Mbunge wa Wafanyakazi Janejelly Ntate Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa Miaka Miwili Madarakani kwa Aliyoyafanya kwa Watumishi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,886
938

MBUNGE WA WAFANYAKAZI JANEJELLY NTATE AMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA MIAKA MIWILI MADARAKANI KWA ALIYOYAFANYA KWA WATUMISHI

Mbunge wa Viti Maalum, Mwakilishi wa Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza Miaka Miwili Madarakani kwa ushindi hasa kwa kuangalia namna anavyoshirikiana na Wafanyakazi.

"Watumishi walioondolewa kwa vyeti feki, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa huruma kabisa kwa waliokuwa watumishi wake, na kwa kufundisha tendo la msamaha alielekeza walipwe mafao yao waliyokuwa wanachangia wenyewe."

"PSSF, mfuko unaohusika na mafao ya watumishi wa Serikali walipokea madai ya waliokuwa watumishi 12,007. Hadi sasa mwaka 2023 wamelipwa watumishi 11,416 fedha zilizotumika ni Shilingi Bilioni 29,267,238,188.25/=."

"Hadi kufikia tarehe 13.3.2023 wamebakiza idadi ya walipwaji 591 tu na hawa ni ambao taarifa zao hazijafika kwenye mfuko. Niwapongeze sana PSSF chini ya Wizara ya Kazi, Ajira na wenye Ulemavu Kwa kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais kwa uharaka"

Hapa mimi kama mwakilishi wa watumishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba ya walipwaji niseme nini zaidi ya asante kwa zawadi ya miaka miwili kutoka Kwa Mama Samia. Nitaendelea kuwahabarisha mengi hadi tunafikia kilele cha tarehe 19.03.2023.

WhatsApp Image 2023-03-15 at 10.42.45.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-15 at 11.31.40(1).jpeg
 
Back
Top Bottom