Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,890
- 939
BUPE MWAKANG'ATA - MASWALI NA MAJIBU BUNGENI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa na Mwanzilishi wa Bupe Foundation, Mhe. Bupe Mwakang'ata ameuliza swali Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambalo kwa niaba ya Waziri lilijibiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Mhandisi Godfrey Kasekenya
"Ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Mloo - Kilimatundu - Ilemba - Mtowisa - Majimoto, ni lini itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?" - Mhe. Bupe Mwakang'ata
"Barabara ya kipande cha Mloo hadi Kamsamba imewekwa kwenye mapendekezo ya bajeti, ilikuwa ni ahadi, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliagiza lakini upande wa Kilimatundu hadi Muze tumeshaanza ujenzi kutoka Ntendo hadi Muze kwenda Kilimatundu, ni barabara ndefu yenye urefu usiopungua Kilomita 300" - Mhe. Mhandisi Godfrey Kasekenya