Mbunge bibi miaka 60, aolewa na kijana wa miaka 26

Mbunge bibi miaka 60, aolewa na kijana wa miaka 26

Hebu tuache unafiki ukisoma vizuri utagundua kuwa huyu mama alitumia umaskini wa kijana huyu kumpata kimapenzi,tujiulize huyu mama anaweza kumzalia huyu kijana mtoto?
Kawaida mwanamme hakui kwa mwanamke lkn mwanamke akishafikisha umri wa 50+ labda aolewe na mzee mwenzie aliyekwisha zaa ili kupeana kampani.
basi olewa wewe mkuu sioni kinachokusumbua binafsi najua mapenzi hayana umri wala utajiri kama mtu kafikisha umri wa utu uzima habari ya uzee hayazungumzwi kisheria.
 
Mbunge wa ccm aolewa na kinda (pata full story mwanzo - mwisho)
[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD]Mbunge CCM aolewa na kinda

• Ana miaka 60, kijana 26


na Martin Malera

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="class: cms_table"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD="bgcolor: #ffffff"]MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60), amejikuta kwenye kashfa nzito ya kufunga ndoa na kijana, kinda wa miaka 26, Michael Christian.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG), linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge wanaoifahamu pamoja na majirani wanaoishi na mbunge huyo.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya wanandoa hao na majirani wanaowazunguka, vililiambia gazeti hili kuwa ndoa hiyo ilifungwa Septemba Mosi mwaka 2011, na imebaki kuwa siri kabla ya wawili hao kukorogana.
Kabla ya wawili hao kuamua kufunga ndoa, mbunge huyo kutoka mkoani Rukwa, mwenye makazi yake Bagamoyo mkoani Pwani, alikuwa akimtumia Michael kwenye shughuli mbalimbali na muda wote alikuwa akiishi nyumbani kwa mbunge huyo.
Inaelezwa kuwa mbunge huyo ambaye ana familia ya watoto wawili ambao kiumri wanalingana na Michael, alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo kwa siri kubwa na baadaye alifanikiwa kumshawishi wafunge ndoa huku akimuahidi kumpa huduma mbalimbali anazotaka.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao waliamua kufunga ndoa katika Kanisa la TAG baada ya mbunge huyo kufanikiwa kumshawishi Mchungaji Rwakatare kwamba ndoa hiyo itakuwa siri, hasa kutokana na tofauti ya kiumri kati yao.
Hata hivyo ndoa hiyo kwa sasa imekumbwa na mgogoro mkubwa, huku mbunge huyo akidaiwa kuzuia kila kitu cha mumewe huyo, hasa vyeti vyake vya shule kama njia ya kumbana warudiane.


Siku ya harusi



Kwa mujibu wa mashuhuda wa harusi hiyo ya aina yake, mbunge na kijana huyo walikwenda kanisani wakiwa wawili bila mashahidi kama ilivyo kawaida, na ndoa hiyo ilifungwa katika ofisi ya kanisa na sio ndani ya kanisa.
Mashahidi wa ndoa hiyo waliitwa hapo hapo kanisani na walisimamia na kushuhudia utiaji saini wa cheti cha ndoa na kisha wanandoa hao kutawanyika kwenda kwenye fungate (Honey Moon). Hakukuwa na sherehe baada ya kufungwa ndoa.
Inadaiwa kuwa hakukuwa na ndugu yeyote wa maharusi hao aliyeshuhudia tukio hilo la kihistoria la wawili hao kuunganishwa na kuwa mwili mmoja.


Kauli ya Bwana harusi



Tanzania Daima Jumatano, lilifanikiwa kumpata Michael, ambaye katika mazungumzo yake alikiri kufunga ndoa na mbunge huyo Septemba Mosi mwaka 2011, lakini kwa sasa wametengana kutokana na sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.
"Mimi nadhani hili ni jambo binafsi, sio vizuri kulizungumza hadharani ila kweli nilifunga naye ndoa maana inaonekana mnajua mambo mengi kunihusu, na ni kweli kwa sasa tumeachana," alisema kwa kifupi.
Alisema walikutana na mbunge huyo Bagamoyo wakati alipokuwa akifanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali ya wilaya hiyo kama muuguzi mkunga wakati mbunge huyo akiwa muuguzi mkuu wa wilaya katika hospitali hiyo.
Alipoulizwa sababu za kukubali kufunga ndoa na mama wa umri wa miaka 60 wakati ana miaka 26 na sababu za ndoa hiyo kuvunjika, Michael alisema ana historia ndefu katika maisha yake kwani alizaliwa yatima na amekua na kulelewa kwa ufadhili wa kituo cha Safina Street Network.
"Katika mazingira niliyokulia, unaweza kujua kwanini nilikubali kuingia kwenye ndoa hiyo. Sina ndugu hata wa kunishauri. Hata hivyo, hayo tuyaache. Lakini ukweli ndio huo, lakini kwa sasa tumeachana, kila mtu ana maisha yake," alisema Michael kwa masikitiko.
Michael ambaye kwa sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, pia alikiri kuwa mbunge huyo anashikilia vyeti vyote vya shule ambavyo anavihitaji sana kwa ajili ya kusaka ajira baada ya kumaliza masomo yake Muhimbili.
Alitaja sababu ya kuvunja ndoa hiyo kuwa ni manyanyaso kwa vile ni mdogo na masikini kwani hakuwa na sauti na alibanwa kwa kila kitu kiasi cha kukosa kabisa amani katika maisha yake.
"Kimsingi ndoa yangu na mama imevunjika na ilivunjikia mikononi mwa Rwakatare wakati akijaribu kutusuluhisha, alinitaka nirudi kwa mama, hapana, siko tayari na hapa nataka vyeti vyangu tu basi," alisema Michael.


Mbunge ang'aka



Kwa upande wake, mbunge huyo alipoulizwa, kwanza alikuwa mbogo na kukataa katakata kuzungumza kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo zito kwenye simu.
Mbunge huyo alikiri kuwapo kwa ndoa hiyo, lakini alipinga kwamba haijavunjika na kumhoji mwandishi wa habari hizi kama anajua taratibu za kuvunja ndoa.
"Michael kakuambia hiyo ndoa imevunjika? Wewe si unajua taratibu za ndoa kuvunjika? Kwanza nimeshasema sitaki kuzungumzia suala hili kwenye simu ukitaka tuonane kesho kwani kuna haraka gani? Jambo la haraka ni la mjamzito kutaka kujifungua, lakini kama ni suala hilo hakuna sababu ya uharaka," alisema mbunge huyo.
Hata hivyo baada ya kubanwa, mbunge huyo alimtaka mwandishi wa habari hizo kukutana naye katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ufafanuzi, lakini cha ajabu mwandishi alipofika katika ofisi hizo hizo, mama huyo alizima simu yake na hakupatikana tena.


Mchungaji Rwakatare



Alipotakiwa kuzungumzia ndoa hiyo, Mchungaji Rwakatare kwanza aling'aka kwamba hajawahi kufungisha ndoa ya aina hiyo.
Lakini alipobanwa alikiri kuikumbuka ndoa hiyo na kwamba ilifungishwa na mchungaji wa kanisa lake, aliyemtaja kwa jina la Mchungaji Mtetumo.
Alimtetea mchungaji wake kwamba alichokifanya ni kutimiza wajibu wake wa kichungaji wa kufungisha ndoa, hasa kama wanandoa wametimiza vigezo.
"Wajibu wa kanisa ni kufungisha ndoa, kama wanandoa wamekidhi vigezo vya kanisa. Sio kazi ya kanisa kuwachagulia wachumba kwa maana hakukuwa na sababu ya kuhoji umri wao, wala jambo lolote zaidi ya kufungisha ndoa hiyo," alisema Mchungaji Rwakatare[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

​
 
kwani kuna haraka gani? jambo la haraka ni mwanamke kutaka kujifungua alisema mbunge huyo
 
Mbunge kanjanja, Mchungaji aliyefungisha ndoa ni kanjanja pia, yeye mwenyewe Mchungaji hana ndoa...Maccm wote ni mapunguani....Punguani kamfungisha ndoa punguani..
 
basi olewa wewe mkuu sioni kinachokusumbua binafsi najua mapenzi hayana umri wala utajiri kama mtu kafikisha umri wa utu uzima habari ya uzee hayazungumzwi kisheria.

Huyu mama kwaabisha watoto wake ambao inasemekana wanaumri sawa na huyo kijana...Hao vijana wataficha wapi sura zao na aibu hii...Inasikitisha sana..
 
Masuala ya mahusiano ya kingono baina ya wawili ni yao wenyewe wawili. Sidhani kuwa hii ni issue kubwa ya kuumiza watu vichwa as long wote wawili ni watu wazima. Kijana wa miaka 26 tayari ni mtu mwenye akili timamu na mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yake binafsi.

Kabla hajaanzisha mahusiano na huyo mama hadi kufikia kufunga nae ndoa hata kama ni ya siri, alikuwa anafahamu kuwa ana umri mkubwa wa miaka 60 lakini bado aliridhika kuwa nae, kwahiyo hapo hakuna jambo la ajabu wala kitu cha kushangaza.
 
sasa kashfa iko wapi.....jamani mapenzi ni kitu cha watu wawili......mimi mbona nina miaka 23...na mpenzi wangu 35....sasa kasha nini hapo...kama wawili tumependana......gazeti la mtanzania daima sasa linaelekea kuwa la udakuuuu..


na mwandishi wa huyu wa habali hii akili yake imekaa kisiasa na ushabiki....wa kitoto ....hivi mtu mzima na akili zako utasema hii ni kashifaa
 
Siasa za TZ kazi sana, sasa gazeti la maana kama hili linageuka Shigongoz?
 
Kama kuna sheria ama kanuni iliyokiukwa?

Mkuu hapo hakuna sheria ya nchi iliyo kiukwa.Hapo msingi ni suala la kimaadili tu kwamba iwapo ni sawa katika Jamii yetu ya Tanzania kwa mjukuu kumvua nguo za Ndani Bibi yake.Kabisa kwa tofauti ya Umri wao hapo ni mtu na Bibi yake.Kimaadili ni tatizo na changamoto kwa jamii yetu ya Tanzania ila kisheria wako sawa ispokuwa tu iwapo
1. Itathibitika hakukuwa na mashahidi
2. Itathibitika Mfungishaji hakuwa mtu mwenye mamlaka ya kufanya hivyo
3. Wahusika ni maharimu(yaani ndugu wa damu)
4. Au kulikuwa na shinikizo katika kufunga ndoa hiyo
5.Mmoja wa wanandoa hakufikisha umri unaokubalika kisheria.

Vinginevyo ndoa hiyo ni halali kabisa na sharti itenguliwe na Mahakama na siyo kutimka mbio kila mtu na Lwake kama walivyo fanya hawa wandugu. .
 
Hii sio kashfa hata kidogo. Ingekuwa kashfa kama huyo mbunge ana uhusiano na mume wa mtu. Je ingekuwa mbunge mwanamume wa miaka 60 ameoa msichana wa miaka 26 ingekuwa issue? Mimi sioni tatizo hapo kama hakuna sheria iliyovunjwa labda kama jamaa angekuwa under 18. Sheria za TZ ni kuwa mtu akishafikisha miaka 18 ni mtu mzima. Tofauti ya miaka kwenye ndoa sio tatizo ila ni mazoea kuwa wanaume ndio huwa wanakuwa na umri mkubwa kuliko wanawake lakini sio sheria. Huyo mama angeweza kuolewa hata na kijana wa miaka 18 ili mradi wamependana na kukubaliana hata kama watoto wake huyo mama watakuwa na umri wa miaka 42 itabidi wamwite huyo kijana (mume wa mama yao) "baba" na wampe "shikamoo" yake!
 
Kwa nature tuu hata kwenye maandiko ya pande zote utaona kuna wanaume wazee wameoa vigoli na hata hali ya klawaida wababa huwakaza mabinti ila sio kawaida kwa wamama kukazwa na watoto!!!!mbo--o iko simple na mazingira yake hayachoki ila k ni mbaya na kadri umri unavokuwa nayo inazidi kuning'inia na kuchambuka na minyonyo hulegea na litumbo huwa libaya na ngozi nayo inachoka mno na makalio hata yawe makubwa vipi hujikusanya katikati na kuwa kama ---- moja(baya)sasa hapo ndipo panaposhangaza maana uzuri wa mwanamke usiempenda kiukweli ni yeye kuwa mzuri ili kukupa tamaa ya kumkwea!!!!!sasa mama kama huyu lazima alikuwa anamtesa sana kijana maana kulala nae ni zoezi gumu!!yaani mpaka mashine ipae ni noma unaweza ukawa unakula mambo gafla jamaa akalala!!!!! Sasa huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kulala pamoja kwa muda wote huo ni noma imagyn kulala daily na mwanamke kigoli mzuri yenyewe nis hida huwa unachoka na kukinahi itakuwa huyu bibi na obvious atakuwa anataka daily!!!hii nimeongea from my experience kutoka kwa marafiki wnasema inatisha kulala na mmama mzee na mbaya nawasilisha.....afu vijana siku hizi wanapenda 0713 huyu itakuwaje?
hivi na mengi kamuasili yule miss eee??
 
Mkuu hapo hakuna sheria ya nchi iliyo kiukwa.Hapo msingi ni suala la kimaadili tu kwamba iwapo ni sawa katika Jamii yetu ya Tanzania kwa mjukuu kumvua nguo za Ndani Bibi yake.Kabisa kwa tofauti ya Umri wao hapo ni mtu na Bibi yake.Kimaadili ni tatizo na changamoto kwa jamii yetu ya Tanzania ila kisheria wako sawa ispokuwa tu iwapo
1. Itathibitika hakukuwa na mashahidi
2. Itathibitika Mfungishaji hakuwa mtu mwenye mamlaka ya kufanya hivyo
3. Wahusika ni maharimu(yaani ndugu wa damu)
4. Au kulikuwa na shinikizo katika kufunga ndoa hiyo
5.Mmoja wa wanandoa hakufikisha umri unaokubalika kisheria.

Vinginevyo ndoa hiyo ni halali kabisa na sharti itenguliwe na Mahakama na siyo kutimka mbio kila mtu na Lwake kama walivyo fanya hawa wandugu. .

Well said!
 
Jamaa alikuwa hana plan za kupata mtoto nini mpaka akakubali kumuoa Bibi kama huo?
 
Back
Top Bottom