Mbunge Neema Mgaya Aitaka Serikali Kufanyia Ukarabati Shule Kongwe Hapa Ncnini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE NEEMA MGAYA AITAKA SERIKALI KUFANYIA UKARABATI SHULE KONGWE HAPA NCHINI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Mhe. Neema William Mgaya katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ametaka kujua mpango wa Serikali kukarabati Shule Kongwe katika Mkoa wa Njombe

"Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa bwalo la Shule ya Sekondari Ibwachanya Njombe" - Mhe. Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe

"Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa Bwalo katika Shule za Sekondari nchini. Hata hivyo, natoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wang'ing'ombe kuanza kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa bwalo Shule ya Sekondari Ibwachanya" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

"Lini Serikali itakarabati na kujenga upya majengo ya Shule chakavu Wilaya ya Njombe, Ludewa, Wang'ing'ombe na Makete ndani ya Mkoa wa Njombe? - Mhe. Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe

"Lini Serikali itatatua tatizo la upungufu wa Walimu wa Sayansi ndani ya Mkoa wa Njombe? - Mhe. Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe

"Serikali ilikwisha karabati Shule 89 hapa nchini ambapo Mkoani Njombe kuna Shule 2 ambazo zilipata fedha za ukarabati ambapo ni Kipavi Sekondari iliyokuwepo Makambako na Njombe Sekondari. Tunaendelea kuangalia namna ya kukarabati Shule Kongwe ikiwemo zilizopo Mkoani Njombe" - Mhe. Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI

"Serikali ipo katika ukamilishaji wa kuajiri Walimu wa Sayansi na Walimu kwa ujumla ambao ni 13,390 ambao wataanza kazi muda si mrefu. Mkoani Njombe pia watapata mgao wa Walimu ambao wanakuja" - Mhe. Deo Ndejembi, Naibu Waziri TAMISEMI.

6956-Mbunge akichangia.jpg
 
Back
Top Bottom