Mbunge Bahati Ndingo AWAKATIA BIMA Wazee 1,000

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
MBUNGE BAHATI AWAKATIA BIMA WAZEE 1000

Katika kuadhimisha siku ya wazee Duniani mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila amesema Serikali itaendelea kuthamini mchango wa wazee ikiwa ni pamoja na kutafuta utatuzi wa kero zinazowakabili ikiwemo katika sekta za afya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mwila amesema hayo wakati akizungumza na wazee, viongozi na wananchi mbalimbali wa Mbarali kwenye maadhimisho ya siku ya wazee Tanzania kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera ambapo kwa Wilaya ya Mbarali yamefanyika katika kijiji cha Azimio Mapula Kata ya Kongolo ambapo shughuli hiyo imehudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na sekta binafsi.

Mwila amesema wazee ni hazina na kundi muhimu katika jamii ndio maana Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuboresha mazingira yao tofauti na baadhi ya nchi duniani ambazo wazee hawathaminiwi na wamekuwa wakitengwa.

"Ndugu zangu wazee wetu na wananchi kwa ujumla kwenye taarifa yenu Baraza la wazee inaonyesha kero yenu moja wapo ni kuachiwa mzigo kwa kulea wajukuu sasa niwaambie mnavyokuwa mnatafuta watoto mnakuwa peke yenu kupata raha inakuwaje mnaleta watoto mnashindwa kuwalea na kuwapa mzigo wazee!", Amehoji Dc Denis Mwila.

Aidha mkuu huyo wa Wilaya amesema tangu awamu ya kwanza Serikali imekuwa ikilitupia macho kundi la wazee mpaka sasa ambapo amesema bado Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya na kuwaomba wazee na wananchi kujiunga na mpango wa bima iliyoboreshwa ili kuepuka gharama kubwa wanapougua.

Pia amempongeza Mbunge mteule wa jimbo la Mbarali Bahati Keneth Ndingo kwa kujitolea kuwalipia bima za afya wazee elfu moja katika jimbo lake.

"Kwakweli nimpongeze sana Mhe. Mbunge (Bahati Ndingo) mteule, ninakupongeza sana sana sana yaani haujaapishwa lakini unafanya haya (kuwalipia bima ya afya wazee 1000 wa Mbarali) na sina mashaka naye kwa ninavyomfahamu, asante sana kwa kuiunga mkono Serikali", Denis Mwila, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.

Akizungumza kwenye hadhara hiyo, Mbunge mteule wa Jimbo la Mbarali Bahati Keneth Ndingo amesema kwa kutambua umuhimu wa wazee katika ujenzi wa Taifa Ofisi yake itajitoa kuwakatia bima za afya wazee elfu moja jimboni humo.

"Wazee wangu wa Wilaya hii (Mbarali) katika kuungana nanyi kwenye siku ya wazee Duniani kwa sisi Mbarali nitahakikisha katika kata zote ishirini nitawakatia bima za afya wazee Hamsini kwa kila kata hivyo Mhe.mgeni rasmi mwezi wa 12, 2023 tutakukaribisha uje ugawe kadi kwa wazee elfu moja hapa Mbarali", Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge mteule wa Mbarali.

Hata hivyo ameahidi kwenda kuwawakilisha vema bungeni wananchi wake wakiwemo wazee ikiwa ni pamoja na kuhakikisha sera ya wazee inafanyiwa maboresha kwani iliyopo imepitwa na wakati.

Katibu wa Baraza la wazee Wilaya ya Mbarali akisoma risala ya wazee hao ameitaka Serikali kuboresha huduma za afya kwa kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na kuongeza ujenzi Zahanati wa Vituo vya afya na kuboresha mazingira ya wananchi wao hasa wazee ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa Taifa ambapo maadhimisho ga siku ya wazee Duniani hufanyika Oktoba Mosi ya kila mwaka ili kukumbuka, kutafakari na kuenzi n mchango wa kundi hilo kote ulimwenguni.
 

Attachments

  • F7bpJLZXQAAg8D2.jpg
    F7bpJLZXQAAg8D2.jpg
    61.3 KB · Views: 1
  • F7bpIhBXsAAw8XW.jpg
    F7bpIhBXsAAw8XW.jpg
    68 KB · Views: 2
  • F7bpJd8X0AEqYAW.jpg
    F7bpJd8X0AEqYAW.jpg
    84.6 KB · Views: 2
Wakuu mimi ndio kiranja mkuu huku kuzimu yote yaliyosemwa sio kweli. Narudia tena ni uwongo mtupu.

Kunyweni bia sana imbeni na fanyeni ibada kujifurahisha mwili. Huku hakuna mambo ya duniani kwa hiyo fanyeni mpaka mzeekee.

Huku ni kuzuri ila sio kama duniani. Kuna shida na karaha kuliko duniani. Sio sehemu ya kufikiria kuja ukiwa na nguvu. Ni bora ukae gerezani kuliko kuzimu huku haina vitu vya duniani.
 
Back
Top Bottom