Mbunge adaiwa kununua vitabu vya msemakweli na kuchoma moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge adaiwa kununua vitabu vya msemakweli na kuchoma moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Mar 6, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,115
  Likes Received: 6,453
  Trophy Points: 280
  Mbunge adaiwa kununua vitabu kuchoma moto

  Mwandishi Wetu , Mwanza


  KITABU cha ‘Mafisadi wa Elimu’ kimezidi kuwa lulu jijini Mwanza baada ya

  nakala zake 25,000 ambazo zilitarajiwa kusambazwa kwa mauzo,

  kununuliwa na mmoja wa wabunge na kuchomwa moto.


  Habari zilizopatikana jijini Mwanza na kuthibitishwa na mmoja wa

  mawakala waliopewa jukumu la kusambaza ili kuuza vitabu hivyo,

  zilieleza kuwa mwanasiasa huyo kupitia kwa watu wake wa karibu aliomba

  kununua nakala zote hizo za vitabu kwa nyakati tofauti kwa madai ya

  kuvisambaza bure kwa watu.


  Kitabu hicho ambacho kimeanza kusambazwa katika mikoa mbalimbali kwa

  mauzo kimekuwa kikitafutwa na wananchi kwa ajili ya kusoma ili

  kutambua kilichoandikwa hivyo kuwa gumzo kwa wananchi.


  Imeelezwa kuwa mbunge huyo wa kanda ya ziwa kwa mara ya kwanza

  alipata taarifa za kuingia kitabu hicho na kutuma watu kukusanya

  nakala hizo katika meza za wauzaji na kwenda kuchoma moto.

  “Baada ya nakala za kwanza ambazo zilikuwa kama 5,000 kununuliwa

  kwa siku moja na kuisha, wakala aliwasiliana na mwenye kitabu ambaye

  aliamua kutuma nakala nyingine kwa ajili ya kuuzwa, lakini pia

  aliambiwa zimeisha baada ya siku mbili” alieleza mmoja wa wauza

  magazeti wa mkoani Mwanza.


  Kutokana na kukosekana kwa kitabu hicho baadhi ya wafanyabiashara kwa

  kutumia moja ya nakala ambazo wamebahatika kuwa nazo wameanza kudurufu

  kitabu hicho kwa kutoa nakala ambazo wanaziuza mitaani

  kwa bei ya Sh3000.

  “Mimi binafsi kila ninapokwenda kuuza magazeti watu wamekuwa

  wakiniulizia kitabu hicho na wengine wameniomba kikifika tu

  niwapelekee wakanunue, sasa nilipowaambia bado hakipatikani ila kuna

  nakala walisema niwapelekee na waliweza kununua kwa bei

  ile ya kitabu” alieleza muuza magazeti huyo.


  Katika kitabu hicho wabunge ambao walidaiwa kuwa na shahada feki ni

  Anthony Diallo, Deodarus Kamala pamoja na Raphael Chegeni ambao

  walitajwa kuwa na shahada ya uzamili(masters) na uzamivu(PhD) feki
   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 8,134
  Likes Received: 1,706
  Trophy Points: 280
  Sasa ni dhahiri hao waheshimiwa wana digrii feki,kwanini wanaogopa hicho kitabu kisomwe na watu kama kweli mtu ana digrii ya kweli,pia baado sijaridhika na digrii ya David Mathayo na inabidi sijui(bahati mbaya Takukuru nao hawaaminiki) wangelichunguza hilo swala,Prof Nkunya katuongopea anakuwa naye kama sio musomi kuhusu suala la kumsafisha David hata mimi ngumbaru nimeona kuna walakini mkubwa au ndio ufisadi wa elimu umemuingia huyo Professor,pia naona siasa zimeingilia kati sidhani kama hao wabunge wangekuwa wa upinzani serikali ingekaa kimya,aibu kwenu wabunge vihiyo nyie ndio mko tayari kuwaibia mitihani watoto wenu!aibu kwenu
   
 3. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Hii sredi inahusiana vp na MMU? Mods plz do ze nidful! Imekaa kipolitikali zaidi
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,115
  Likes Received: 6,453
  Trophy Points: 280
  we unajua MMU kitandani tu
  kutana na MMU KWENYE MAKARATASI
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Mar 6, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,206
  Likes Received: 375
  Trophy Points: 180
  Nasikia kuwa hata Dkt Mwakyembe alifeli Form IV akatumia cheti cha ndugu yake kuendelea na masomo ya A Level!
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Nasikia hata jina lake halisi ni Harry na hata PhD yake alipewa kwa upendeleo!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,115
  Likes Received: 6,453
  Trophy Points: 280
  vithibitisho muhimu
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Capt hapo itakuwa kazi kidogo! wewe meza tu
   
 9. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,370
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Miaka ile ilikuwa vigumu sana kwenda secondary bila kurudia mitihani mara saba au nane hivi, Bonde la mto Lufilyo karibu wasomi wowte walirudia madarasa na shule baada ya kuhitimu kujaribu bahati zao tena.
   
 10. M

  Msharika JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwandishi Wetu , Mwanza
  Chanzo: Gazeti la Mwanchi Jumapili

  KITABU cha "Mafisadi wa Elimu" kimezidi kuwa lulu jijini Mwanza baada ya nakala zake 25,000 ambazo zilitarajiwa kusambazwa kwa mauzo, kununuliwa na mmoja wa wabunge na kuchomwa moto.

  Habari zilizopatikana jijini Mwanza na kuthibitishwa na mmoja wa
  mawakala waliopewa jukumu la kusambaza ili kuuza vitabu hivyo, zilieleza kuwa mwanasiasa huyo kupitia kwa watu wake wa karibu aliomba kununua nakala zote hizo za vitabu kwa nyakati tofauti kwa madai ya kuvisambaza bure kwa watu.

  Kitabu hicho ambacho kimeanza kusambazwa katika mikoa mbalimbali kwa
  mauzo kimekuwa kikitafutwa na wananchi kwa ajili ya kusoma ili kutambua kilichoandikwa hivyo kuwa gumzo kwa wananchi.

  Imeelezwa kuwa mbunge huyo wa kanda ya ziwa kwa mara ya kwanza
  alipata taarifa za kuingia kitabu hicho na kutuma watu kukusanya nakala hizo katika meza za wauzaji na kwenda kuchoma moto.

  "Baada ya nakala za kwanza ambazo zilikuwa kama 5,000 kununuliwa kwa siku moja na kuisha, wakala aliwasiliana na mwenye kitabu ambaye aliamua kutuma nakala nyingine kwa ajili ya kuuzwa, lakini pia aliambiwa zimeisha baada ya siku mbili" alieleza mmoja wa wauza magazeti wa mkoani Mwanza.

  Kutokana na kukosekana kwa kitabu hicho baadhi ya wafanyabiashara kwa
  kutumia moja ya nakala ambazo wamebahatika kuwa nazo wameanza kudurufu kitabu hicho kwa kutoa nakala ambazo wanaziuza mitaani kwa bei ya Sh3,000.

  "Mimi binafsi kila ninapokwenda kuuza magazeti watu wamekuwa wakiniulizia kitabu hicho na wengine wameniomba kikifika tu niwapelekee wakanunue, sasa nilipowaambia bado hakipatikani ila kuna nakala walisema niwapelekee na waliweza kununua kwa bei ile ya kitabu" alieleza muuza magazeti huyo.

  Katika kitabu hicho wabunge ambao walidaiwa kuwa na shahada feki ni
  Anthony Diallo, Deodarus Kamala pamoja na Raphael Chegeni ambao walitajwa kuwa na shahada ya uzamili (masters) na uzamivu (PhD) feki.

  MY Comments: .
  Kama hawahusiki na vyeti feki , vijitabu wanachoma moto vya nini? Nadhani kuna kila sababu ya wananchi kuhoji na kuomba TCU iwaite watu hao kwa lazima wapeleke vyeti vyao.
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu mbunge atanunua hizo kopi mpaka lini?Na huyo mchapaji wa hicho kitabu si ataendelea kutajirika?Huyo mbunge kweli ana upungufu wa elimu
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu Ben,

  Kweli aliyesema ukiona Elimu ghali, jaribu Ujinga..kweli hakukosea.
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama kweli Dialo kanunua na kuchoma moto vitabu ni upungufu wa maarifa ni sawa na mwanafuzi kushindwa somo la hesabu na kuamua kuchoma moto kitabu cha hesabu kitu ambacho hakitasaidia kitu
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  kaa ni kweli huu ni upimbi wa hali ya juu..lolz
   
 15. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona habari aina chanzo?
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  Umeanza kuisoma habari paragraph gani . Kwenye mitihani ya shule primary na sekondary tuliambiwa kabla ya kujibu mawasli soma maelekezo unaweza kukuta maelekezo ni usijibu swali. kama hujaona source rudia kusoma kwa makini.

  Hawa jamaa wamezoea kununua magazeti sasa wamenza na kwenye vitabu.
   
 17. M

  Msharika JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  chanzo ni Mwanannchi Jumapili
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Mar 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,868
  Likes Received: 4,268
  Trophy Points: 280
  Tunawahukumu wenyewe! TCU ni hao hao. kama cheti chako ni cha halali why bother?

  na mkoa wa mwanza ina wengi kwenye hako kajitabu, so kuna uwezekano hata hizo hela walichanga! huwezi ukapambana na wananchi, hivi sasa wameongeza kasi ya kitabu kununuliwa.

  Hatuna viongozi tuna wahuni wahuni tu, huyo mbunge alichofanya si ujinga wala umbumbumbu, ni uhuni!
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 24,228
  Likes Received: 23,379
  Trophy Points: 280
  Biashara nzuri sana hii,ngoja niwasiliane na wachapishaji ili ninunue kwao vitabu kisha nawauzia "mafisadi wa Elimu" wanavichoma kisha naagiza vingine hivyo hivyo mpaka na mie nitoke. Hii itakuwa biashara halali maana lazima kodi ntalipa.
   
 20. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,677
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
   
Loading...