Mwandishi Wetu , Mwanza
Chanzo: Gazeti la Mwanchi Jumapili
KITABU cha "Mafisadi wa Elimu" kimezidi kuwa lulu jijini Mwanza baada ya nakala zake 25,000 ambazo zilitarajiwa kusambazwa kwa mauzo, kununuliwa na mmoja wa wabunge na kuchomwa moto.
Habari zilizopatikana jijini Mwanza na kuthibitishwa na mmoja wa mawakala waliopewa jukumu la kusambaza ili kuuza vitabu hivyo, zilieleza kuwa mwanasiasa huyo kupitia kwa watu wake wa karibu aliomba kununua nakala zote hizo za vitabu kwa nyakati tofauti kwa madai ya kuvisambaza bure kwa watu.
Kitabu hicho ambacho kimeanza kusambazwa katika mikoa mbalimbali kwa mauzo kimekuwa kikitafutwa na wananchi kwa ajili ya kusoma ili kutambua kilichoandikwa hivyo kuwa gumzo kwa wananchi.
Imeelezwa kuwa mbunge huyo wa kanda ya ziwa kwa mara ya kwanza alipata taarifa za kuingia kitabu hicho na kutuma watu kukusanya nakala hizo katika meza za wauzaji na kwenda kuchoma moto.
"Baada ya nakala za kwanza ambazo zilikuwa kama 5,000 kununuliwa kwa siku moja na kuisha, wakala aliwasiliana na mwenye kitabu ambaye aliamua kutuma nakala nyingine kwa ajili ya kuuzwa, lakini pia aliambiwa zimeisha baada ya siku mbili" alieleza mmoja wa wauza magazeti wa mkoani Mwanza.
Kutokana na kukosekana kwa kitabu hicho baadhi ya wafanyabiashara kwa kutumia moja ya nakala ambazo wamebahatika kuwa nazo wameanza kudurufu kitabu hicho kwa kutoa nakala ambazo wanaziuza mitaani kwa bei ya Sh3,000.
"Mimi binafsi kila ninapokwenda kuuza magazeti watu wamekuwa wakiniulizia kitabu hicho na wengine wameniomba kikifika tu niwapelekee wakanunue, sasa nilipowaambia bado hakipatikani ila kuna nakala walisema niwapelekee na waliweza kununua kwa bei ile ya kitabu" alieleza muuza magazeti huyo.
Katika kitabu hicho wabunge ambao walidaiwa kuwa na shahada feki ni Anthony Diallo, Deodarus Kamala pamoja na Raphael Chegeni ambao walitajwa kuwa na shahada ya uzamili (masters) na uzamivu (PhD) feki.
MY Comments: .
Kama hawahusiki na vyeti feki , vijitabu wanachoma moto vya nini? Nadhani kuna kila sababu ya wananchi kuhoji na kuomba TCU iwaite watu hao kwa lazima wapeleke vyeti vyao.