Mbunge Devotha Mburarugaba: Wanawake wakienda kuomba mkopo wanaaambiwa intaneti ipo chini

Mbunge Devotha Mburarugaba: Wanawake wakienda kuomba mkopo wanaaambiwa intaneti ipo chini

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mbunge viti Maalum wa Kagera Devotha Daniel Mburarugaba kwenye kipindi cha maswali na majibu bungeni leo Februari 5, 2026 amehoji Serikali imeweka mikakati gani kuhahakikisha maafisa wanapata vitendea kazi kwani wanawake wakienda kuomba mikopo wanaambiwa intaneti ipo chinihawawezi kupata huduma.

Swali hilo limejibiwa na Naibu waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Reuben Kwagilwa akieleza kuwa kwa sasa kila mwaka fedha zinapopelekwa Fedha za OC Kwenye mikoa na halmashauri serikali imekuwa ikitenga fedha kuwawezesha maafisa wa Maendeleo ya Jamii kuweza kunua bando ili kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha ameeleza serikali inafanya jitihada kujenga mkongo wa mawasiliano ili kuhakikisha kila eneo katika taifa linapata intaneti.



 
Back
Top Bottom