Milioni 13 za Mbunge wa Ulanga/Mahenge Neema kwa Wachimbaji Wadogo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MILIONI 13 ZA MBUNGE ULANGA NEEMA KWA WACHIMBAJI WADOGO

Mbunge wa jimbo la Ulanga Salim Alaudin Hasham ametoa kiasi cha shilingi milioni kumi na tatu (13,000,000) kwaajili ya malipo ya leseni za wachimbaji wadogo wanaofanya kazi zao za uchimbaji wa madini katika kata ya Lukande wilayani humo.

Hatua hiyo imekuja baada ya wachimbaji hao kulalamika kwa mbunge kuwa wanashindwa kufanya shughuli zao za uchimbaji kutokana na kushindwa kulipa fedha ya leseni jambo lililopelekea kuzuiwa kufanya shughuli hizo katika maeneo hayo huku wao wakitegemea kazi hiyo kwaajili ya utafutaji wa riziki zao.

Akiwasilisha kero hiyo kwaniaba ya wachimbaji hao diwani wa kata hiyo ya Lukande Novatus Majiji amesema wachimbaji wana mchango mkubwa sana katika kata hiyo hivyo kwa zuio hilo la kuacha uchimbaji kutokana na kukosa fedha ya leseni itasababisha vijana wengi kushindwa kuendesha maisha yao.

Akizungumza katika mkutano wake na wananchi mbunge wa jimbo hilo la Ulanga Salim Alaudin Hasham amesema yeye binafsi atawalipia kiasi hicho cha fedha ili waendelee na shughuli zao na amewataka kuwa makini pindi wanapopata madini wakumbuke kulipia leseni zao ili kuondokana na changamoto ya zuio hilo kwa wakati mwengine kutokana na deni la leseni.

Kata ya Lukande ina zaidi ya wachimbaji wadogo 300 ambao wanachimba madini ya vito katika kata hiyo.
WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.42.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.41(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.41.jpeg
    64.5 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.40(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.40(1).jpeg
    65.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.40.jpeg
    66.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.39(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.39(2).jpeg
    77.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.39(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-19 at 17.18.39(1).jpeg
    47.9 KB · Views: 5
Back
Top Bottom