Mbunge Janejelly James Ntate Asifu Miaka Miwili ya Rais Samia Madarakani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Viti Maalum, Mwakilishi wa Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujikita kuangazia katika suala la Ajira na Upandishwaji vyeo.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilitenga Shilingi Bilioni 26,297,541,175.00 kwa ajili ya Ajira mpya 32,604 ili kuziba pengo la uhaba wa watumishi na kuongeza Kasi ya maendeleo.

Kipaumbele cha ajira zilizotolewa ilikuwa ni katika Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Kada zingine zilizokuwa na pungufu.

Upande wa upandishwaji vyeo Serikali ya awamu ya sita inayotokana na CCM ilitenga Shilingi Bilioni 23,078,224,169.50 ili kuwapandisha watumishi 92,619, na bado wanaendelea kupandisha vyeo watumishi.

Zaidi ya hiyo Mheshimiwa Rais wetu kipenzi cha Watumishi nchini amaruhusu mwaka wa fedha wa 2023/2024 itengwe bajeti ya kuwapandisha vyeo watumishi wote waliopandishwa vyeo 2016 na 2017 halafu vikafutwa.

Hapa niwapongeze pia Mhe. Jenister Mhagama na menejimenti yake yote ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora kwa kupokea maelekezo ya Mheshimiwa Rais na kuyatekeleza Kwa uharaka.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kafanya mambo mazito kwa watumishi.

WhatsApp Image 2023-03-15 at 11.31.41.jpeg
 
Back
Top Bottom