Mbu wa Muhimbili wamesababishwa na wao

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Nikwamba mbu waliozagaa Muhimbili walisababishwa na wao kitengo cha utafiti maana walizalishwa wengi bondeni Msimbazi na baada yakuzidi katika lubhall wakawafungulia na inasemekana wanaweza kuwa "Mbu hatari kwani niwakutengenezwa"!! Nawahusika wameidanganya serikali na jamii ionekane wametokea mto Msimbazi lakini siyo kweli!!!

Be were of that mosquitos!!: A S-danger:
 
Hivi kweli eh!? maana mimi mwenyewe nilshangaa waibuke ghafla tuu wengi kiasi hicho!
 
Dah, watakuwa wamefanya kosa kubwa sana, maana hao mbu ni wengi kuliko maelezo, na cha ajabu ni kwamba uongozi uliamua kupuliza dawa ili kuwadhibiti, lakini cha ajabu zaidi ni kwamba wamekuwa kama wamewachochea wazaliane zaidi, maana ukija ule muda wa saa 11 alfajiri mpaka around saa 1 wanakuwa wengi kiasi kwamba hata kupita njiani inakuwa tabu maana wanaingia mdomoni, puani na hata masikioni! Yaani sijui uongozi wa Muhimbili unalichukuliaje suala hili!
 
Jamani hao mbu wa Muhimbili nilifikiri masihara kwanza! akka kumbe kuna mbu wengi kiasi hicho hospitali? ndio wagonjwa watapona hivyo?
 
Hizo ndio reseach zetu zisizozingatia taaluma!! kwanza Muhimbili yenyewe imeficha!! wewe fikiria mbu ghafula ujiulizi sasa habari ndio hiyo!!
 
Kuna mfereji mkubwa unaotoa maji taka kutoka ndani ya kiwanda cha Tanzania Breweries. Mfereji huu unapita nyuma ya uwanja wa michezo wa Yanga kisha unavuka barabara ya morogoro na kupita karibu na shule ya wasichana ya Jangwani, Azania sekondari na nyuma ya hospitali ya Muhimbili.

TBL inaelekea hawausafishi huu mtaro tena, kama zamani, umejaa mchanga, chupa za plastic na kila aina ya uchafu, ambao umezuia maji yatuame eneo lote kuanzia shule ya jangwani hadi nyuma ya hospital, siku za nyuma eneo la bondeni ya hospital kulikuwepo na kiwanja cha mpira lakini sasa hivi pamegeuka bwawa kubwa la maji, ambalo ndilo sasa limegeuka shamba la kuzalishia mbu wanaotishia uhai wa wagonjwa na wanafunzi wa Jangwani, Azania, Chuo kikuu cha tiba, watumishi wa hospital na wakazi wa maeneo hayo.

Lawama zote ni lazima wabebe TBL kwa uzembe wa kutiririsha maji taka bila udhibiti wa kutosha. Ombi langu kwa serikali, iwalazimishe wajenge bomba la kupitisha maji taka toka ndani ya kiwanda chao hadi baharini, badala ya kupitisha maji taka kwenye mtaro wa wazi. TBL watoe gharama zote za kupuliza dawa za kuangamiza mbu eneo liloadhiriwa na mfereji wao. Kisha wagharamie uchunguzi wa vipimo vya afya kwa wanafunzi wa Jangwani, Azania na Muhimbili.
 
Nikwamba mbu waliozagaa Muhimbili walisababishwa na wao kitengo cha utafiti maana walizalishwa wengi bondeni msimbazi na baada yakuzidi katika lubhall wakawafungulia na inasemekana wanaweza kuwa "Mbu hatari kwani niwakutengenezwa"!!Nawahusika wameidanganya serikali na jamii ionekane wametokea mto msimbazi lakini siyo kweli!!!
Be were of that mosquitos!!:A S-danger:

mkuu unashangaa hiyo. nenda Ifakara ukaone mbu waliopo pale. Nasikia wote ni kazi ya Ifakara Health Research, eti wanawafuga na kuwaachia wakafanye kazi, kisha wanaanza kurekodi idadi ya wagonjwa wa malaria wanaofika St Francis Hospital. Kwa mgeni ukikaa wiki Ifakara, utakuwa na bahati kubwa sana ikiwa hutatoka na malaria.
 
Mkuu asante,

Its not strong reason!Huo mtaro unaosema unasikunyingi ..... mimi naona unaongelea jambo kwakusikia katika midomo yawatu au vyombo vya habari! Mbu wa muhimbili wana takribani two month hivi nakinachosemwa siyo kitu cha kufikirika!! Ni ukweli maana hata uongozi ujalitolea tamko kwanini mbu wako hapo kama unataka kuamini nenda hapo usiku-alfajiri au lala hapo utaniambia ...... Hivi hao mbu ni hapo tu muhimbili tu? Mbona wakazi waupanga kalenga unapopita hakuna?? ........... fikiria chukua atua!!!:nono:
 
mkuu unashangaa hiyo. nenda Ifakara ukaone mbu waliopo pale. Nasikia wote ni kazi ya Ifakara Health Research, eti wanawafuga na kuwaachia wakafanye kazi, kisha wanaanza kurekodi idadi ya wagonjwa wa malaria wanaofika St Francis Hospital. Kwa mgeni ukikaa wiki Ifakara, utakuwa na bahati kubwa sana ikiwa hutatoka na malaria.
Kama ni hivi basi hizi research hadi zifanikiwe watu wengi watakuwa wametekea!
 
yani Tanzania bana..kila kukicha vitu vya ajabuajabu, sasa sehemu ya wagonjwa tena hospitali ya rufaa, mi mbu nayo ndio hiyo! na hizo research si wangeenda kufanyia machokoroni huko, wanaiga ulaya wenzao wako full in facilities...mara wengine wafanyiwe operation kichwani badala ya miguuni, mara wanawake wanajifungua kwenye korido yani balaa tu kila kukicha! jamani we need strategies zenye positive output katika inchi hii tuache masihara!
 
Mkuu, hapo kwenye red ndiyo tatizo, nani ktk watawala na wanasiasa wetu anaelewa maana ya hilo neno?
 
Mkuu asante,Its not strong reason!Huo mtaro unaosema unasikunyingi.....mimi naona unaongelea jambo kwakusikia katika midomo yawatu au vyombo vya habari!!Mbu wa muhimbili wana takribani two month hivi nakinachosemwa siy kitu cha kufikirika!!Niukweli maana hata uongozi ujalitolea tamko kwanini mbu wako hapo kama unataka kuamini nenda hapo usiku-alfajiri au lala hapo utaniambia......Hivi hao mbu ni hapo tu muhimbili tu??Mbona wakazi waupanga kalenga unapopita hakuna??...........fikiria chukua atua!!!:nono:

Mbu huzaliana kwenye maji yaliyosimama, tatizo lililopo Muhimbili sasa hivi ni maji taka yanayotoka ndani ya kiwanda cha bia cha TBL. Suluhisho lake ni mfereji usafishwe maji yatembee kwa kasi kuelekea baharini. Reserch za mbu zinazofanyika jangwani walipojenga vibanda vingi vidogo vidogo kamwe hawazalishi mbu.
 
wanakuwa wengi kiasi kwamba hata kupita njiani inakuwa tabu maana wanaingia mdomoni, puani na hata massikioni

ha ha ha ha! nimecheka peke yangu kama zuzu. Aisee, hao mbu ni shughuli. Wanaingia mpaka mdomoni, ha ha ha!
 
Wakuu... Mwenzenu sina habari kamili.... NIni kinaendelea huko Muhimbili na hao mbu??
 
Nikwamba mbu waliozagaa Muhimbili walisababishwa na wao kitengo cha utafiti maana walizalishwa wengi bondeni msimbazi na baada yakuzidi katika lubhall wakawafungulia na inasemekana wanaweza kuwa "Mbu hatari kwani niwakutengenezwa"!!Nawahusika wameidanganya serikali na jamii ionekane wametokea mto msimbazi lakini siyo kweli!!!
Be were of that mosquitos!!:A S-danger:

Wewe hujui unachokiongea,na wala usiwadanganye wananchi pole sana, utapona tu.
 
Malaria haikubaliki ............................... Hao mbu wamewekewa some chemicals ( geneticaly engeneering) ambapo wameachiwa ili wajamiiane na hawa mbu wa kawaida, na watoto watakaozalishwa watakuwa hawana uwezo tena wa kusambaza malaria, ni stail kama ile ya mbug'o (tse tse fly). Wao wenyewe wanakunywa damu lakini hawaenezi vimelea vya malaria kwa hiyo msihofu.......
 
What if something goes wrong (medical failure) na hawa mbu wakawa na uwezo wa kusambazo vijidudu vya ukimwi? tests zingine zinatisha sana.
 
Back
Top Bottom