Mbunge Joseph Mbilinyi apata ajali milima ya Kitonga

Mbunge Joseph Mbilinyi apata ajali milima ya Kitonga

TUMSHUKURU MUNGU
MH Sugu amepata ajali kitonga ila yupo salama
 

Attachments

  • IMG-20150110-WA0013.jpg
    IMG-20150110-WA0013.jpg
    121.4 KB · Views: 1,159
  • IMG-20150110-WA0014.jpg
    IMG-20150110-WA0014.jpg
    122.2 KB · Views: 1,049
Mungu tunakushukuru kwa kumlinda na kumuepusha kamanda Sugu na madhara zaidi...
 
Toyota Landcruiser VX100, hicho kitu hakuna, kuna tatizo tu la dereva aliyekuwa akiendesha.
Ukiniambia mwendo kasi , kupinduka kwa sehemu hizo rahisi sana, wiki mbilizilizopita nimepita hapo mara nne, kuna hairpin bends ambazo zinawachukua wazembe.
Kwa gari dogo kupinduka lazima mwendo kasi tu.
mkuu hakuna gari lisilopata hitilafu kamwe. Mengine ni mbwembwe tupu.
 
Toyota Landcruiser VX100, hicho kitu hakuna,
what you mean kitu hicho hakuna, VX100 hazi feli break? Kama ma pads na ma fluids yamekwisha litashika tu breki? Zinafeli break za ndege itakuwa VX? Vipi Mkuu.

Anyhow, mi ningeanza na sobriety test, lakini kwa bongo by the time polisi anafika na maji yenyewe yashakutoka kichwani
 
amenusurika ajali mbaya!!!mbona naona ajali imetokea sasa kanusurika ajali au...
 
Toyota Landcruiser VX100, hicho kitu hakuna, kuna tatizo tu la dereva aliyekuwa akiendesha.
Ukiniambia mwendo kasi , kupinduka kwa sehemu hizo rahisi sana, wiki mbilizilizopita nimepita hapo mara nne, kuna hairpin bends ambazo zinawachukua wazembe.
Kwa gari dogo kupinduka lazima mwendo kasi tu.
brake zaweza fail hata kwa gari ya aina hiyo,kuna ajali nyingine zinasababishwa na nguvu zisizo za kibinadamu, nimewahi kupata ajali iliyosababishwa na brake ku fail na stering kutokata kwa gari aina ya Nissan Patrol ambayo ilikuwa sawa hadi nikagonga gari lilokuwa limesimama mbele,bahati nzuri sikuwa kwenye spidi na barabara wala si ya mteremko,na baada ya ajali stering ikawa sawa,na brake zikafanya kazi kama kawaida,kwa hiyo si lazima iwe ni uzembe wa dereva ktk ajali
 
msiwe wepesi wa kudhani ni hira za watu cha msingi ni kumuomba sana mungu kanusulika achen mira potovu elimiken
 
Mbunge wa Mbeya mjini Mr Sugu na rafiki yake wakiwa kando ya gari lao baada ya kupinduka katika mteremko wa Kitongo leo

................................................................................................
MBUNGE wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Mr Sugu (Chadema) amenusurika kifo baada ya gari lake kupinduka katika mlima wa Kitonga wilaya ya Kilolo kwenye barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea mchana wa leo wakati gari la mbunge huyo likiwa na watu wengine wanne likitokea Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam .

Hata hivyo vyanzo vya habari hizi viliueleza mtandao huu wa Mzee wa matukio daima kuwa mbunge huyo amepatwa na michubuko kiasi na hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akimethibitisha kutokea kwa ajali hiyo japo amesema taarifa kamili zitapatikana mara baada ya askari waliokwenda eneo la tukio kurejea.
 
Kimbia fasta ukianguka ukiumia inuka vumilia!!!!!! Amka kamanda tuendelee na vita!!!
 
Huduma yake bado inahitajika Mbeya, swala la kifo bado sana.
 
Back
Top Bottom