Serikali Kuendeleza Kutoa Mafunzo kwa Watumishi wa Umma Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Je, ni lini Serikali itarejesha utaratibu wa mafunzo elekezi ya Uongozi, Utawala Bora na Uadilifu kwa Watumishi ambao wamefikia ngazi ya Afisa Mkuu ili wanapopata nafasi za Uteuzi waweze kutumika ipasavyo?" - Mhe. Janejelly James Ntate, Mbunge wa Viti Maalum (Anayewakilisha Wafanyakazi Nchini)

"Kwa mujibu wa Kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma na ibara (4-8) inampa Mamlaka Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha Utumishi wa Umma unakuwa ulio Bora, Weledi na kuwahudumia wananchi" - Mhe. Ridhiwani Kikwete, Naibu Waziri Ofisi ya Rais - Utumishi

"Namhakikishia Mbunge Janejelly James Ntate na Bunge kuwa Serikali imeendelea na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa watumishi wote ambao wanakuwa katika ngazi za uteuzi ili kuwa katika viwango Bora vya kutoa huduma kwa wananchi" - Mhe. Ridhiwani Kikwete, Naibu Waziri Ofisi ya Rais - Utumishi.

 
Back
Top Bottom