Mbunge Janejelly James Ntate aomba Sheria za Utumishi wa Umma zilizopitwa na wakati zifanyiwe marekebisho

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

WhatsApp Image 2023-04-19 at 17.29.05.jpeg

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate amechangia bajeti ya Wizara ya Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora na kuiomba Wizara ifanye baadhi ya Sheria.

Mhe. Ntate ameiomba Wizara ya Utumishi ikaangalie upya sheria, kanuni na miongozo iliyopitwa na wakati ifanyiwe marekebisho ndani ya Utumishi wa Umma ili kukidhi mahitaji ya sasa ya watumishi wa umma.

Mhe. Ntate amesema kazi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya Ajira ni Kuajiri. Wizara zisifanye kazi ya kusimamia ajira ili Serikali iwe na kanzidata ya kutunza watu walioomba ajira.

Aidha, Mhe. Ntate ameomba viongozi warejeshewe sehemu zao za kupumzikia mfano Leaders Club DSM na club zote ambazo zilikuwa kila Mkoa, pia aliomba ijengwe leaders Club Dodoma.

Mhe. Ntate ameiomba Serikali kuwa Chuo cha Sekretare Tabora, IDM, Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni na Mzumbe visibadirishiwe dhana ya kuanzishwa kwake ili watumishi wa umma wakafundishwe maadili.
 
Huko ndiko kunakofanyika interview na kupatikana teuzi na viti maalum. Club zirudishwe.
 
Back
Top Bottom