Mbunge Edward Ole Lekaita Asisitiza Matumizi ya Uchumi wa Kidigitali & Apongeza Ujio wa Minara ya Mawasiliano kwenye Kata 12 za Jimbo la Kiteto

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE EDWARD OLE LEKAITA ASISITIZA MATUMIZI YA UCHUMI WA KIDIGITALI & APONGEZA UJIO WA MINARA YA MAWASILIANO KATIKA KATA 12 ZA KITETO

"Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka fedha nyingi sana kwenye Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Nampongeza Waziri Nape na Naibu Waziri Eng. Kundo tukianzia na hafla ya utiaji saini Mikataba ya Minara 158. Sisi tunaotoka Vijijini mmetufurahisha sana" - Mhe. Edward Ole Lekaita

"Uchumi wa Kidigitali (Digital Economy) ni kitu muhimu sana. Ripoti ya Benki ya Dunia (World Bank) inasema Uchumi wa Kidigitali umefikia kati ya Bilioni 14 mpaka Bilioni 16 asilimia ya GDP. Ni lazima tuendeleze na tuweke pesa zaidi" - Mhe. Edward Ole Lekaita

"Kiteto, mwaka 2021 niliandika Ripoti nikaleta Kata 25 Kiteto zilikuwa na shida ya Mawasiliano lakini kwenye bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kata 12 zipo kwenye Minara. Kata ya Laiseri ilikuwa haina Mnara hata mmoja lakini Vijiji vyote vimo. Kata ya Laiseri, Lengatei, Loolera, Mabungu, Lamerok, Partimbo, Sunya, Loltepesi, Songambele, Peresa, Njoro, Dosidosi na Ndirigish na Vijiji karibu 23" - Mhe. Edward Ole Lekaita

"Liko jambo la wizi unaotokana na mitandao, limekuwa ni janga kidogo na linasumbua watanzania waliowengi. Ninaomba tuendelee kuongeza Teknolojia ili wezi na matapeli wa mitandao wasiwatapeli watanzania" - Mhe. Edward Ole Lekaita

"Kwa mujibu wa sheria tunatakiwa kuripoti kosa kwa matapeli wanaotupigia Mitandaoni na tumekuwa tukiripoti kwa makampuni ya simu ambacho hatupati ni marejesho (feedback) kutoka makampuni ya simu. Ni lazima makampuni ya simu yatuambie kama wateja kwamba simu uliyoripoti wao wamefanya nini na nini" - Mhe. Edward Ole Lekaita
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-19 at 22.17.04.mp4
    46.9 MB
Back
Top Bottom