Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,682
- 1,234
MBUNGE JACQUELINE KAINJA AHITIMISHA ZIARA KWA KUTEMBELEA WILAYA YA SIKONGE MKOA WA TABORA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew tarehe 17 Julai, 2023 amehitimisha ziara yake ya kutembelea Wanawake wa Wilaya zote za Mkoa wa Tabora ambapo alikuwa Wilaya ya Sikonge ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kukabidhi Milioni 81,000,000 za kuwasaidia wanawake wajasiriamali kiuchumi.
Mhe. Jacqueline Kainja amefanya ziara hiyo na kuhakikisha kila Kata ya Mkoa wa Tabora inanufaika na fedha za miradi kiasi cha Shilingi Milioni 81,000,000 ambazo zimegawiwa kwa kila Kata kuviwezesha kiuchumi vikundi vya akina mama wa UWT.
Mhe. Jacqueline Kainja pamoja na mambo mengine aliwasomea taarifa ya kazi akina Mama na kuwapatia taarifa yake ya kazi ya miaka mitatu huku akiwasisitiza Wanawake wa Baraza UWT Sikonge kuhakikisha fedha hizo zinazaa matunda na pia wapende kuwa na umoja.
Mhe. Jacqueline Kainja akiwa Wilaya ya Sikonge kuonana na Wanawake wa UWT aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Sikonge Mhe. Joseph George Kakunda pamoja na Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Sikonge
Aidha, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew alizungumza sana mafanikio na maendeleo yaliyofanywa na yanayofanywa na Uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta zote.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42.jpeg69.8 KB · Views: 7
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42(1).jpeg55.2 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42(2).jpeg72.1 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42(3).jpeg46.4 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42(4).jpeg84.4 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42(5).jpeg86.4 KB · Views: 6
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42(6).jpeg101 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-07-18 at 11.01.42(7).jpeg70.9 KB · Views: 4