Mbunge wa Viti Maalum Kundi la Vijana anayetokea Zanzibar Mhe. Latifa Juwakali Wakati Akichangia Hotuba ya Bajeti Wizara ya Elimu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE LATIFA JUWAKALI AKICHANGIA HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA ELIMU 2023-2024 BUNGENI JIJINI DODOMA

Mbunge wa Viti Maalum Kundi la Vijana anayetokea Zanzibar Mhe. Latifa Juwakali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maono makubwa na jinsi alivyojipambanua katika Elimu kwa vitendo.

Katika maeneo mbalimbali ya Majimbo Shule nyingi zimejengwa, miradi ya Elimu inatakelezwa na kuzidi kukuza Human Capital na Physical Capital

Mhe. Latifa Juwakali katika hotuba yake Wizara ya Elimu amejikita maeneo yafuatayo;

Katika maboresho ya Mitaala ya Elimu, Walimu wanatakiwa wapate ujuzi mpya unaoendana na mahitaji ya maboresho ya Mitaala.

Pia, kwa Mwalimu aliyepata shahada ya pili wengi wao hawapati Promotion. Ni vyema wanapirudi kusoma na kuongeza ujuzi wa Elimu waangaliwe na kutiwa moyo kwa hatua nyingine ya Elimu waliipata kwani ujuzi wao unaendelea kutumika katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumzia Elimu ya vyuo vya Kati, Juwakali amesema watu hawa nao waangaliwe katika kuwapa mikopo. Huku akisema ni vyema mishahara ya walimu pia iangaliwe n kuwaongezea ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-17 at 20.01.48.mp4
    58.1 MB
Back
Top Bottom