Mbowe: Zitto kajiharibia mwenyewe kwa kurubuniwa na CCM

Mbowe: Zitto kajiharibia mwenyewe kwa kurubuniwa na CCM

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,703
Reaction score
140,407
mbowe3-300x169.jpg

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuijua historia ya mageuzi ya Mkoa huo ili kuepuka kuwalaumu viongozi wanaosimamia vyama hivyo pindi wanapochukua maamuzi magumu.

Alisema wananchi wengi wamekuwa wakishabikia na kuwahukumu viongozi hao bila kuangalia chimbuko la vyama hivyo, vilikotoka na hatimaye kufikia hatua vilipo sasa hususan katika mkoa huo ambao umekuwa chimbuko la mabadiliko.

Akijibu swali lililoulizwa na mtu ambaye alijitambulisha kwa jina la Cheche wa Cheche, katika mkutano wa hadhara wa ‘Oparesheni Delete CCM', uliofanyika kwenye kijiji cha Mnanila Manyovu mkoani hapa jana, Mbowe alisema Mkoa wa Kigoma ulizalisha viongozi wengi maarufu katika mageuzi.

Alisema utumishi ndani ya chama hicho haupimwi kutokana na mtu kutoka mkoa gani, bali hupimwa kutokana na ujasiri, uwezo wa mtu na kamwe kiongozi makini hawezi kumpiga vita mtu kwa sababu ya kabila au dini yake.

Akitoa mfano wa viongozi waliotegemewa na wanachi wa mkoa huo katika kuendeleza mageuzi, Mbowe, alisema Daniel Nsanzugwanko, Aman Kabourou na Zitto Kabwe walionyesha umahiri wao katika kuongoza vyama vya siasa enzi zao kabla ya kurubuniwa na kuvisaliti.

Akifafanua zaidi kuhusu lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake na chama anachokiongoza, hususan kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, Mbowe alisema kuwa kamwe hawezi kumzibia kwa kuwa ndiye aliyemtafuta na kumuingiza katika siasa akiwa kijana mdogo.

Labda nilazimike kutoa ufafanuzi huu ili muelewe ukweli wake. Mimi ndiye nilimwingiza Zitto katika siasa akiwa kijana madogo, nilimwita akitokea masomoni Ujerumani, kisha nikamshauri akagombee ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini, nikampa pesa na gari ambalo mpaka sasa hajalirudisha," alifafanua.

Alisema Zitto ndiye aliyetia mchanga kitumbua chake kwa kusaliti chama kutokana na kukubali kurubuniwa na viongozi wa CCM, jambo ambalo lisingelivumiliwa ndani na nje ya chama.

Huku akishangiliwa na umati mkubwa uliofurika katika Uwanja wa Community Centre mjni Kigoma, Mbowe alisema kuwa, atahakikisha anakilinda chama hicho kwa gharama yoyote bila kumwonea mtu ili kukijengea imani kwa watanzania.

Akizungumzia usaliti wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Dk. Aman Kabourou, alisema kwamba akiwa kijana mwanzilishi wa chama hicho, alishiriki kikamilifu kumpigania Dk. Kabourou kumleta nchini na hatimaye kugombea ubunge mwaka 1993 katika uchaguzi mdogo.

"Nyinyi vijana wengi inawezekana hamjui hiki chama kilianza vipi katika mkoa huu. Mimi nilishiriki kikamilifi kumwezesha Dk. Kabourou kuwania ubunge wa Kigoma Mjini kwa kutoa nauli ya kumleta kutoka Uingereza alikokuwa akiishi, yeye na mkewe na pia nikampa pesa kumwezesha kufanya kampeni, leo hii mnanihukumu Mbowe," aliongeza.

Alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa anampiga vita Zitto, jambo ambalo si kweli kwa kuwa amemlea, amekula na kulala nyumbani kwake kabla hajakua kiuchumi.

Jana, Mbowe alifanya ziara yake katika jimbo la Manyovu, Kigoma mjini katika uwanja wa Community Centre Mwanga, Munawila na Mahembe ambako aliendelea kuwasisitiza wananchi kuwapa dola upinzani kwa kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Chanzo:Tanzania daima
 
Gazeti la Tanzania Daima leo limeripoti kuwa Mh.Mbowe akihutubia umati wa watu katika operesheni delete CCM Kigoma,amewaambia wananchi kuwa hawezi kumzuia Zitto katika harakati zake,ila akasisitiza kuwa Mh.Zito alirubuniwa mwenyewe na CCM.Mwenye taarifa kamili atuwekee

Sijawahi kuona Mchagga katili na asiye na shukrani kama MBOWE, Pamoja na wanayomtuhumu nayo ZITTO yote , bado alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu kwa kuwa ZITTO amekitoa Chama mbali sana. Ndiyo anayea kambi hivyo huyo MBOWE anachezea watu wa KIGOMA.
 
Nakuomba mkuu Zitto Kabwe uje hapa jukwaani kututhibitishia aliyo yasema mkuu MBOWE.
Ili kuondoa dhana potofu.
 
Last edited by a moderator:
Sijawahi kuona Mchagga katili na asiye na shukrani kama MBOWE, Pamoja na wanayomtuhumu nayo ZITTO yote , bado alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu kwa kuwa ZITTO amekitoa Chama mbali sana. Ndiyo anayea kambi hivyo huyo MBOWE anachezea watu wa KIGOMA.

Watu wa kigoma wananini kwani?
 
SLAA naye akasema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa hawana tatizo na ZITTO, ni kijana wao. Nani mkweli? CHADEMA acheni kutudanganya, muombeni msamaha ZITTO.

CDM ndio imwombe zzk msamaha kweli au yeye ndio yampasa kuomba msamaha kwa usaliti wa chama na taifa? Daima hakuna alie juu ya chama.
 
MBOWE katika ziara yake ya Kigoma alipata taabu sana alipokuwa jukwaani baada ya kukutana na zomea zomea kila alipokuwa akimgusa Zitto jukwaani,hali alivoina kuwa ni mbaya ikabidi aanze kumsifia Zitto na kubaki kusema kuwa Zitto alikosa subira tu. Mbowe akasema sina tatizo na Zitto ni kijana mweledi tena ninayemkubali sana ila zomea zomea haikukoma,alivoshuka jukwaani pindi anaongea na wake alikiri kiukweli Kigoma ni ya Zitto na taarifa nazopewa na watu wa Kigoma kusema tupo sawa huku ni unafiki sana nimejionea mwenyewe
Umemaliza au bado hadithi inaendelea?

Kama umemaliza hadithi hii kakufundisha nani?

Kakuambia ina maana gani?

.............Na hapa ndipo tumefikia mwisho wa kipindi chetu cha chei chei shangazi kupitia Radio Tanzania, Daslam.
 
Sijawahi kuona Mchagga katili na asiye na shukrani kama MBOWE, Pamoja na wanayomtuhumu nayo ZITTO yote , bado alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu kwa kuwa ZITTO amekitoa Chama mbali sana. Ndiyo anayea kambi hivyo huyo MBOWE anachezea watu wa KIGOMA.

Zzk amekitoa chama mbali ama chama ndo kimemtoa mbali??
Kat ya mbowe na zzk nani kakitoa chama mbali??
Nasktka sn team zzk hampendi kumwambia zzk ukweli, na ndo mana mbele atajuta sana.
 
SLAA naye akasema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa hawana tatizo na ZITTO, ni kijana wao. Nani mkweli? CHADEMA acheni kutudanganya, muombeni msamaha ZITTO.
Si mlisema Chadema itakufa ? Sasa huoni kuwa ndio inasonga mbele na yale makelele kwenye media kila uchwao huoni yamepita ? Spinner is no longer ...........
 
Sijawahi kuona Mchagga katili na asiye na shukrani kama MBOWE, Pamoja na wanayomtuhumu nayo ZITTO yote , bado alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu kwa kuwa ZITTO amekitoa Chama mbali sana. Ndiyo anayea kambi hivyo huyo MBOWE anachezea watu wa KIGOMA.

amekitoa wapi,na ilikua mwaka gani?zitto alikikuta chama na chama ndio kimemtangaza zitto na zitto amekiacha kikiendelea na makali yake
 
Sijawahi kuona Mchagga katili na asiye na shukrani kama MBOWE, Pamoja na wanayomtuhumu nayo ZITTO yote , bado alitakiwa kuwa na mshipa wa aibu kwa kuwa ZITTO amekitoa Chama mbali sana. Ndiyo anayea kambi hivyo huyo MBOWE anachezea watu wa KIGOMA.

Hii mambo ya kukitoa mbali chama ndio imeiua CCM,,,,! na mh,,zitto mwenyewe aliamini hivyo,,, ila nafasi bado ipo anaweza kuwaomba Radhi viongoz wenzake na wanachama akaendelea kwenye safari ndefu kujikwaa kupo chamuhimu kutambua ulupokosea
 
Back
Top Bottom