Mbunge Kainja na Wanawake wa Manispaa ya Tabora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE JACQUELINE KAINJA NA WANAWAKE WA WILAYA YA TABORA (KATA YA MPELA) MKOA WA TABORA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew tarehe 16 Julai, 2023 amefanya Mkutano wa Hadhara Kata ya Mpela Wilaya ya Tabora ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukabidhi Milioni 81,000,000 za kuwasaidia wanawake wajasiriamali kiuchumi.

Akiwa Kata ya Mpela Manispaa ya Tabora, Mhe. Kainja ametembelea kikundi cha akina Mama wanaoponda kokoto na kuwapatia vifaa vya kazi ikiwemo Makoti 30, Kofia 30, Nyundo 10, Glovu 30 za kufanyia kazi, Miwani ya kazi 30 na Shilingi Laki Mbili (200,000)

Katika ziara na Mkutano wa Hadhara wa Mhe. Kainja uliofanyika Kata ya Mpela, Wafanyabiashara wawili, Ndugu Mlutu na Mama Kape walimuunga mkono Mbunge Jacqueline Kainja Andrew kwa kuchangia kikundi cha akina Mama wanaoponda kokoto Shilingi Laki Nne (400,000) ili ziwasaidie kuinua uchumi wao.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara Kata ya Mpela Manispaa ya Tabora Mhe. Jacqueline Kainja aliwaambia wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi kuhusu suala la Uwekezaji wa bandari na Kampuni ya DP World na kusisitiza kuwa wasiwe na wasiwasi na mawazo ya Mheshimiwa Rais Samia kwani nia ya Serikali ya awamu ya sita ni nzuri sana na itakuwa na mafanikio makubwa kwa Taifa

Aidha, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew alizungumza sana mafanikio na maendeleo yaliyofanywa na yanayofanywa na Uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta zote.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(5).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(5).jpeg
    83.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.26.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.26.jpeg
    115 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(8).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(8).jpeg
    76.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(6).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(6).jpeg
    113.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.25(1).jpeg
    100 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.24.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-16 at 23.09.24.jpeg
    100.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-16 at 20.43.36(6).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-16 at 20.43.36(6).jpeg
    72 KB · Views: 1
Back
Top Bottom