye au Mungu tu ndio wataamua hatma yake huko Arusha.

Sasa wewe Kohelethi kama una ubavu wa kiakili au vinginevyo msaijie huyu kijana, maana wabaya wake wamemtight.

Alishakaa Magereza sembuse central police..UNATUMIKA
 
Last edited by a moderator:
Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi onevu wa Polisi wakati huu wa usiku; Mh. Lema amekubali kukamatwa na amechukuliwa na gari la polisi wakati huu na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.

Wananchi wengi wamejitokeza ku-support mbunge wao na huenda Asubuhi wananchi wakawa wengi zaidi.

Scene two ni hali itakavyokuwa huko polisi.

Updates
Sasa wamefika CLocktower anasindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza ku-support kuelekea kituo cha polisi.

Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha amesachiwa na kuingizwa ndani. Kamanda Lema alikuwa ameambatana na magari ya makamanda waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.

Hivi sasa polisi wamewafukuza makamanda wote hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo. Makamanda wameondoka kwa amani na kwenda kupaki Safari hoteli wakisubiriana kupata mwongozo.

03:41am
Wamekutana pembeni ya kituo cha polisi na wamekubaliana kuwa watawanyike wakalale hadi kesho asubuhi watajuzwa kinachoendelea. Hivyo, Lema yupo ndani na wananchi waliomsindikiza wametawanyika kwenda kulala. Tutaonana asubuhi kwa yale yatakayojiri.

11:15am
Kwa sasa Lema bado yuko ndani na bado hajahojiwa. Kwa sasa anasubiriwa Mwanasheria wake ili ahojiwe. Mpaka sasa hakuna tamko lolote juu ya sababu za kukamatwa kwake. Baada ya kuhojiwa huenda mwanasheria wake atasema kilichojiri. Watu waharuhusiwi kukaa au kusimaa vikundi vikundi eneo la polisi.


Earlier by Emanzi:

Ukweli na uongo siku zote hujitenga ngoja tuone kipi kitajiri,kwa mtu anae tetea maslai ya wanyonge mwisho wa siku hushinda
 
Kama Wangeshindwa kumkamata ningeidharau sana serikali...
 
Kamwe ''hakuna uhuru bila kupitia utumwa''.
 
Kwa kweli hali hii si njema, kwani Mbunge hana kinga kwa mambo ambayo si ya jinai? Hii ina kaaje jamaniiii!
 
Tunasema kwamba tuna demokrsia ya uhuru wa kweli ? Nazani sasa matukio ya Lindi, Bumbuli wananchi kuchoma kituo
cha police, Na maeneo mengi ya nchi hii ni lazima serikali ijichunguze kwa makini,

Naaandika hii taarifa nikiwa nje ya nchi kwa ziara ya siku mbili na nimepokea taarifa ya kukamatwa kwa Mh Mbunge Lema
kwa mshituko mkubwa!

Mbunge ni mwakilishi wa Wananchi katika eneo lake, ni jambo la msingi serikali ikatambua kwamba sikuzote mtoto mdogo
Umleavyo ndivyo akuavyo.

Sasa serikali imelea mtoto kwa kumnyima chakula je ina tegemea kwamba mtoto akale wapi? Mtoto ni Mwanchi mwenye
shida, mwananchi mwenye kushindwa kununua hata sabuni ya kufulia nguo, mwananchi mwenye kushindwa kununua hata sukari,Mwananchi mwenye kushindwa kulas hata mlo mmoja kwa siku.

Lazima sasa ni wakati wa wananchi kuikataa serikali hii kwa kuiondoa kwa kura mwaka 2015 kwa kubadilisha viongozi
na sio sura wala majina yao!
Matukio yamezidi na wananchi sasa wamechoka tena na kudanganywa
Shime viongozi wetu muogopeni ,Muogopeni Mungu.
 
“Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika” –Mwalimu Julius Nyerere (Januari, 1966)
 
Back
Top Bottom