Na kwa mpango huo nashukuru wanatusaidia uchaguzi uwe mwepesi kwa CDM maana watu wanazidi kuwa na hasira juu ya vitendo vya unyanyasaji kama huo.Mkuu siku zote serikali zilizo madarakani ndizo chanzo cha matatizo. Sidahni kama hiyo ni issue ya kupeleka polisi hata kupekuwa nymbani kwa kamanda Lema. Kwa namna hii, CDM itaendelea kujulikana na kujikita mioyoni mwa watu bila gharama ya kuwafikia. Zote hizi ni baraka za Mungu. Watu wanaona na dunia inaangalia.
Hata kule alikukimbilia Idd Amin?
Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi onevu wa Polisi wakati huu wa usiku; Mh. Lema amekubali kukamatwa na amechukuliwa na gari la polisi wakati huu na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.
Wananchi wengi wamejitokeza ku-support mbunge wao na huenda Asubuhi wananchi wakawa wengi zaidi.
Scene two ni hali itakavyokuwa huko polisi.
Updates
Sasa wamefika CLocktower anasindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza ku-support kuelekea kituo cha polisi.
Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha amesachiwa na kuingizwa ndani. Kamanda Lema alikuwa ameambatana na magari ya makamanda waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.
Hivi sasa polisi wamewafukuza makamanda wote hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo. Makamanda wameondoka kwa amani na kwenda kupaki Safari hoteli wakisubiriana kupata mwongozo.
03:41am
Wamekutana pembeni ya kituo cha polisi na wamekubaliana kuwa watawanyike wakalale hadi kesho asubuhi watajuzwa kinachoendelea. Hivyo, Lema yupo ndani na wananchi waliomsindikiza wametawanyika kwenda kulala. Tutaonana asubuhi kwa yale yatakayojiri.
11:15am
Kwa sasa Lema bado yuko ndani na bado hajahojiwa. Kwa sasa anasubiriwa Mwanasheria wake ili ahojiwe. Mpaka sasa hakuna tamko lolote juu ya sababu za kukamatwa kwake. Baada ya kuhojiwa huenda mwanasheria wake atasema kilichojiri. Watu waharuhusiwi kukaa au kusimaa vikundi vikundi eneo la polisi.
Earlier by Emanzi:
Yawezekana wanataka kumtengenezea ushahidi wa uongo kwenye simu, ipad na laptop waliyochukua. Au wanataka kufuta sms iliyotumwa na mkuu wa mkoa? Tutaona mengi ya kuudhi ili tuwe na hasira ya kutosha tutakapoamua.
Ndugu yangu haya yote ni mashinikizo. Walijua kabisa kama hawatamkamata siku au usiku wa alhamis basi wasingetimiza lengo lao la kumlaza rumande (lock up) wikiendi nzima bila dhamana, kwa kuwa siku ya ijumaa ni sikukuu ya muungano wa tanzania na jumamosi na jumapili watasema ni wikiendi mahakama hazifanyi kazi. Kwa hiyo watakaa naye wikiendi nzima hapo kituo cha polisi kwa kisingizio hicho, kuwa asubiri kufikishwa mahakamani siku ya jumatatu ambako ndiko atapata dhamana. Kosa lenyewe wanajua linadhaminika labda ndo wambambikizie kosa la ugaidi ili asipewe dhamana na hivyo kumpotezea muda tu.Umekosa nini we Lema,
kuvamiwa usiku bila staha?
Mwenye kustahili haya,
si wewe si wewe Lema, ni Magesa!
Kwa sasa Lema anajisaidia haja kubwa kwenye ndoo,nita rusha video yake na kuwajuza kila tukio humu ndani lumande
Tayari uongozi wa chama mkoa chini ya katibu wa mkoa wameshaongea na RCO, muda si mfupi kamanda Lema atachukuliwa maelezo, ndiyo taratibu zingine zitafuata ikiwa ni pamoja na dhamana.
Nchi hii nidhamu ya uongozi imepotea kabisa, haiingii akilini RC anafanya kazi ya siasa. Huu wote ni mwendelezo wa siasa chafu za ccm na mawakala wake.
Jamani mkiangalia ile video ya pale IAA lazima ujiulize sababu ya Lema kukamatwa ni nini? Magesa anaonekana ana shinikizo pia nyuma yake.
Haya ni matumizi mabaya ya madaraka
Hii yote no matokeo ya kupeana vyeo kiswahiba....huyu mkuu wa mkoa ni mbumbumbu wa kutupwa! Ametengeneza uhasama kwenye kitu kilichohitaji a minute common sense! Kulikuwa na haja ya yote haya? Km ameshindwa ku-control wanachuo tu sidhani hata family yake anaiweza.....seuze mkoa! (Mind u this come from a pro CCM)