Mbunge Bernadeta Mushashu aitaka Wizara ya Elimu ikubali mfumo una tatizo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge Bernadeta Mushashu ameitaka Wizara ya Elimu pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo kukubali kuna tatizo katika mfumo wa Elimu wa hapa Nchini. Amesema hayo leo Bungeni Dodoma.

Ameeleza, "Wafungue mjadala mpana tukae tujadili tuangalie Mfumo wetu ni wapi kuna tatizo, kitu gani kinakosekana na tuongeze nini. Hiyo ndio itaweza kutupeleka kwenye dira yetu ya Uchumi wa Viwanda"

Aidha, Mbunge huyo pia ametoa wito kwa Serikali kuweka mkakati wa kuajiri Walimu akisema Mkoa wa Kagera una upungufu wa Walimu 7,607 wa Shule za Msingi na 1,340 kwenye Shule za Sekondari.
 
Back
Top Bottom