mwakajilae
Member
- Mar 11, 2011
- 58
- 46
Mh Cecilia Paresso[mb] Karatu,jana amepata rasmi baraka za wananchi wa Karatu,huku akianza kazi kwa kishindo mara baada ya kusindikizwa na msafara wa magari zaidi ya 60 na piki piki 100,Makubwa yaliyojitokeza katika Viwanja vya Mbowe Wilayani Karatu ambapo mkutano wa hadhara mkubwa ulifanyika.
Ni hotuba aliyoitoa Mbunge huyo kijana kwa kutekeleza yale ambayo serikali ya CCM imeshindwa kuyafanya hasa kupitia sera inayosimamia Jinsia,wanawake na Watoto, ambapo ni pamoja na kuwatambua watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Mh Cecilia Paresso jana ameamua kuwasomesha watoto 100 ambao ni Yatima,lakini pia katika kuhakikisha anafanya kazi katika mazingira ya kisasa kwa kuwa na mfumo wa kiuwajibikaji ndani ya Chama cha CHADEMA,Ameanua kulipia kodi zote za pango la ofisi za Chama na mabaraza yake yote hapo wilayani, ili watendaji na viongozi wa chama kutumia muda wao mwingi katika kuimarisha chama na kuratibu shughuli za kiofisi katika mazingira yaliyo salama kwa ustawi wa chama na jamii kwa ujumla.
Mbunge huyo kijana anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika mhimili wa bunge unaojadili uhai wa Taifa na wananchi wake ambao kwa ujumla hawana mahusiano mazuri na Serikali yao iliyo wasaliti na kuwadharau.
Lakini wakati huo huo CHADEMA kimempata mbunge ambaye anaushawishi mkubwa kwa wanawake na vijana kwa ujumla,hivyo kupelekea Chama hicho kuzidi kujiwekeza kwa vijana na safari hii kwa wanawake zaidi.
CHADEMA ni chama ambacho kimekuwa tishio kubwa kwa uhai wa Chama cha Mapinduzi[CCM] na kuwa Tumaini kwa wanyonge walio athiliwa na mfumo wa kimatabaka wa chama cha Mapinduzi.