kwahio unataka kusemaje? Sijakuelewa
Rejea mchango wangu kwamba Mtanzania anajitambua na anajua haki zake na wapi pa kuzipata, Kikatiba, akizikosa. Wewe bado kwa kushabikia wanasiasa wakutumie kufanikisha malengo yao!
Hivi hujatambua tu kuwa viongozi wa CHADEMA, baada ya kushindwa kuwashawishi Watanzania kuwaingiza Ikulu, kwa kauli mbiu ya 'mabadiliko Lowasa - Lowasa nabadiliko', wanahaha sasa kutafuta jinsi ya kuvuruga juhudi za 'mabadiliko' ya kweli ya Rais Magufuli na viongozi wenzake katika Serikali ya awamu ya 5.
Kuna Watanzania wanajifanya kipofu wakati macho yao yaona kinachoendelea. Wapo wengine wanajifanya hawasikii wakati maasikio yao mazima yanasikia. Ila naamini wana matatizo ya kuchambua pumba na mchele, kama ilivyotokea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kuzungusha mikono.
Muda wa siasa za Kampeni umekwisha wasubiri 2020. Kwa sasa, vyama vya upinzani:
1) Vijiimarishe kaa siasa za maendeleo (kutimiza ahadi) kwenye majimbo waliyopewa ridhaa na Watanzania kuongoza. Kama Serikali, kwa njia yoyote itawawekea vikwazo, halali kuhamasisha Wananchi kupinga hilo.
2) Vitumie mafanikio ya maendeleo katika majimbo hayo kujijenga kisiasa.
3) Hata kama Serikali haikosilewi moja kwa moja, kushindwa kwake kutimiza ahadi zake, kutumike kuiondoa madarakani 2020.
SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA KAMWE