Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,906
- 22,050
Mbunge adaiwa kununua vitabu kuchoma moto
Mwandishi Wetu , Mwanza
KITABU cha âMafisadi wa Elimuâ kimezidi kuwa lulu jijini Mwanza baada ya
nakala zake 25,000 ambazo zilitarajiwa kusambazwa kwa mauzo,
kununuliwa na mmoja wa wabunge na kuchomwa moto.
Habari zilizopatikana jijini Mwanza na kuthibitishwa na mmoja wa
mawakala waliopewa jukumu la kusambaza ili kuuza vitabu hivyo,
zilieleza kuwa mwanasiasa huyo kupitia kwa watu wake wa karibu aliomba
kununua nakala zote hizo za vitabu kwa nyakati tofauti kwa madai ya
kuvisambaza bure kwa watu.
Kitabu hicho ambacho kimeanza kusambazwa katika mikoa mbalimbali kwa
mauzo kimekuwa kikitafutwa na wananchi kwa ajili ya kusoma ili
kutambua kilichoandikwa hivyo kuwa gumzo kwa wananchi.
Imeelezwa kuwa mbunge huyo wa kanda ya ziwa kwa mara ya kwanza
alipata taarifa za kuingia kitabu hicho na kutuma watu kukusanya
nakala hizo katika meza za wauzaji na kwenda kuchoma moto.
âBaada ya nakala za kwanza ambazo zilikuwa kama 5,000 kununuliwa
kwa siku moja na kuisha, wakala aliwasiliana na mwenye kitabu ambaye
aliamua kutuma nakala nyingine kwa ajili ya kuuzwa, lakini pia
aliambiwa zimeisha baada ya siku mbiliâ alieleza mmoja wa wauza
magazeti wa mkoani Mwanza.
Kutokana na kukosekana kwa kitabu hicho baadhi ya wafanyabiashara kwa
kutumia moja ya nakala ambazo wamebahatika kuwa nazo wameanza kudurufu
kitabu hicho kwa kutoa nakala ambazo wanaziuza mitaani
kwa bei ya Sh3000.
âMimi binafsi kila ninapokwenda kuuza magazeti watu wamekuwa
wakiniulizia kitabu hicho na wengine wameniomba kikifika tu
niwapelekee wakanunue, sasa nilipowaambia bado hakipatikani ila kuna
nakala walisema niwapelekee na waliweza kununua kwa bei
ile ya kitabuâ alieleza muuza magazeti huyo.
Katika kitabu hicho wabunge ambao walidaiwa kuwa na shahada feki ni
Anthony Diallo, Deodarus Kamala pamoja na Raphael Chegeni ambao
walitajwa kuwa na shahada ya uzamili(masters) na uzamivu(PhD) feki