Mbu wa Muhimbili wamesababishwa na wao

Malaria haikubaliki ............................... Hao mbu wamewekewa some chemicals ( geneticaly engeneering) ambapo wameachiwa ili wajamiiane na hawa mbu wa kawaida, na watoto watakaozalishwa watakuwa hawana uwezo tena wa kusambaza malaria, ni stail kama ile ya mbug'o (tse tse fly). Wao wenyewe wanakunywa damu lakini hawaenezi vimelea vya malaria kwa hiyo msihofu.......

hiki ni kichekesho Mganga wa jadi.
BTW Do you mean what tou are saying? or its just a joke.
Kama ni kweli. then we are done!!
unasemaje?
 
What if something goes wrong (medical failure) na hawa mbu wakawa na uwezo wa kusambazo vijidudu vya ukimwi? tests zingine zinatisha sana.

Hilo kubwa mtu wangu... Mi naona mambo ya GMO tuwaachie wathungu waliojidatia. Hivi hadi sasa nani ana hakika kama HIV haikuwa product ya genetic engineering?
 
inasemekana hao mbu kazi yao ni KUWALA MBU WANAOENEZA MALARIA - walitengenezwa kwa ajali hiyo. HATA HIVYO KWA TAARIFA ZAIDI UNAWEZA KUTEMBELEA MUHIMBILI UKAULIZIA.
 
What if something goes wrong (medical failure) na hawa mbu wakawa na uwezo wa kusambazo vijidudu vya ukimwi? tests zingine zinatisha sana.

Uwezekano wa hawa mbu kueneza magonjwa haupo, hata hiyo malaria hawana uwezo wa kueneza, Wanachoweza kufanya ni ku itransmit hiyo gene ya kushindwa ku transmit magonjwa kwa offspring wengine (uzao wake) na do maana wameachiwa ili wazaliane na kuchanganyika na hawa mbu wa kawaida ili wawamalizie uwezo wao wa kusambaza magonjwa ikiwemo hili sugu la malaria.
 
Kuna mfereji mkubwa unaotoa maji taka kutoka ndani ya kiwanda cha Tanzania Breweries. Mfereji huu unapita nyuma ya uwanja wa michezo wa Yanga kisha unavuka barabara ya morogoro na kupita karibu na shule ya wasichana ya Jangwani, Azania sekondari na nyuma ya hospitali ya Muhimbili.

TBL inaelekea hawausafishi huu mtaro tena, kama zamani, umejaa mchanga, chupa za plastic na kila aina ya uchafu, ambao umezuia maji yatuame eneo lote kuanzia shule ya jangwani hadi nyuma ya hospital, siku za nyuma eneo la bondeni ya hospital kulikuwepo na kiwanja cha mpira lakini sasa hivi pamegeuka bwawa kubwa la maji, ambalo ndilo sasa limegeuka shamba la kuzalishia mbu wanaotishia uhai wa wagonjwa na wanafunzi wa Jangwani, Azania, Chuo kikuu cha tiba, watumishi wa hospital na wakazi wa maeneo hayo.

Lawama zote ni lazima wabebe TBL kwa uzembe wa kutiririsha maji taka bila udhibiti wa kutosha. Ombi langu kwa serikali, iwalazimishe wajenge bomba la kupitisha maji taka toka ndani ya kiwanda chao hadi baharini, badala ya kupitisha maji taka kwenye mtaro wa wazi. TBL watoe gharama zote za kupuliza dawa za kuangamiza mbu eneo liloadhiriwa na mfereji wao. Kisha wagharamie uchunguzi wa vipimo vya afya kwa wanafunzi wa Jangwani, Azania na Muhimbili.

Hatimaye leo mganga mkuu wa afya na wafanyakazi wa wilaya ya Ilala wameanza kuondoa mchanga na kuzibua mtaro huo wa maji machafu na kunyunyuzia dawa za kuuwa viluwiluwi vya mbu.

Nadhani Tanzania Breweries ndiyo chanzo cha tatizo la mbu wa muhimbili, kwa sababu huo mtaro wa maji machafu unamilikiwa na kiwanda cha bia. Tunasubiri adhabu kali kwa TBL kwa uchafuzi wa mazingara na kumwaga maji ovyo.
 
Nikwamba mbu waliozagaa Muhimbili walisababishwa na wao kitengo cha utafiti maana walizalishwa wengi bondeni msimbazi na baada yakuzidi katika lubhall wakawafungulia na inasemekana wanaweza kuwa "Mbu hatari kwani niwakutengenezwa"!!Nawahusika wameidanganya serikali na jamii ionekane wametokea mto msimbazi lakini siyo kweli!!!
Be were of that mosquitos!!:A S-danger:

Hapana, this can't be! Siwezi ku-imagine kabisa!
Inawezekana kweli kuna watu wamefanya hiki kitendo? Km ndivyo basi inabidi watafutwe akili yao ifanyiwe utafiti, nasuspect itakuwa juu sana kiasi baadaye inaweza ikatusaidia hata kupata resources pamoja na technology ya kutengeneza chomb\ao ambaco kinaweza kufika hata kwenye andromeda in a day's time. Watakuwa huwa wanafikiria sana (sisemi huwa wanafikiria vizuri, maana si lazima kila kufikiria sana ni kuzuri)
 
Ndege ya Kenya kuua mbu Muhimbili Wednesday, 18 August 2010 08:20 Mwanchi

Hussein Kauli

BAADA ya Hospitali Taifa Muhimbili (MNH)kuvamiwa na mbu waliozaliana kwa wingi katika bonde la Msimbazi jijini Dar es Salaam, serikali imekodi ndege kutoka Kenya kwa ajili ya kunyunyiza dawa ya kuangamiza mazalia yao.
kazi hiyo itafanyika wakati ambapo tayari serikali imetumia Sh 26 milioni kwa ajili ya kuangamiza mbu hao bila mafanikio.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Rozina Lyipyoga wakati akizungumzia mikakati inayofanywa na hospitali hiyo kutokomeza mbu hao jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya wataalamu kutumwa kwenye eneo hilo kwa lengo la kuchukua sampuli ya mbu wanaozaliwa kwenye mto huo.
Lyipyoga alisema wamefikia hatua ya kuagizia ndege hiyo kutoka nchini Kenya, kutokana na bonde hilo la Msimbazi kutoweza kufikika kwa urahisi wakati wa kunyunyiza dawa ya kuua mbu.
Alisema pamoja na kuripotiwa kuwa hospitali ya Muhimbili kuvamiwa na mbu hao mwezi mmoja uliopita, hakuna ongezeko la ugonjwa wa malaria hospitalini hapo kwa wagonjwa na wafanyakazi waliodhaniwa kusababishwa na mbu hao.
"Kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya, walikuja wataalamu kwa lengo la kufanya utafiti kwenye eneo hilo waligundua kuwepo kwa mbu wengi aina ya Culex wanaosababisha ugonjwa wa matende, na mbu wachache aina ya Anopheles wanaosabisha malaria na Aedes aegypti wanaosababisha homa ya manjano" alisema Lyipyoga.
Alisema hata hivyo, wagonjwa wa matende bado hawajagundulika kuongezeka kutoka na kuwepo kwa wingi kwa mbu hao kwani huchukua muda mrefu kugundulika.
Mbali na mikakati hiyo kupambana na mbu hoa walikuwa kero Muhimbili, hospitali hiyo imetumia shilingi 26 milioni kunyunyiza dawa ambayo hata hivyo haikufua dafu. Alisema mto huo ulikuwa umeziba kutokana na taka kuuziba na huku maji machafu yanayotoka kwenye kiwanda kimoja, hali iliyosababisha kuzaliana kwa mbu hao.

Alisema kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo la mbu kwenye bonde hilo, aliwataka wananchi wanaoishi pembezoni kuacha kutupa takataka ambazo ndizo chanzo cha tatizo hilo.
 
Jamani bonde la msimbazi lipo tangu lini? Na huu mlipuko wa mbu mbona hauna hata miezi 6?
Nadhani ni wakati muafaka kwa serikali kuwaambia wananchi ukweli badala ya kuzunguka hoja!
Tunajua kuna research iliyokuwa inafanyika kwenye bonde hilo, na wananchi tunahitaji kujua pia medicolegal impact yake!
 
Back
Top Bottom