Mbowe: Zitto kajiharibia mwenyewe kwa kurubuniwa na CCM

Mbowe: Zitto kajiharibia mwenyewe kwa kurubuniwa na CCM

Anachonifurahisha Zitto Kabwe, ni wanampiga majunu weeee, yeye kimya. Ukimya ni jibu zuri sana. Pamoja na majungu yote hayo bado nyota yake katika utendaji, uzalendo wake kwa Taifa letu vimeendelea kuwa dhahiri. Zitto Kabwe ndo mwanasiasa pekee amepigwa mishale mingi sana.

Kinachosikitisha ni kwamba watu waliandaliwa kudanganywa na mkakati wa Uongo ulipokamilika wakadanganywa na wakakubali. Kukubali kudanganywa ni uzembe wa kutokuwa tayari kufikiri na kufanya analysis ya uongo unaoendelea kusambazwa. Na umweli ni kwamba, wakati viongozi wengine wa vyama vya siasa umaarufu wao ukishuka, wa Zitto Kabwe unaongezeka.

Zitto ndo mwanasiasa pekee ambaye amejijengea jina na umaarufu ndani na nje ya Tanzania. Kile chama kitaharibiwa siyo na Mbowe wala Dr Slaa, bali Lema, Kilewo, Lissu na Msigwa. Hawa ndo wanaonekana washauri wakuu wa viongozi wa juu wa chama. Wanawashauri ujinga kujijengea umaarufu.
 
SLAA naye akasema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa hawana tatizo na ZITTO, ni kijana wao. Nani mkweli? CHADEMA acheni kutudanganya, muombeni msamaha ZITTO.

UKISOMA ALICHOSEMA MBOWE PIA, HAJASEMA ANA TATIZO NA ZITTO, na wala hawezi kumzibia, bali anasimamia principles za chama na katoa historia nzuri

I think mngemshauri Zitto amalizane na wazee wake waliomlea kabla hajakua kiuchumi

msimpotoshe zitto wakati nyie mna kazi zetu, hata kama haziingizi kipato kikubwa... hizi keyboards zisiwafanye kuwa na courage ya kumpotosha kijana mwenzenu
 
Ndugu unakosea sana
kumfananisha zitto na hao watu hapo nadhani moyo wako unajua
ukweli,zitto amekuwa chachu ya mabadiliko Tanzania nzima vijana wengi
wanaobwabwaja humu walikuwa inspired na zitto kuingia kwenye siasa hao
kina sugu wamekuta njia imeshafagiliwa wao ilikuwa ni kupita tu na kwa
jimbo kama Mbeya ilikuwa hata likigombea jiwe ilimradi tu ni Cdm lazima
lingeshinda.JF IMEKUWA SIYO SEHEMU YA GREAT THINKERS WATOTO MMEKUWA
WENGI SANA

sugu alishinda kwa sabbu ya Zitto!? nyinyi wapambe wanafiki ndo mnaompotosha Zzk
 
Akili nyingine kweli si akili!

Just imagine, report ya CAG inawataja viongozi wawili wa upinzani kuhusua na ukwapuaji wa RUZUKU ya Chama Tawala (CCM)

Tulia sindano ipenye. Ndo maana hamtaki ripoti isomwe
 
mbowe3-300x169.jpg

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuijua historia ya mageuzi ya Mkoa huo ili kuepuka kuwalaumu viongozi wanaosimamia vyama hivyo pindi wanapochukua maamuzi magumu.

Alisema wananchi wengi wamekuwa wakishabikia na kuwahukumu viongozi hao bila kuangalia chimbuko la vyama hivyo, vilikotoka na hatimaye kufikia hatua vilipo sasa hususan katika mkoa huo ambao umekuwa chimbuko la mabadiliko.

Akijibu swali lililoulizwa na mtu ambaye alijitambulisha kwa jina la Cheche wa Cheche, katika mkutano wa hadhara wa ‘Oparesheni Delete CCM’, uliofanyika kwenye kijiji cha Mnanila Manyovu mkoani hapa jana, Mbowe alisema Mkoa wa Kigoma ulizalisha viongozi wengi maarufu katika mageuzi.

Alisema utumishi ndani ya chama hicho haupimwi kutokana na mtu kutoka mkoa gani, bali hupimwa kutokana na ujasiri, uwezo wa mtu na kamwe kiongozi makini hawezi kumpiga vita mtu kwa sababu ya kabila au dini yake.

Akitoa mfano wa viongozi waliotegemewa na wanachi wa mkoa huo katika kuendeleza mageuzi, Mbowe, alisema Daniel Nsanzugwanko, Aman Kabourou na Zitto Kabwe walionyesha umahiri wao katika kuongoza vyama vya siasa enzi zao kabla ya kurubuniwa na kuvisaliti.

Akifafanua zaidi kuhusu lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake na chama anachokiongoza, hususan kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, Mbowe alisema kuwa kamwe hawezi kumzibia kwa kuwa ndiye aliyemtafuta na kumuingiza katika siasa akiwa kijana mdogo.

Labda nilazimike kutoa ufafanuzi huu ili muelewe ukweli wake. Mimi ndiye nilimwingiza Zitto katika siasa akiwa kijana madogo, nilimwita akitokea masomoni Ujerumani, kisha nikamshauri akagombee ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini, nikampa pesa na gari ambalo mpaka sasa hajalirudisha,” alifafanua.

Alisema Zitto ndiye aliyetia mchanga kitumbua chake kwa kusaliti chama kutokana na kukubali kurubuniwa na viongozi wa CCM, jambo ambalo lisingelivumiliwa ndani na nje ya chama.

Huku akishangiliwa na umati mkubwa uliofurika katika Uwanja wa Community Centre mjni Kigoma, Mbowe alisema kuwa, atahakikisha anakilinda chama hicho kwa gharama yoyote bila kumwonea mtu ili kukijengea imani kwa watanzania.

Akizungumzia usaliti wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Dk. Aman Kabourou, alisema kwamba akiwa kijana mwanzilishi wa chama hicho, alishiriki kikamilifu kumpigania Dk. Kabourou kumleta nchini na hatimaye kugombea ubunge mwaka 1993 katika uchaguzi mdogo.

“Nyinyi vijana wengi inawezekana hamjui hiki chama kilianza vipi katika mkoa huu. Mimi nilishiriki kikamilifi kumwezesha Dk. Kabourou kuwania ubunge wa Kigoma Mjini kwa kutoa nauli ya kumleta kutoka Uingereza alikokuwa akiishi, yeye na mkewe na pia nikampa pesa kumwezesha kufanya kampeni, leo hii mnanihukumu Mbowe,” aliongeza.

Alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa anampiga vita Zitto, jambo ambalo si kweli kwa kuwa amemlea, amekula na kulala nyumbani kwake kabla hajakua kiuchumi.

Jana, Mbowe alifanya ziara yake katika jimbo la Manyovu, Kigoma mjini katika uwanja wa Community Centre Mwanga, Munawila na Mahembe ambako aliendelea kuwasisitiza wananchi kuwapa dola upinzani kwa kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Chanzo:Tanzania daima

Duuu bulaza mbowe ana ukwasi tuuuu
 
Anachonifurahisha Zitto Kabwe, ni wanampiga majunu weeee, yeye kimya. Ukimya ni jibu zuri sana. Pamoja na majungu yote hayo bado nyota yake katika utendaji, uzalendo wake kwa Taifa letu vimeendelea kuwa dhahiri. Zitto Kabwe ndo mwanasiasa pekee amepigwa mishale mingi sana.

Kinachosikitisha ni kwamba watu waliandaliwa kudanganywa na mkakati wa Uongo ulipokamilika wakadanganywa na wakakubali. Kukubali kudanganywa ni uzembe wa kutokuwa tayari kufikiri na kufanya analysis ya uongo unaoendelea kusambazwa. Na umweli ni kwamba, wakati viongozi wengine wa vyama vya siasa umaarufu wao ukishuka, wa Zitto Kabwe unaongezeka.

Zitto ndo mwanasiasa pekee ambaye amejijengea jina na umaarufu ndani na nje ya Tanzania. Kile chama kitaharibiwa siyo na Mbowe wala Dr Slaa, bali Lema, Kilewo, Lissu na Msigwa. Hawa ndo wanaonekana washauri wakuu wa viongozi wa juu wa chama. Wanawashauri ujinga kujijengea umaarufu.

Zitto amekulia kwenye familia ya kifikara. Temna mama ake alikuwa na peaa ya kuunga unga tu.

Mbowe ndio kamfikisha hapo alipo ila kwa kuwa wayz huwa hatuna shukran ndio aina ya viongozi wetu.

Mara ngapi Zitto kamrushia makombora Mbowe?
 
Anachonifurahisha Zitto
Kabwe, ni wanampiga majunu weeee, yeye kimya. Ukimya ni jibu zuri sana.
Pamoja na majungu yote hayo bado nyota yake katika utendaji, uzalendo
wake kwa Taifa letu vimeendelea kuwa dhahiri. Zitto Kabwe ndo mwanasiasa
pekee amepigwa mishale mingi sana.

Kinachosikitisha ni kwamba watu waliandaliwa kudanganywa na mkakati wa
Uongo ulipokamilika wakadanganywa na wakakubali. Kukubali kudanganywa ni
uzembe wa kutokuwa tayari kufikiri na kufanya analysis ya uongo
unaoendelea kusambazwa. Na umweli ni kwamba, wakati viongozi wengine wa
vyama vya siasa umaarufu wao ukishuka, wa Zitto Kabwe unaongezeka.

Zitto ndo mwanasiasa pekee ambaye amejijengea jina na umaarufu ndani na
nje ya Tanzania. Kile chama kitaharibiwa siyo na Mbowe wala Dr Slaa,
bali Lema, Kilewo, Lissu na Msigwa. Hawa ndo wanaonekana washauri wakuu
wa viongozi wa juu wa chama. Wanawashauri ujinga kujijengea
umaarufu.

msimpotishe zitto, ukweli ni kwamba umaarufu wake umeathiriwa sana na haya yaliyotokea
 
Ninatarajia kuleta uzi maalum kushauri Zitto, katika uzi huo nitaandika hata niliyowahi kumshauri huko nyuma.
 
Hakuna ubishi 'Zitto AMETOKA na chama mbali' (sio amekitoa chama mbali) na mchango wake kwa Chadema ni mkubwa mno, lakini hilo halihalalishi usaliti alioufanya. Chadema si chama strong Kigoma, NCCR is..miaka yote ambayo Zitto amekuwa Chadema ameshindwa kukifanya Chama kuwa strong Kigoma kama ambavyo kina Mbowe wamefanya chama kuwa strong Kilimanjaro, Slaa alivyofanya chama kuwa strong Arusha na Karatu, au hata new-comer Sugu alivyofanya chama kuwa strong Mbeya. Hakuna haja ya Mbowe kuwa na shukrani kwa Zitto, alipaswa kutimiza wajibu wake kwa chama na kwa waTanzania...sijawahi kuona sehemu Mbowe akiwashukuru Sugu, Mnyika, Mdee, Msigwa, Arfi, Lissu...why Zitto ashukuriwe!?

Hii ni comment bora kwangu kwa kufungia mwaka, wanakazi ya ziada wengine kuipindua ili niipe uzito comment nyingine. pokea LIKE KUBWA MKUU
 
Uwe na heshima Vianelly Vian ...si lazima ukashifu kutoa hoja. Sijabeza mchango wa Zitto kwenye siasa za Tanzania hasa kwa vijana, nilikuwa nikisoma Muhimbili wakati Zitto anasoma Mlimani, na yeye ndiye aliyeni'inspire' kujiunga na Chadema (nilishawahi kukiri hili hapa JF), lakini hilo haliondoi ukweli kuwa amejiwekea 'price tag', amenunulika, na amekuwa msaliti...si kwa chama tu...pia kwa sisi aliotuinspire, vijana wa Tanzania, na pia waTanzania wamependao mabadiliko. Inawezekana kina Sugu wamekuta njia imeshafagiliwa ndio, lakini imefagiliwa na nani!? Si Zitto pekee, na kama Zitto akidai credit za kukifagilia chama...Slaa atadai nini!? Na kama hao waliokuta njia imefagiliwa wanawork hard kuimaintain safi wakati mfagizi yuko busy kurudisha takataka njiani...nani ana thamani kwetu!?

It's too low ..
Keeping on blaming ... Usaliti.. Usaliti... Without clear evidence is silly ..
We're is a GT
 
Zitto kaeni mmalize hu mgogoro, mbona naona kama nyota yako ni kuchezea cdm
 
Zitto ni msaliti kama kawaida ya watu wa kigoma hakuanza yeye,alikuwepo katibu mkuu wa chadema dr wilbrod kaburu,kuna mwingine nsanzaguako wa NCCR mageuzi wote wakigoma walirubuniwa na ccm na kupewa vyeo wakasaliti vyama vyao kigoma njaa sana.

Hapana, hao watu watatu hawawezi kuwa na tabia zinazowawakilishi tabia za watu wote wa Kigoma. Usaliti ni tabia ya mtu binafsi hakuna kinasaba kinachobeba usaliti kwenye vimengenya vya binadamu...watalaamu watafafanua zaidi hili.
 
hawa watu wa kigoma wana matatizo gani hawa,,

Acha maneno ya kijinga. Mtu kuwa msaliti ni akili na tabia yake, regardless anatoka sehemu gani. Wako watu wengi wamesaliti vyama vyao na wanatoka mikoa tofauti. Pamoja na hao wachache kurubuniwa bado mkoa wa kigoma uko juu ktk mageuzi Kulinganisha na mikoa mingine. Wahukumu waliosaliti, lakini usihukumu watu wote wa mkoa .
 
Sijawahi kuona Mchagga katili na asiye na shukrani kama MBOWE, Pamoja na wanayomtuhumu nayo ZITTO yote , bado alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu kwa kuwa ZITTO amekitoa Chama mbali sana. Ndiyo anayea kambi hivyo huyo MBOWE anachezea watu wa KIGOMA.

Ungeandika tu jina "MBOWE" ingetosha hao "WACHAGA" achana nao
 
Lazima kutakuwa na majibu hapa...
Ngoja kwanza niingie mzigoni... nitakuwa kuyasoma baadae
 
bila ya kuwa upande wa mbowe au zitto Mimi nataka kujua ukweli kuhusu tuhuma mnazozielekeza kwa zitto.

Niseme kuwa huwezi jua zitto anaweza kweli akawa ametumika na ccm au ikawa ni uongo.

Sasa Mimi ninachosema mbowe asitupumbaze, ni kwamba toka waanze kumtuhumu zitto anatumiwa na ccm hawajawahi kusema zitto anatumikaje, na nani, na lini kwa ushahidi.

Ninachokumbuka zitto alivuliwa uongozi kwa tuhuma ya kuandaa mkakati wa mabadiliko ya 2013 ulioandaliwa na kitila na mwigamba. mbona tuhuma za yeye kutumika na ccm hazijatolewa kwa njia ya maandishi na kila mmoja akajionea? mbona ni mashambulizi ya majukwani na sio official?

suala la mbowe kumsaidia zitto ndio kigezo cha yeye kumnanga kila siku kwa tuhuma zisizo na ushahidi? zitto alisema vyama vyote havijakaguliwa na CAG chama kikasema zitto muongo cdm imeshakaguliwa, sasa huu ukaguzi uliofanywa na CAG kwenye vyama vyote chadema haikuhusika kwakuwakuwa chama kilishakaguliw,?

tukiachana na taarifa iliyowekwa humu zitto alivyokuwa anapokea pesa toka mwaka 2008.ambapo Katibu mkuu, mwasisi na mkurugnzi wa habaari walikanusha kuwa walaka ule hawaufahamu, Nani mwenye ushahidi wa jinsi zit to anvyotumika.
 
Back
Top Bottom