Mbunge Cecilia Paresso atekeleza yaliyoshindikana kwa serikali ya CCM iliyo na miaka 50 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Cecilia Paresso atekeleza yaliyoshindikana kwa serikali ya CCM iliyo na miaka 50

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwakajilae, May 7, 2012.

 1. m

  mwakajilae Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh Cecilia Paresso[mb] Karatu,jana amepata rasmi baraka za wananchi wa Karatu,huku akianza kazi kwa kishindo mara baada ya kusindikizwa na msafara wa magari zaidi ya 60 na piki piki 100,Makubwa yaliyojitokeza katika Viwanja vya Mbowe Wilayani Karatu ambapo mkutano wa hadhara mkubwa ulifanyika.

  Ni hotuba aliyoitoa Mbunge huyo kijana kwa kutekeleza yale ambayo serikali ya CCM imeshindwa kuyafanya hasa kupitia sera inayosimamia Jinsia,wanawake na Watoto, ambapo ni pamoja na kuwatambua watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu.

  Mh Cecilia Paresso jana ameamua kuwasomesha watoto 100 ambao ni Yatima,lakini pia katika kuhakikisha anafanya kazi katika mazingira ya kisasa kwa kuwa na mfumo wa kiuwajibikaji ndani ya Chama cha CHADEMA,Ameanua kulipia kodi zote za pango la ofisi za Chama na mabaraza yake yote hapo wilayani, ili watendaji na viongozi wa chama kutumia muda wao mwingi katika kuimarisha chama na kuratibu shughuli za kiofisi katika mazingira yaliyo salama kwa ustawi wa chama na jamii kwa ujumla.

  Mbunge huyo kijana anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika mhimili wa bunge unaojadili uhai wa Taifa na wananchi wake ambao kwa ujumla hawana mahusiano mazuri na Serikali yao iliyo wasaliti na kuwadharau.

  Lakini wakati huo huo CHADEMA kimempata mbunge ambaye anaushawishi mkubwa kwa wanawake na vijana kwa ujumla,hivyo kupelekea Chama hicho kuzidi kujiwekeza kwa vijana na safari hii kwa wanawake zaidi.

  CHADEMA ni chama ambacho kimekuwa tishio kubwa kwa uhai wa Chama cha Mapinduzi[CCM] na kuwa Tumaini kwa wanyonge walio athiliwa na mfumo wa kimatabaka wa chama cha Mapinduzi.
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  well done madame uzi huohuo hadi tulibandue gamba!!!
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mbona hii ni kama kampeini ya kumg'oa mbunge wa Karatu Mheshimiwa Natse?
  Hapa kunanukia mgogoro wa ndani, CDM muwe macho.
   
 5. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hongera sana Mama fanya kazi
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Huyo Dada ni noma na 2015 ipon kazi hapo, yule mbunge wa kuchaguliwa anaweza pigwa chini, na Karatu linaweza kuwa jimbo litakalo kuwa na kinyang'anyiro kigumu sana kwenye kumpata mtu wa kugombea kwa tiketi ya CHADEMA, make kule kuna vichwa vya kutosha, mwenyekiti wa halimashauri naye anapiga jeramba na yeye ni mtu anaye kubalika sana, kwa kifupi karatu kutakuwa na mtifuano wa kufa mtu,
   
 7. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa serikali ya ccm imeshindwa kulipa kodi za chadema za pango kama alivyofanya yeye na kamwe haitoweza
   
 8. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Kitakachosaidia ni doctor wa ukweli kukaa mbali na moto huu maana ana mgongano wa maslahi mkubwa.

  Doctor anamkubali sana mbunge wa sasa natse kwa sababu alishughulika kumsahwishi agombee na hata kumwombea ruhusa kwa Askofu wake.

  Doctor ni rafiki sana na Mwenyekiti wa Halmashauri na wametoka mbali sana katika kukiimarisha chama, na wanaheshimiana kwa kutanguliza chama kwanza.

  Doctor ni rafiki wa kweli wa mbunge Parseko tangu akiwa diwani na yeah! ni marafiki wanaoheshimiana.
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  kwa kuwa unakiri wanaheshimiana, umepaswa kukumbuka kuwa kimsingi wote wana heshima, hatimaye wataheshimu maamuzi ya wapiga kura wakati wa uteuzi chamani. peopleeeeeeez. . . . . . .
   
 10. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kama wananchi wataamua hivyo na itakuwa hivyo. Ukiwa katika chama cha kidemokrasia hutakiwi kuogopa kivuli chako na kukataza wengine kusaidia jamii ya wenye mahitaji kisa tu watakung'oa. Haya mambo yanabakia kule kule ccm kwa kuwa wako katika hatua za mwisho za uhai wa chama. Wakati ukifika kila mwenye nia ya kugombea jimbo atachukua fomu, hakuna haki miliki ya jimbo.

  Nitashangaa sana kama kutazuka mgogoro mtu atakapoomba kugombea jimbo lolote kama katiba inavyomruhusu, yule atakayedhani ananyang'anywa jimbo ujue hana elimu ya uraia.
   
 11. G

  Galaticos Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  moto wa chadema unatisha kama simba sc.....
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ukiwa na watu competent ni "a blessed problem". So I will be watching Karatu more closely
   
 13. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  chama kwanza urafiki badae
   
 14. M

  Makupa JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Cdm ina takribani miaka ishirini na sidhani kama kuna dalili yoyote kuishinda ccm 2015
   
 15. K

  Kongi JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Hii habari imekaa kidaku na kishabiki sana bana... Pamoja na kuwa mimi ni CHADEMA sikubaliani kabisa na huyu dada kuwa mbunge viti maalumu kutoka mkoa wa Arusha wakati hicho kiti kilikuwa kinashikiliwa na marehemu Regia kutoka Mororgoro. Ina maana chama kweli mlikosa mtu kutoka mikoa kama Tabora, Dodoma, Tanga au huko kusini mikoa ambayo hatuna mbunge hata mmoja????

  Nasema tena kwa sauti kubwa sikubaliani na huyu Pareso wa Arusha kuchukua kiti cha marehemu Regia wa Morogoro...
   
 16. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Umejiridhisha kwanza na utaratibu uliotumika kabla ya kutokubaliana na uteuzi huu?
  Kwenye hili CDM hawakuwa waamuzi bali Tume ya uchaguzi kufuatia orodha waliyopelekewa na CDM 2010.
   
 17. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wewe sasa unalala kuleta mgogoro usio na kichwa sala miguu hapa...au ulitaka awe Kama Yule kila za aliyejadiliwa Jana humu jukwaani?.
   
 18. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  vp anajiandaa kuchukua jimbo gani? Make apo kuna mzee natse kajaa,.
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Muanzisha thread mpe cheo chake kamili Mbunge Cecilia Paresso, ni Mbunge wa viti maalum umeandika utadhani hulijui hilo.

  Hicho unachosema kafanya mbona kawaida tu mkuu au umeamua kumpamba kuna wabunge wengi wanasomesha watoto ukitaka orodha yao takupa.

  Kusomesha watoto 100 shule za kata wala sio kitu cha kujivunia, ada ya shule za kata ni 15,000 kwa mwaka.

  15,000 x 100= 1,500,000
   
 20. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Peoplessss!ngoja walau nichome kg 2 za nyama ngombe hapa mnadan karatu leo tar 7,karatu ina vichwa,karatu ni noma!chimbuko la upinzani tangia enzi za nyerere!
   
Loading...