Mbowe: Zitto kajiharibia mwenyewe kwa kurubuniwa na CCM

Mbowe: Zitto kajiharibia mwenyewe kwa kurubuniwa na CCM

Mbowe na Zitto ni weight mbili tofauti sana kisiasa ,tatizo la mbowe fedha ndo anaona kila kitu na ufadhili wa chama ndo unambeba
 
Zitto ndo tumaini la watanzania wanyonge piga kazi achana na wachanga tunawaelewa na wabinafsi na waroho wa madaraka
 
mkuu umenena zitto hata kama kalubuniwa bado hakutakiwa kufanyiwa hayo kama wanavyosema zitto bado ni mtu makini naimani hiyo kuteleza sio kuanguka.

usaliti ni laana mbaya sana .
 
Mbowe na Zitto ni weight mbili tofauti sana kisiasa ,tatizo la mbowe fedha ndo anaona kila kitu na ufadhili wa chama ndo unambeba

MH MBOWE ni kamanda wa ukweli sana , na ni tajiri wa kutupwa !
 
Zitto kuna mahali aliteleza kibinadamu. Anauwezo mkubwa,anasifa na nini,ila kuna sehemu alikosea hesabu kiroho safi tuu ajitazame upya. Mnaompa kichwa hamumjengi na wala sio afya kisiasa hasa upande wake.
 
Jamaa hajawahi kanusha kusaidiwa na Mbowe mpaka kesho. Nahisi Mbowe anamengi juu ya mwanae Zitto kamsitiri tuu kibusara ndio uzazi. Mtoto akikosea hatumkani ila tunasimamia nidhamu tuu.
 
Aliyekitoa chama mbali ni aliyekianzisha tu kama ulikikuta kipo mbali ungeenda kilichokaribu....chama ni taasisi yenye mfumo,muundo na mambo mengine yanayofanya kijiongoze ...umbali au ukaribu Wa ulipokikuta sio credit ya taasisi kukupa utofauti
 
Sijawahi kuona Mchagga katili na asiye na shukrani kama MBOWE, Pamoja na wanayomtuhumu nayo ZITTO yote , bado alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu kwa kuwa ZITTO amekitoa Chama mbali sana. Ndiyo anayea kambi hivyo huyo MBOWE anachezea watu wa KIGOMA.

uchaga umekujaje hapo mamayo zako!
 
Ndugu unakosea sana kumfananisha zitto na hao watu hapo nadhani moyo wako unajua ukweli,zitto amekuwa chachu ya mabadiliko Tanzania nzima vijana wengi wanaobwabwaja humu walikuwa inspired na zitto kuingia kwenye siasa hao kina sugu wamekuta njia imeshafagiliwa wao ilikuwa ni kupita tu na kwa jimbo kama Mbeya ilikuwa hata likigombea jiwe ilimradi tu ni Cdm lazima lingeshinda.JF IMEKUWA SIYO SEHEMU YA GREAT THINKERS WATOTO MMEKUWA WENGI SANA

Uwe na heshima Vianelly Vian ...si lazima ukashifu kutoa hoja. Sijabeza mchango wa Zitto kwenye siasa za Tanzania hasa kwa vijana, nilikuwa nikisoma Muhimbili wakati Zitto anasoma Mlimani, na yeye ndiye aliyeni'inspire' kujiunga na Chadema (nilishawahi kukiri hili hapa JF), lakini hilo haliondoi ukweli kuwa amejiwekea 'price tag', amenunulika, na amekuwa msaliti...si kwa chama tu...pia kwa sisi aliotuinspire, vijana wa Tanzania, na pia waTanzania wamependao mabadiliko. Inawezekana kina Sugu wamekuta njia imeshafagiliwa ndio, lakini imefagiliwa na nani!? Si Zitto pekee, na kama Zitto akidai credit za kukifagilia chama...Slaa atadai nini!? Na kama hao waliokuta njia imefagiliwa wanawork hard kuimaintain safi wakati mfagizi yuko busy kurudisha takataka njiani...nani ana thamani kwetu!?
 


Akifafanua zaidi kuhusu lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake na chama anachokiongoza, hususan kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, Mbowe alisema kuwa kamwe hawezi kumzibia kwa kuwa ndiye aliyemtafuta na kumuingiza katika siasa akiwa kijana mdogo.

Labda nilazimike kutoa ufafanuzi huu ili muelewe ukweli wake. Mimi ndiye nilimwingiza Zitto katika siasa akiwa kijana madogo, nilimwita akitokea masomoni Ujerumani, kisha nikamshauri akagombee ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini, nikampa pesa na gari ambalo mpaka sasa hajalirudisha," alifafanua.


Akizungumzia usaliti wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Dk. Aman Kabourou, alisema kwamba akiwa kijana mwanzilishi wa chama hicho, alishiriki kikamilifu kumpigania Dk. Kabourou kumleta nchini na hatimaye kugombea ubunge mwaka 1993 katika uchaguzi mdogo.

"Nyinyi vijana wengi inawezekana hamjui hiki chama kilianza vipi katika mkoa huu. Mimi nilishiriki kikamilifi kumwezesha Dk. Kabourou kuwania ubunge wa Kigoma Mjini kwa kutoa nauli ya kumleta kutoka Uingereza alikokuwa akiishi, yeye na mkewe na pia nikampa pesa kumwezesha kufanya kampeni, leo hii mnanihukumu Mbowe," aliongeza.

Chanzo:Tanzania daima

haya maneno mazito sana haya, wapi #TeamZitto

CC: omarilyas

Vipi jamaa yako atarudisha lini gari la watu?
 
Last edited by a moderator:
watu wa kigoma ni kawaida yao historia hii hapa:mwaka1962 shehe Amri abed karuta aliwahi kufukuzwa uwaziri na nyerere 1996 mpologomi alifukuzwa unaib waziri wa fedha mbwiliza alifukuzwa ukuu wa mkoa wa kilimanjaro daniel nsazugwanko akarubuniwa na maccm kifu gulam hussen katimkia ccm kufata ukuu wa wilaya ya mbalali kafulila si mnamjua mwl. wa siasa dr.kabour mnamjua Ngenda kirumbi alikuwa katibu wa ccm mkoa wa dar na katibu wa makatibu wa ccm tz nzima alifukuzwa mnamshangaa zzk poleni
 
Kuwapa gari au hela ya Kampeni haimanishi kwamba ndio uwafunge midomo kwamba kwa sababu uliwapa hela za kampeni hutaki wakukosoe ukienda kombo umejifanya wewe ndiye afisa manunuzi wa chama na unajilipa isivyotakiwa watu wakuangalie tu kwa sababu uliwapa hela ya kampeni na gari?? au ndio unajilipa zile hela ulizotoa kwa ajili ya kampeni na lile gari?? Hutaki wenzako wagombee uenyekiti wa chama taifa eti kwa sababu tu uliwapa hela ya kampeni na ukawapa na gari! OK sasa lini utaruhusu na wengine wagombee na ya uenyekiti Taifa bila mizengwe?? au hadi urudishe hela uliyotoa kwa ajili ya Kampeni na gari??
 
Zitto:

“Naumia sana, lakini naamini ipo siku ama nikiwa hai au nimekufa watu wataujua ukweli,” alisema mwanasiasa huyo kijana aliyepata umaarufu kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja.

Alisema, akiwa mwenyekiti wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu (Daruso) yeye na mwenyekiti wake ndiyo waliokijenga chama wakati huo Mbowe akiwa mbunge wa Hai.

Alisema wakati huo Mbowe alikuwa akienda chumbani kwake kusuka mikakati ya kuiinua Chadema na kwamba walikuwa wakila chips pamoja na wakati mwingine kwenye klabu ya usiku ya Bilicanas inayomilikiwa na Mbowe.

“Wakati mwingine naangalia, naumia sana. Wakati tunafanya hayo yote wengine walikuwa CCM, wengine walikuwa wafanyabiashara, lakini sasa ndiyo wana sauti katika chama,” alisema Zitto.

Zitto alisema kuwa wakati huo walikuwa na kampeni yao waliyoiita ‘Real Madrid’ ambayo ilikuwa na lengo la kuingiza kila mwanasiasa bora katika chama chao.


My take: CCM ndo wapambe wenyewe waliofanikiwa kuufitinisha uhusiano huu.
 
Usaliti ni sumu kubwa sana ZZK isiyosamehewa.Ushauri wa bure ni uachane na siasa uende ukafundishe tu.Taifa lilishamezwa na maharamia mafisadi.Mwenyezi Mungu analikomboa hili Taifa kupitia wapinzani
 
Una uhakika gani kama hayo maneno kayasema Mbowe? Hayo yameandikwa na Tanzania Daima ikidai imemnukuu Mbowe. Kama nia yako ni kupata kauli ya Zitto ungeanza na Mbowe aje ku comfirm taarifa ya Tanzania Daima

mkuu natumia simu,hivyo napenda kukupa like ya mdomo,nimeipenda hii.
kabla ya yote mh. mbowe anatakiwa athibitishe kama haya yaliyoandikwa na gazeti ambalo ni mchekeshaji wa mfalme ni sahihi kweli ama si sahihi,halafu ndio tujue pa kuanzia maana hili gazeti limekuwa na mambo ya mpiga zumari....
 
Back
Top Bottom