Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,111
- 34,940
Mbu wavamia tena Muhimbili
Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo mbalimbali wanakabiliwa
Dar es Salaam. Wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo mbalimbali wanakabiliwa na maradhi mengine
mapya kutokana na wodi kuvamiwa na mbu.
Tatizo linalofanana na hilo liliibuka katika hospitali hiyo Julai na Agosti, 2010 na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), ilibaini
kuwa chanzo chake kilikuwa ni chemba za vyoo kuwa wazi huku katika Bonde la Msimbazi kukiwa na matairi ya magari yaliyotupwa kwenye
mfereji wa maji machafu unaopeleka maji yake baharini.
Mmoja wa wagonjwa aliyelazwa katika Wodi ya Sewahaji chumba namba 17, Kulwa Maganga alisema jana kuwa alilazwa hapo tangu Septemba
10 baada ya kuvunjika mguu lakini amekuwa akiugua malaria mara kwa mara.
Alisema pamoja na kupata tiba na kinga ya maradhi hayo, haoni maana ya kuwa na chandarua kutokana na mbu hao kuwa wengi hivyo
kushindwa kuwadhibiti kwa kuwa analala chini hivyo kushindwa kukaa vyema kwenye godoro.
?Madirisha yapo wazi, nyavu zimetoka, mbu wanaingia na wananishambulia mchana, jioni na usiku, ukija asubuhi sana wanaranda kama maua.
Nimekuwa chakula chao, nimeumwa malaria mara tatu, hii ya mwisho niliumwa kwa wiki mbili,? alisema Maganga.
Zuhura Mrisho alisema amelazwa hospitalini hapo kwa miezi mitatu lakini hana raha kutokana na kushambuliwa na mbu kiasi cha kutoka vipele
na kuwashwa.
Alisema ameumwa malaria mara tatu akiamini hali hiyo inatokana na mbu waliojaa wodini.
?Hata kama ningekuwa na chandarua ni usiku tu, mchana siwezi kuweka chandarua kwa hiyo naumwa na mbu, ni wengi sana,? alisema.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema tatizo la mbu lipo nje ya uwezo wao kwani wamefanya kila jitihada kupambana nao bila mafanikio.
?Wiki iliyopita tumepuliza dawa lakini siku inayofuata asubuhi ukirudi unawakuta wanarukaruka, hiyo ni changamoto kubwa kwetu,? alisema.
Alisema mbu hao wanazaliana katika Bonde la Mto Msimbazi ulio nyuma ya hospitali hivyo kila wanapopuliza dawa hurudi kwa wingi.
Wiki iliyopita wagonjwa walitibiwa nje, katika eneo la wazi baada ya uongozi kuamua kupuliza dawa ya kuua wadudu katika wodi za Mwaisela na
Kibasila.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi alisema wanalifahamu tatizo la mbu kuzaliana kwa wingi Bonde la Msimbazi, jambo ambalo alisema
chanzo chake ni kujazana kwa matope katika mto huo.?Tunapeleka greda kwa ajili ya kuchimba matope hayo ili kuhakikisha maji yanatiririka
kupunguza tatizo la mbu eneo hilo.
chanzo.Mbu wavamia tena Muhimbili