Mbunge bibi miaka 60, aolewa na kijana wa miaka 26

Mbunge bibi miaka 60, aolewa na kijana wa miaka 26

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,463
>>>>>>>>>>>>
BUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60), amejikuta kwenye kashfa nzito ya kufunga ndoa na kijana, kinda wa miaka 26, Michael Christian.

Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG), linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge wanaoifahamu pamoja na majirani wanaoishi na mbunge huyo.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya wanandoa hao na majirani wanaowazunguka, vililiambia gazeti hili kuwa ndoa hiyo ilifungwa Septemba Mosi mwaka 2011, na imebaki kuwa siri kabla ya wawili hao kukorogana.

Kabla ya wawili hao kuamua kufunga ndoa, mbunge huyo kutoka mkoani Rukwa, mwenye makazi yake Bagamoyo mkoani Pwani, alikuwa akimtumia Michael kwenye shughuli mbalimbali na muda wote alikuwa akiishi nyumbani kwa mbunge huyo.
Inaelezwa kuwa mbunge huyo ambaye ana familia ya watoto wawili ambao kiumri wanalingana na Michael, alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo kwa siri kubwa na baadaye alifanikiwa kumshawishi wafunge ndoa huku akimuahidi kumpa huduma mbalimbali anazotaka.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao waliamua kufunga ndoa katika Kanisa la TAG baada ya mbunge huyo kufanikiwa kumshawishi Mchungaji Rwakatare kwamba ndoa hiyo itakuwa siri, hasa kutokana na tofauti ya kiumri kati yao.
Hata hivyo ndoa hiyo kwa sasa imekumbwa na mgogoro mkubwa, huku mbunge huyo akidaiwa kuzuia kila kitu cha mumewe huyo, hasa vyeti vyake vya shule kama njia ya kumbana warudiane.


Siku ya harusi
Kwa mujibu wa mashuhuda wa harusi hiyo ya aina yake, mbunge na kijana huyo walikwenda kanisani wakiwa wawili bila mashahidi kama ilivyo kawaida, na ndoa hiyo ilifungwa katika ofisi ya kanisa na sio ndani ya kanisa.
Mashahidi wa ndoa hiyo waliitwa hapo hapo kanisani na walisimamia na kushuhudia utiaji saini wa cheti cha ndoa na kisha wanandoa hao kutawanyika kwenda kwenye fungate (Honey Moon). Hakukuwa na sherehe baada ya kufungwa ndoa.
Inadaiwa kuwa hakukuwa na ndugu yeyote wa maharusi hao aliyeshuhudia tukio hilo la kihistoria la wawili hao kuunganishwa na kuwa mwili mmoja.


Kauli ya Bwana harusi
Tanzania Daima Jumatano, lilifanikiwa kumpata Michael, ambaye katika mazungumzo yake alikiri kufunga ndoa na mbunge huyo Septemba Mosi mwaka 2011, lakini kwa sasa wametengana kutokana na sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.
“Mimi nadhani hili ni jambo binafsi, sio vizuri kulizungumza hadharani ila kweli nilifunga naye ndoa maana inaonekana mnajua mambo mengi kunihusu, na ni kweli kwa sasa tumeachana,” alisema kwa kifupi.
Alisema walikutana na mbunge huyo Bagamoyo wakati alipokuwa akifanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali ya wilaya hiyo kama muuguzi mkunga wakati mbunge huyo akiwa muuguzi mkuu wa wilaya katika hospitali hiyo.
Alipoulizwa sababu za kukubali kufunga ndoa na mama wa umri wa miaka 60 wakati ana miaka 26 na sababu za ndoa hiyo kuvunjika, Michael alisema ana historia ndefu katika maisha yake kwani alizaliwa yatima na amekua na kulelewa kwa ufadhili wa kituo cha Safina Street Network.

“Katika mazingira niliyokulia, unaweza kujua kwanini nilikubali kuingia kwenye ndoa hiyo. Sina ndugu hata wa kunishauri. Hata hivyo, hayo tuyaache. Lakini ukweli ndio huo, lakini kwa sasa tumeachana, kila mtu ana maisha yake,” alisema Michael kwa masikitiko.

Michael ambaye kwa sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, pia alikiri kuwa mbunge huyo anashikilia vyeti vyote vya shule ambavyo anavihitaji sana kwa ajili ya kusaka ajira baada ya kumaliza masomo yake Muhimbili.
Alitaja sababu ya kuvunja ndoa hiyo kuwa ni manyanyaso kwa vile ni mdogo na masikini kwani hakuwa na sauti na alibanwa kwa kila kitu kiasi cha kukosa kabisa amani katika maisha yake.
“Kimsingi ndoa yangu na mama imevunjika na ilivunjikia mikononi mwa Rwakatare wakati akijaribu kutusuluhisha, alinitaka nirudi kwa mama, hapana, siko tayari na hapa nataka vyeti vyangu tu basi,” alisema Michael.


Mbunge ang’aka
Kwa upande wake, mbunge huyo alipoulizwa, kwanza alikuwa mbogo na kukataa katakata kuzungumza kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo zito kwenye simu.
Mbunge huyo alikiri kuwapo kwa ndoa hiyo, lakini alipinga kwamba haijavunjika na kumhoji mwandishi wa habari hizi kama anajua taratibu za kuvunja ndoa.
“Michael kakuambia hiyo ndoa imevunjika? Wewe si unajua taratibu za ndoa kuvunjika? Kwanza nimeshasema sitaki kuzungumzia suala hili kwenye simu ukitaka tuonane kesho kwani kuna haraka gani? Jambo la haraka ni la mjamzito kutaka kujifungua, lakini kama ni suala hilo hakuna sababu ya uharaka,” alisema mbunge huyo.
Hata hivyo baada ya kubanwa, mbunge huyo alimtaka mwandishi wa habari hizo kukutana naye katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ufafanuzi, lakini cha ajabu mwandishi alipofika katika ofisi hizo hizo, mama huyo alizima simu yake na hakupatikana tena.


Mchungaji Rwakatare
Alipotakiwa kuzungumzia ndoa hiyo, Mchungaji Rwakatare kwanza aling’aka kwamba hajawahi kufungisha ndoa ya aina hiyo.
Lakini alipobanwa alikiri kuikumbuka ndoa hiyo na kwamba ilifungishwa na mchungaji wa kanisa lake, aliyemtaja kwa jina la Mchungaji Mtetumo.
Alimtetea mchungaji wake kwamba alichokifanya ni kutimiza wajibu wake wa kichungaji wa kufungisha ndoa, hasa kama wanandoa wametimiza vigezo.
“Wajibu wa kanisa ni kufungisha ndoa, kama wanandoa wamekidhi vigezo vya kanisa. Sio kazi ya kanisa kuwachagulia wachumba kwa maana hakukuwa na sababu ya kuhoji umri wao, wala jambo lolote zaidi ya kufungisha ndoa hiyo,” alisema Mchungaji Rwakatare.



 

Attachments

  • gggg.bmp
    gggg.bmp
    499.1 KB · Views: 3,274
  • untitled.JPG
    untitled.JPG
    37.1 KB · Views: 3,789
Hamjaobwa kadi mnalalamika fanyeni yenu wengine wanatamani wangekuwa wao alaaaaaaaa
 
vijana umasikiini utatumaliza kitu yake ishasinyaaa cjui kijana anafaidi nn
 
kijana kachukua ajira jamani shida iko wapi.... ndoa ni biashara mmoja anauza mwingine ananunua ktk kesi hii kijana ndio anauza jasho na mama ananunua!!

Unasema hivyo kwa kuwa siyo mtoto wako wala ndugu yako. Bila shaka angekuwa mwanao wa kwanza kumshtaki angakuwa huyo Rwakatare aliyefunga hiyo ndoa. Mchungaji gani asiyekuwa na hekima na busara hata kama ya mtoto wa chekechea? Huyu mchungaji ametia aibu mni. Shame on her.
 
Kama kuna sheria ama kanuni iliyokiukwa?

Makupa najua wewe mara ni mpuuzi wa hoja na hapa kwa kwa ni Mbunge wa CCM unamtetea lakini nami nakubaliana nawe kwamba ndoa yao ni maisha hakuna haja ya kuandika ujinga kama huu .Kijana miaka 26 aliamua mwenyewe na maisha yao haya mahusiano na status za kazi zao .Habari hii haisaidii lolote maana mitaani wadada wa miaka 20 anatembea na wazee na vijana wadogo taste zao ni akina Mama watu wazima .FREEDOM
 
CCM, wanachama wake, viongozi wake kuanzia ngazi ya shina mpaka taifa wanaongozwa na rushwa,

Huwezi ukapata tiketi ya kugombea udiwani, ubunge CCM bila kutoa rushwa na urais ndio inabidi ujenge mtandao zaidi ya miaka 10 ili ujiwekee nafasi nzuri

Niliposikia Mch. Lwakatare amekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, nilishangaa sana na nilihoji uadilifu wake, huwezi ukamtumikia MUNGU kwa nafasi ya Mchungaji ukawa mbunge tena kwa chama cha CCM

Nilijua kuna mengi yatakuwa yamejificha, busara ya kimungu ilihitajika, roho alipaswa aseme naye na kama kiongozi wa kanisa kama kweli anasema hakuifungisha yeye alipaswa aitengue

Kitu kingine Biblia inakataza kuwa na Mchungaji Mwanamke, na imeenda mbali biblia inasema mwanamke hapaswi kukaa mbele madhabahuni na kusema mbele ya wanaume

Wakatoliki wanaliheshimu neno hili, na ndio maana hakuna askofu wala padri mwanamke
 
kama ni hivyi ngija na mimi nikafunge ndoa na FAIZAFOX WANGU
 
Hapo hakuna ndoa sema kijana maisha magumu kaamua hapo ndio atachukua maisha kwahiyo tatizo liko wapi?

Kulingana na gazeti kijana na yatima hawajui wazazi na wala hana ndugu. Sasa hilo limama tena mbunge badala ya kumwasili anamvulia mtoto mdogo nguo. Mtu mzima hovyo. Halafu bila aibu anasimama bungeni na kuchangia hoja kumbe ni mnyanyasi wa watoto. Wanaharakati tafadhali angalieni hili jambo. Huyu kizee alichukua advantage ya umaskini wa kijana huyu kumhujumu. Haikubaliwi.
 
Safiiiii.....Madonna hamumuoni?ukichukua dogodogo wamama wanachukua wachanga......Love is Wicked...
 
Kulingana na gazeti kijana na yatima hawajui wazazi na wala hana ndugu. Sasa hilo limama tena mbunge badala ya kumwasili anamvulia mtoto mdogo nguo. Mtu mzima hovyo. Halafu bila aibu anasimama bungeni na kuchangia hoja kumbe ni mnyanyasi wa watoto. Wanaharakati tafadhali angalieni hili jambo. Huyu kizee alichukua advantage ya umaskini wa kijana huyu kumhujumu. Haikubaliwi.

Hivi na Mengi kamuasili yule miss eee??
 
Kwani tatizo liko wapi ?. Binafsi naona sawa tu maana tunaenda sambamba na mabadiliko ya kitabia na maadili, haipaswi kuanza kuchangaa ya wengine wakati una mambo mengi ya kufanya, pia acheni umbea eti ugumu wa maisha ndio umemfanya kijana aolewe na bibi kizee, suala la mapenzi ni gumu sana
 
Back
Top Bottom