Mbunge Joseph Mbilinyi Sugu mara moja moja acha "UTOTO"

Mbunge Joseph Mbilinyi Sugu mara moja moja acha "UTOTO"

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
5,080
Reaction score
3,770
Mitandao ya kijamii imekuwa kama ni moja ya nyenzo ya mawasiliano baina ya "mtu na mtu" na hata "mtu na watu"

Wafanyabiashara mbalimbali wamekuwa wakitumia mitandao hii kama njia moja ya mawasiliano na wateja wao hivyo hivyi na wanasiasa wamekuwa wakitumia mitandao hii kwa ajili ya kuwasiliana na wananchi wao au tuseme wapiga kura wao


ila kuna kitu nimekiona sio sawa kinachoendelea ndani ya mitandao hii ya kijamii.. nayo ni aina ya uwasilishwaji wa ujumbe kutoka kwa watu hao kwenda kwa wananchi wao..

sijui niseme ni usela, au utoto content inaweza kuwa ni nzuri ila sasa kwa jinsi ilivyoandikwa inakuwa ni utumbo kama sio ushuzi mpaka unakaa unasema huyu kweli na umri huu anaweza kufanya hili anayoyafanya

naweza kusema kuwa ni elimu ila pia nasema ni kutojitambua kwani kuna watu wengi hawana degree wala masters ila kwa umri wao wanafanya mambo ambayoni ya kistaarabu, uongeaji wao na uandishi wao unafuata staha

Mbunge wa Mbeya Mh Joseph Mbilinyi aliwaandikia maelfu ya wafuasi wake au tuseme wapiga kura wake message hii


CDM: We riding high in the sky with them choppers...n people on the ground all over understand n love our messages ...


sio mara moja au mara mbili uandishi wa Mh huyu unakuwa ni wa utata na usioendana na hadhi yake ya
mbunge na watu wa aina hii ndio wanafanya ubunge kuwa kama ni kazi ya wahuni na wavuta bangi ndio maana sitashangaa kesho Afande Sele nae anasema anataka kwenda bungeni.

wote tunaelewa sugu alikuwa msela na mwanamziki wa bongo fleva lakini pia aelewe nyakati zinabadilikka aangalie na muktadha wa kuandika na kuongea maneno ajue neno gani alitumie wapi akiwa chini ya kivuli gani

sugu kama anajua yeye shule haipo aajiri basi mtu wa kuwa anamwandikia alieyeenda shule mtu ajue ni jinsi gani ya kuandika na kufikisha ujumbe kwa watu na watu wakamwelewa....
sio anaandika ujumbe kwa wananchi wake au wapiga kura wake anaandika kama vile yuko studio na p funk wanarekodi nyimbo...

Ubunge una hadhi yake katika jamii na ndio maana wenzetu wana ma PA sidhani sugu kama ane... kama anae basi atakuwa ni MGOSI MKOLONI ambaye nae ni wale wale..

Sugu ajitambue ajue Mbeya, Tanzania wako wanamwangilia yeye basi aact kama Mbunge sio anakuwa kama Mvuta Bangi
kutoka Uswahilini na kuanza kuandika ushuzi kama wavuta bangi wengine tu , Sugu ajitofautishe yeye na mtoto wa miaka 16 ambaye kazoea kuvaa supra na suluari za kubana ambaye kakurupuka asubuhi na kuanza kupost utumbo

Aangalie mfano kutoka kwa wanasiasa wenzake kama vile
ZITTO KABWE, SLAA, NA MH JAKAYA MRISHO KIKWETE




Mh sugu wewe ni mtu mzima bwana acha utoto kuwa kama Mbunge basi ni hayo tu
 
mkuu nikas mtei niwe na wivu wa kike kwa kipi hasa ?
 
C.T.U Hujaeleweka mkuu. Kama una wivu na ubunge wake mwakani siyo mbali nenda Mbeya ukagombee.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna point hapa, kagombee Mbeya Mjini uone

wewe ndio ulivyoandika hakuna point hapo
mie sijaongelea kupendwa kwa mbunge sugu mbeyaa mjini mie nimeongelea kujitambua kwa Mbunge sugu kuwa yeye ni mbunge na act kama Mbunge sio kuact kama mtangazaji wa planet bongo
 
--------------------------------, ---------------!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wewe ndo' bure kabisa huna hata hiyo akili unayoita ya kivuta bangi, neno lipi hapo baya katika huo ujumbe wa sugu?
Next time tumia kichwa na sio mat.ako inapoleta sredi, Damn ----*n hater!


kwa mtu kama wewe huwezi kuona neno baya hata kidogo... ila kwa mtu ambaye maneno kama chaki, madawati, ubao kakutana navyo kwa muda wa zaidi miaka kumi na nane kaona kuna something wrong kwenye huo ujumbe


najua hata hili jibu hujalielewa
 
Hujaeleweka mkuu. Kama una wivu na ubunge wake mwakani siyo mbali nenda Mbeya ukagombee.

Mkuu wangu sina wivu na ubunge .... mie am trying to help kwani najua tuna watoto wanaotaka kuwa wabunge na wabunge wa sasa ndio ma role model wao...
naogopa wasije wakachagua wrong role model
 
Ameathiriwa na aina ya muziki anaoimba

Exactly... ila sasa ifike wakati a wake up na kuwa na (white) double personality (in good way)
sio (black) double personality ile ya kuumwa Dissociative Identity Disorder
Lol
 
Mimi nafahamu kabisa, SUGU BADO ANAVUTA. na anakunywa KONYAGI sana, inawezekana wakati anaandika huu ujumbe alikuwa keshapata mojawapo ya vilevi hivi au vyote kwa pamoja.
 
Hivi CCM huwa mnajiona wasomi sana au mnatanguliza chuki mbele kisa huyu ni Mbunge wa chama kingine?

Yaani "msomi" mzima unakaa kuandika uzi mrefu kwa suala ambalo kimantiki halina shida?

Halafu huelewi kuwa uongozi ni function na sio profession? Haya tueleze abbreviation ya hiyo PA na useme ons umuhimu gani kwa Mbunge.

Nyie MaCCM hivi lini mtaachana na paranoia ya kudhani ukiwa Mbunge wewe si binadamu? Mbona Mwigulu msomi lakini kaenda kuapishwa na skafu kubwa shingoni?

Hii nchi ons mijitu mijinga sana.
 
Mbunge kama huyu anayevuta kwanini yupo Bungeni??

ipo siku wabunge wa aina hii watataka muswada wa bangi ihalalishwe Tanzania...

ipo tu siku
 
Hivi CCM huwa mnajiona wasomi sana au mnatanguliza chuki mbele kisa huyu ni Mbunge wa chama kingine?

Yaani "msomi" mzima unakaa kuandika uzi mrefu kwa suala ambalo kimantiki halina shida?

Halafu huelewi kuwa uongozi ni function na sio profession? Haya tueleze abbreviation ya hiyo PA na useme ons umuhimu gani kwa Mbunge.

Nyie MaCCM hivi lini mtaachana na paranoia ya kudhani ukiwa Mbunge wewe si binadamu? Mbona Mwigulu msomi lakini kaenda kuapishwa na skafu kubwa shingoni?

Hii nchi ons mijitu mijinga sana.

Naomba nikujibu kwa kukuuliza swali..

Angekuwa ni Mbunge wa Chama kingine kaandika aliyoyaanidka
Au angekuwa ni Rais wa nchi angeandika kama sugu alivyoandika
Je ungekaa kimya kwa kuwa haina shida au ungekuja hapa na povu mdomoni, kumkosoa kama ambavyo huwa mnafanya.?
 
c.t.u M4C Chopper.jpgView attachment 134234View attachment 134235View attachment 134236
 
Last edited by a moderator:
Mimi nafahamu kabisa, SUGU BADO ANAVUTA. na anakunywa KONYAGI sana, inawezekana wakati anaandika huu ujumbe alikuwa keshapata mojawapo ya vilevi hivi au vyote kwa pamoja.

Bangi kuvuta sio noma mbona mawaziri wa Kikwete wengi tu tena wakiongoza wizara nyeti tunawajua kuwa wavutaji ganja kwa miongo mingi tu!!!
 
VIJANA WA MBEYA ULAJI HUO UNAKUFUATENI KIULAINI KABISA, MSIFANYE AJIZI, Kofia, T-shirt, Kanga, Ubwabwa, Kimpumu, Bia na Pesa ZOTE TIENI NDANI HALAFU WASUBIRIE HESABU ZA 2015

Chama cha mapinduzi kitafanya sherehe za kutimiza miaka 37 toka kuanzishwa kwake tarehe 05.02. 1977, sherehe hizi kwa mwaka 2014 zitafanyika katika mkoa wetu wa Mbeya tarehe 02.02.2014.

Ifuatayo ni taarifa ya shughuli zitakazofanyika katika kufanikisha sherehe hizi:-




  • Tarehe 25 – 26 January 2014 maafisa wawili kutoka makao makuu watawasili katika mkoa wa Mbeya.




  • Tarehe 28 january 2014, katibu wa NEC siasa na uenezi ndugu Nape Moses Nnauye atawasili katika mkoa wa Mbeya.




  • Tarehe 30. 01. 2014 makamu mwenyekiti bara ndugu Philip Mangula, pamoja na sekretarieti ya taifa watawasili katika mkoa wa Mbeya.




  • Tarehe 31, 01, 2014 saa 4:00 hadi saa 7:00 mchana makamu mwenyekiti bara Ndugu Philip Mangula pamoja na
wajumbe wa sekretarieti ya taifa watafanya ziara katika wilaya ya Mbeya mjini ili kuangalia uhai wa chama katika matawi na utekelezaji wa ilani ya uchagizi wa CCM, pia watashiriki shughuli za ujenzi wa taifa.



  • Tarehe 31, 01 2014 saa 8:00 hadi 12:00 jioni, katibu mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana atakutana na vijana wajasiliamali wa bodaboda na bajaji.




  • Tarehe 01,02, 2014 mwenyekiti wa CCM taifa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya mrisho kikwete atawasili katika mkoa wetu wa Mbeya, na tutampokea kwenye uwanja wa Ndege wa Songwe.




  • Tarehe 01,02,2014 saa 08:00 mchana hadi saa 12:00 jioni katibu mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana atakutana na wana CCM kutoka vyuo vikuu vilivyoko katika mkoa wa MBEYA.


  • Tarehe 02,02,2014 saa 12:00 alfajiri mpaka saa 02 kamili asubuhi yatafanyika matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na mwenyekiti wa CCM taifa ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, matembezi hayo yatakayoanzia Soweto na kupita mwanjelwa, sinde yataishia ofisi kuu ya CCM mkoa wa Mbeya.




  • Tarehe 02,02,2014 saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni sherehe za miaka 37 ya CCM zitakazofanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.




  • Tarehe 03, 02, 2014 viongozi kuanza kuondoka katika mkoa wa Mbeya.

Imetolewa na:

Bashiru S. Madodi
Katibu siasa na uenezi mkoa wa Mbeya.
 
Back
Top Bottom