Mbunge Suma Fyandomo ampongeza Dkt. Tulia kwa ushindi IPU

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma Fyandomo ametoa pongezi kwa ushindi mnono alioupata Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

"Pongezi za dhati kwa Spika wa Bunge letu, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Ushindi huu ni ushuhuda wa kazi kubwa unayoendelea kuifanya na imani wajumbe waliyonayo juu yako na nchi yetu" - Mhe. Suma Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

Itakumbukwa kuwa, Mhe. Spika Dkt. Tulia Ackson ameshinda kwa kishindo kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa kupata kura 172 dhidi ya wagombea wengine kutoka Somalia 🇸🇴 (Kura 11), Senegal 🇸🇳 (59) na Malawi 🇲🇼 (61).

Mhe. Suma Fyandomo amehitimisha salamu zake za Pongezi kwa kusema, "Mungu Ibariki Tanzania 🇹🇿. Mungu Mbariki Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mungu Mbariki Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

WhatsApp Image 2023-10-27 at 23.12.14.jpeg
 
Back
Top Bottom