Mbunge Bupe Mwakang'ata aibana Serikali kuhusu Matibabu ya Afya kwa Wazee

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza gharama za matibabu kwa akina Mama wanapokwenda Kliniki Sumbawanga?" - Mhe. Bupe Nelson Mwakang'ata, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa

"Sera ya Afya ya mwaka 2007 kifungu cha tano (3)(4c) kinaeleza kuwa huduma za afya ya uzazi ikiwemo kuhudhuria Kliniki wakati wa uchungu, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua pamoja na uzazi wa mpango vitakuwa vikitolewa bila malipo." - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

"Naomba kutoa wito kwa watumishi katika vituo vya kutolea huduma za Afya kutowatoza gharama za uzazi wanawake wote wanaofika vituoni kupata huduma za Afya ya uzazi" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

"Ni kwanini Sera hii haitekelezeki kikamilifu kwasababu wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka 5 bado wanalipishwa kwenye suala zina la Afya" - Mhe. Bupe Nelson Mwakang'ata, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa

"Sera ya wazee chini ya miaka 60 bado wanatozwa fedha wanapokwenda kutibiwa, Je, Sera hii kwanini haitekelezeki? - Mhe. Bupe Mwakang'ata, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa

"Kuna kipindi tulipitia kwenye shida ya upungufu wa dawa. Inapokuwepo upungufu wa dawa na vifaa tiba inaathiri eneo hili. MSD ikipata mtaji badala ya kutegemea fedha kutoka kwenye vituo mnyororo wa upatikanaji wa dawa hautakatika" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

"Tumeagiza kila kituo cha Afya, Zahanati, Hospitali kuwepo na dirisha la Wazee na tunawaomba Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wasimamie eneo la akina Mama na wazee kuhakikisha takwa la kisera linatekelezwa" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

WhatsApp Image 2023-06-01 at 18.19.16.jpeg
WhatsApp Image 2023-06-01 at 18.19.17.jpeg
 
Back
Top Bottom